Friday, December 20, 2013

SIMBA ACHENI UYANGA, WATANI YANGA MAJANGA



1
Hao hasa ndio yanga, Kwao ndio kujipanga.
Okwi sifa sitapinga, Tano wakumbuka Yanga.
Wakongo waende yanga, Nonda alivyowapanga.
Wageni Yanga mapanga, Kuwamaliza wachanga.
Lengo kubwa lao Yanga, Eti Simba kuwatwanga.
Kelele leo za Yanga, Okwi waona Mganga.
SIMBA ACHENI UYANGA, WATANI YANGA MAJANGA
2
Wageni waende Yanga, Kwetu Simba si Uganga.
Wageni Yanga Uganga,Simba tano kutufunga.
Mogela aliwaganga, Hakupenda kutufunga?
Kenya haikuwaganga, Uganda watawaganga?
Waghana sio waganga? Kagame mkatufunga.
Nurdini hakuwaganga, Chuji ameshatufunga?
Ngasa acheza Kiyanga, Simba aweza ifunga.
SIMBA ACHENI UYANGA, WATANI YANGA MAJANGA
 3
Simba kweli kama Yanga, Japo yanga ni majanga.
Uzalendo zero yanga. Pesa nyingi na Ujinga,
Usajili wa kijinga, Lengo Simba kuifunga.
Acheni saka waganga, Mchawi wenu Ujinga.
Sasa eti wajipanga, Mbeya City Kuifunga.
CAF Villa yawafunga, Enyimba Mtaifunga?
SIMBA ACHENI UYANGA, WATANI YANGA MAJANGA
4
Ujinga watani Yanga, Uswahili wawafunga.
Sio Simba si wajinga, Mmetuzidi Ujinga.
Jangwani Hamujajenga,Bora ya wetu ujinga.
Miaka nane mwafunga, Pesa lukuki ni Yanga.
Makabati mmefunga, Hatua mbili Majanga.
Kagameni mwatufunga, Ndio mwisho wenu Yanga.
SIMBA ACHENI UYANGA, WATANI YANGA MAJANGA
 5
Simba yangu sio Yanga, Japo tunao Uyanga.
Mwaga hela kama Yanga, Misri tunawafunga.
Sita kwao watufunga, Saba nyumbani twafunga.
Mpira kweli si chenga, Msingi hasa kufunga.
Simba ni noma kwa chenga, Magoli bora twafunga.
Soka Simba, Mbio Yanga, Bora goli ndio Yanga.
SIMBA ACHENI UYANGA, WATANI YANGA MAJANGA
6
Haka katimu ka Yanga, Yangu Simba kaifunga?
Lunyamila kweli Yanga, Hata Simba kuifunga.
Kizota sibishi Yanga, Kalimagonga ni Yanga.
Chambua  alitufunga,Bila mamia waganga.
Homa la jiji Mganga?, Na Simba alitufunga.
Yanga rudieni Yanga, Tupeni Yanga majanga
SIMBA ACHENI UYANGA, WATANI YANGA MAJANGA
 7
Nje chachu sitopinga, Wageni sifa Ujinga.
Simba acheni Uyanga, Simba yangu sio Jinga.
Zambia tuliporinga, Nani mgeni mganga?
Pawasa Aseke ifunga, Ngapi wakongo waganga?
Matola kuto kufunga, Na Masha hawakulonga!
Simba acheni ujinga, Kuiga mambo ya Yanga.
SIMBA ACHENI UYANGA, WATANI YANGA MAJANGA
 8
Bongo leo ni majanga, Soka katawala Yanga.
Nchini kuna ujinga, Ukweli tunaupinga.
Fikira PEVU za Yanga, Yetu Simba Kuifunga.
Kweli Kandambili Yanga, Kichawi unatufunga.
Uongozi wote Yanga, Macho Simba kuifunga.
Tanzania mwembeyanga,Soka mwisho la mchnga.
SIMBA ACHENI UYANGA, WATANI YANGA MAJANGA







Related Posts:

  • NYERERE BABA WA TAIFA WA KUJIVUNIA ulius Nyerere pictured on January 31, 1985 in Dar es Salam, Tanzania. PHOTO | FILE  NATION MEDIA GROUP "Nadhani hakupaswa Kung'atuka" Nilibahatika kukutana na (BIBI Theresa) ambaye alitem… Read More
  • TQM FOR TANZANIAN EDUCATION QUALITY IMPROVEMENT Normal 0 false false false EN-US X-NONE X-NONE MicrosoftInternetExplorer4 … Read More
  • "Penye UONGO, UKWELI pia HUJITENGA"Baada ya kuona maswala ya SIASA siyaelewi kabisa (Hasa kwenye mchakato wa katiba), nikaona nifungue kidogo Falsafa na Sayansi ya mambo ya Kisiasa. Nikajifunza mengi tu na kwa kifupi, nikaona kuwa mambo yahusuyo taratibu tuliz… Read More
  • SABUNI BORA TOKA TUKUYU-RUNGWE, TANZANIA.  Photo By Hussein Mjasiriamali AZA HERBAL MEDICATED SOAP. Ni sabuni ya asili iliyotengenezwa kutumia vitu vya asili kama tunda la PARACHICHI. Ndani ya tunda hili kuna maji kiasi kidogo sana ukilinganisha na matu… Read More
  • SIMBA UJASIRI NDIO SILAHA YETU YA KWELI  Kujitegemea na Kuthamini MASHABIKI ndio MSINGI wa mafanikio ya KWELI ya timu YETU. Lazima tujifunze kuanzia PALE TULIPO. Tuanze na uwezo wetu, ili tuinuke kwa pamoja, WASHABIKI N… Read More

0 comments:

Post a Comment