Saturday, March 16, 2013

SALAMA JABRI :TUONGOZE WATANZANIA KUMPATIA TREKTA KING MAJUTO

Watanzania tuyatafute matatizo yetu  na kuyatatua badala ya kuyasubiri na kuyafanya DILI.

Mzee Majuto, sisi wengi tunamfahamu kwa vichekesho vyake vyenye maadili na mafunzo kwa jamii yetu. King Majuto kwenye kipindi cha Mkasi, cha Salama Jabri (SO5E12-with Majuto:http://youtu.be/bmTuxMSmRMY) aliongea vizuri sana, na kilichonivutia zaidi katika maongezi yake, ni PAMOJA NA
KUSEMA ANAHITAJI TREKA ILI AWEZE KULIMA KISASA. Hili kwangu mimi ni wazo la kiutu uzima na la kizalendo sana, kama ambavyo amesema kwenye makala hii kuwa AMANI,UTULIVU NA UMOJA ni vitu vya msingi sana. Ukubwa kweli Jiwe, pengine angekuwa kijana kama mimi, angeomba kwanza gari la kifahari au hati miliki ya kazi yake, au pengine hata kuishia kulaumu serikali kama sio kukejeli wenzake. Akihojiwa, King Majuto (Amri Athumani) alisema  ".. umoja wetu, amani na utulivu lazima vibakie kuwa kipaumbele chetu cha kwanza. Naweza kusema kwa kujiamini kuwa filamu na vichekesho vyangu vimesaidia kuiunganisha Tanzania kila wakati nchi ilipoingia [katika mizozo]",(MAKALA: zaidi soma http://sabahionline.com/sw/articles/hoa/arti iliyoandaliwa na Deodatus Balile, Dar es Salaam Machi 14, 2013.)

Watanzania tunapenda zaidi kushabikia zaidi visivyo na umuhimu sana, yaliyo ya umuhimu huwa tunayasahau mpaka tudhulike,  na pengine ndio maana hata serikali pia huwa na kasumba ya namna hiyo. Kwa sababu wanaounda serikali ni Watanzania na wengi wao wana fikra za Kitanzania zaidi yaani za "KI-BONGO MEN" (sHaRo mILioNaiRE). RAI kwenu waandishi wa HABARI, TUONYESHENI NJIA YA KWELI, hakuna haja ya mtu kama majuto kupewa TREKTA na RAISI, MNAWEZA KUENDESHA KAMPENI NDOGO TU,tukamsaidia mzee majuto kupata TREKTA. Tusaidieni kuyafuata matatizo yaliko na kuyaweka bayana na kutuhamasisha kuyatatua badala ya kuyasubiri yatudhulu au yatokee, ndio muanze kutuhamisisha kutoa pole. Nafikiri, hili litatusaidia zaidi, na kuboresha huduma yenu kwetu watanzania. Hata hivyo, nawapongeza kwa hatua mliyonayo,maana hadi hapa tulipo ni juhudi zenu . Tunaishukuru na Serikali kwa kuendelea kutoa nafasi kwa vyombo vya habari kujimwagia uhuru pia,hii ina maananisha tuongeze nguvu kwenye kuyatafuta matatizo ya watanzania na kuyatatua, naamini hata serikali itazidi kuona umuhimu wa kuongeza uhuru wa vyombo vya habari badala ya kuupunguza kama dalili zinavyoonyesha.

Sio kwamba kila mtanzania aombe kusaidiwa na watanzania au mheshimiwa raisi, hapana, ila naamini mzee majuto mpaka kufikia kuongea vile (Mara Ya Tatu) atakuwa kapigana mpaka mwisho, na kwa mtazamo wangu, anastahili msaada kama huo,japo nisingependa kujibu swali la kwa nini naamini hivyo. Najua wengi watahoji kwa nini Mzee majuto na sio watanzania wengine wengi wenye hali ngumu kuliko yeye? Kwa kuwa ndio kawaida yetu kutafuta sababu za kuzuia jambo zuri lisifanyike badala ya kuboresha jinsi gani lifanyike kwa UBORA ZAIDI.

Kiongozi, anatoa mfano, badala ya kuiga tunataka aendelee kufanya yeye, raisi kusaidia baadhi ya watanzania ni kama mfano kwetu, na sio maana yake alazimike kuwasaidia wote. Sasa badala ya kukaa tunahoji kwa nini alimsaidia fulani na sio yule au huyu, ni vema tungeanza kwa kuangalia kama sisi hatuwezi kumuonyesha yeye kuwa alichofanya na sisi tumeelewa umuhimu wake na hivyo tunafanya pia. Vitendo hukidhi haja malidhawa kuliko maneno, naamini kwa kuanza kuongea kwa vitendo serikali yetu itatuelewa zaidi tunachohitaji kuliko kuongea kama MIMI, bila hata kuahidi nitatoa sh ngapi. Tusiseme serikali imetelekeza kilimo wakati sisi wenyewe hatuwajali hata kidogo wakulima wetu kwa vitendo, au tusiseme serikali haijali sanaa yetu wakati sisi ndio wa kwanza kuzipenda na kuzisifu kazi za nje ya nchi! Ifike wakati elimu itumike kuyatafuta matatizo na kuyatatua badala ya kuyasubiri na kuyafanya ndio DILI.

KAULI MBIU KILIMO KWANZA, WAKATI FIKRA ZETU BURUDANI KWANZA,
wapi na wapi bwana?

0 comments:

Post a Comment