Home »
» Kama "Mapera",Fikra hizi nazo Feki!
Monday, December 16, 2013
Zamani, Tukuyu-MBEYA kulikuwa na vyakula
na matunda mbalimbali pengine kuliko leo. Kulikuwa
na aina ya “MAPERA” iliyofahamika kwa jina la “KALUNGA-MUNYU”. Mtu alikuwa hanunui MAPERA, zaidi watoto waliyachezea kama wachezeavyo GOLORI watoto leo
(Kama Wapo). Mapera yalikuwa na radha Fulani iliyokuwa kati ya CHUMVI,
LIMAO, ACHALI, SUKARI, ASALI na vitu vya namna hii. Na kwa kweli kupata
PERA la KALUNGA-MUNYU ilikuwa ni bahati sana! Haikuwa rahisi kula zaidi ya KALUNGA MUNYU 10, katika miaka 15.
LEO,
MAPERA yanauzwa Tukuyu, na si rahisi kuuziwa KALUNGA-MUNYU.
Kupata MAPERA yakiwa yameivia VICHAKANI AU MITINI,imekuwa tabu kidogo,
maana watu mapema wamekwisha “JISEVIA”. Hata uende sehemu za VIJIJINI
zaidi,si rahisi kupata “PERA ORIJINO” na
KALUNGAMUNYU,ndio kabisa huwezi kupata. MAPERA pia yamekuwa FEKI kama
ambavyo tuonavyo vitu vingine vingi nyakati hizi.
Kama kuna
kitu kinadumu DUNIANI huwa ni MABADILIKO, hatuwezi kuyakataa. LAKINI
mabadiliko mengi yatokanayo na maendeleo DUNIANI yanaonekana kuambatana
na kuondoa UBORA na UASILI wa DUNIA na VIUMBE vyake, tukiwemo BINADAMU.
UBORA WA UASILI unaondoka NA unakuja UBORA FEKI yaani UBORA WA
KUTENGENEZWA. Tunaweza kuliona hili, si kwenye VYAKULA TU, bali hata
katika MIILI na AFYA zetu. Kumekwishaanza maneno kuwa karibia tutaanza
kupata MVUA ya kutengenezwa,hivyo pengine tutarajie mengi yatokanayo na
maendeleo YAO, ambayo hasa ndio mwanzo wa kupungua kwa UBORA WA ASILI.
Mfano mzuri ni ongezeko la wasomi na UBORA WA ELIMU, ni kama FEKI
hivi.
YOTE tisa, KUMI ni KUPOTEA kwa
UBORA WA ASILI WA FIKRA ZETU.Ni kama hata FIKRA ZETU ZINAKUWA KAMA
ZINATENGENEZWA. Kila iitwayo siku, watu tunazidi, kuamini kuwa yale
MAZURI, ambayo tumeagizwa na MUNGU au WAZAZI, kuwa hayawezekani,ila yale
yatokanayo na maendeleo YAO, sisi huona ndio hayakwepeki.Hatuyaamini
kabisa yetu, na kukumbatia ya wenzetu, hata tuyaonapo kuwa yanatudhulu.
Eti! Sababu KUU ni UTANDAWAZI au NGUVU YA SOKO HURIA. HIZI sababu nazo
sio FEKI kweli?
Kila ukimuuliza MTU kwa nini anafanya HIKI AU
KILE, jibu ni NDIO UTANDAWAZI UNAVYOTAKA. Hata haya niyasemayo,nayo
nahisi kama ni yatokayo na FIKRA ZENYE UBORA FEKI. Na pengine msomaji
nawe utayasoma kwa FIKRA ZENYE UBORA FEKI, na kuishia kupuuzia ukiamini
KILA FEKI NI FEKI na kubaki na FIKRA FEKI. Huo ndio mwelekeo wetu kwa
sasa,TUNA MAMBO MENGI FEKI,TUNA WATU WENGI FEKI, TUYAONAYO MENGI NI FEKI,
TUYASOMAYO NI FEKI,TUYATENDAYO NI FEKI, TUYASIKIAYO FEKI,TUYASEMAYO NI
FEKI,…………FEKI!
Tunahitaji FIKRA ZENYE UTAMADUNI WA UBORA,
kuweza kutambua UBORA HASA NA FEKI ,ili walau kuweza kupunguza madhara
ya UFEKI unaotuzunguka katika maisha ya kila siku.
0 comments:
Post a Comment