„KISWAHILI Muhimili, Ni Roho mengine mwili“
Kiswahili
Kiswahili, Hebu wote tujadili.
Vifimbo Cheza wa hili, Mudahili Umahili.
Daima tunajadili, Madini si Kiswahili.
KISWAHILI Muhimili, Ni Roho
mengine mwili .
Wengine
tumekalili, Elimu si Kiswahili.
Hawanayo
afadhali, Magwiji wa Kiswahili.
Shahada juu ya
mbili, Hawapewi ujabali.
KISWAHILI Muhimili, Ni Roho mengine mwili .
Hebu na
tutafakali, Tena hata mara mbili.
Ung’eng’e
tunakubali, Kiswahili kiko mbali.
Kivipi tufike
mbali, Duniani wakubali?
KISWAHILI Muhimili, Ni Roho mengine mwili .
Sisi ndio
Kiswahili, Ndio hasa wetu mwali.
Tumpende mara
mbili, Wampende na wa mbali.
Watoe nyingi Mahali, Sifaze zifike Mbali.
KISWAHILI
Muhimili, Ni Roho mengine mwili .
Kiswahili
muhimili, Wasomi hawakubali.
Ubunifu uko
mbali, Hatunayo kandambili.
Elimu Bora ni
swali, Uzalendo uko Mbali.
KISWAHILI Muhimili, Ni Roho mengine mwili .
Wasomi
wamekalili, Ung’eng’e ndio kamili.
Kiswahili si
kamili, Sokoni hakishamili.
Soko lenye Majabali, Kipi chetu Muhimili?
KISWAHILI Muhimili, Ni Roho mengine mwili .
Msingi na wa
Awali, Ung’eng’e si Kiswahili.
Sekondari
Kiswahili, Vyuo pia Kiswahili.
Ofisini
Kiswahili, Binafsi na Serikali.
KISWAHILI Muhimili, Ni Roho mengine mwili .
Ung’eng’e usiwe
mbali, Na nduguze mbalibali.
Utufae kwa
achali, Na pengine kwa ugali.
Lengo kuu
Kiswahili, Kila ngazi kishamili.
KISWAHILI Muhimili, Ni Roho mengine mwili .
Woga shida kukabili, Twaogopa na vivuli.
Sayansi labda
kweli, Uraia sio kweli.
Ung’eng’e na
Kiswahli, Lazima ni Kiswahili.
KISWAHILI Muhimili, Ni Roho mengine mwili .
Tunatupa
Kiswahili, Tunabaki na LIMWILI.
Maroboti yana mwili, Yana pewa na Akili.
Fikiri mara ya Pili, Ufumbue
fumbo hili.
KISWAHILI Muhimili, Ni
Roho mengine mwili .
0 comments:
Post a Comment