Monday, April 15, 2013

BUNGENI: HOJA YA BANGI IFANYIWE KAZI NA IISHE

HOJA YA BANGI: Wakisema nchi za Ulaya tutakataa?

Pengine LAWAMA ije kama Mbunge hakutoa Tathmini ya kina JUU ya FAIDA na HASARA za BANGI na SIGARA! Kiasi cha kutufanya tushindwe kuamua kipi bora. SIDHANI kama hoja hii inapaswa kuwa kama Nyongeza,ukiangalia uzito wake katika jamii, endapo itapewa maamuzi chanya!

LAKINI, hii isimpe nafasi waziri wa wizara husika KUTOFANYIA TATHMINI, maana BANGI imejitokeza mara nyingi BUNGENI (Nisaidieni nukuu zake) Kwa hiyo waziri kajibu vizuri, kusema atafanyia kazi. Afanyie kazi kweli.Tunatabia ya KUPUUZIA MAWAZO yetu mpaka tudhulike.

Mfano: Marehemu Dr Remmy Ongala, aliwahi kulalamika Songea, Uwanja wa Majimaji! alisema " NCHI YETU YA AJABU SANA, NINGEKUWA ULAYA NINGEPEWA ZAWADI KWA WIMBO WANGU WA MAMBO KWA SOKSI, KWA SABABU, WATU WAMEELEWA MOJA KWA MOJA UMUHIMU WA KUJIKINGA NA MAAMBUZI YA UKIMWI. LAKINI VIONGOZI WETU  WAMEPIGA MARUFUKU WIMBO HUO KUPIGWA MAREDIONI, AKAUPIGA LIVE!". Hatukukaa muda VIONGOZI WAKUBWA KABISA na vyombo vya habari vikawa vinaeleza kwa UWAZI kuliko hata REMMY, kuhusu UKIMWI, kama tuonavyo leo. NAAMINI ALIPASWA KULIPWA FIDIA.

VIVYO HIVYO KWA MAMBO MENGINE YASIYO NA TASWIRA NZURI KATIKA JAMII, KAMA IMANI ZA UCHAWI, MADANGURO NA MIZIKI YA AJABU. YANAPIGIWA KELELE, BADALA YA KUONA NINI KIFANYIKE,TUNASEMA HAYAPO! KWELI HAYAPO?

Na akitokea Mtaalamu/Mwanafunzi anatakata kufanyia Utafiti, atapigwa vita/ au kuonekana PUNGUANI. TUBADILIKE sisi wote, WABUNGE, SERIKALI NA WANANCHI. TUZITHAMINI HOJA ZETU NA KUZIJADILI KWA MAPANA YAKE, ILI KAMA ALIYESEMA ALIKUWA HAJUI ANACHOSEMA, BASI AELEWE. 

NA WABUNGE WETU " FANYENI TAFITI NDOGO BASI, KUBORESHA HOJA, AU NAZO MPAKA KUWE NA POSHO". Hata ikiwezekana ziwekeni katika jamii kwa mapana kabla ya kuziweka Bungeni, ambapo wakati mwingine mnakuwa na muda finyu!

Pia, hata kama tafiti ni nzuri kwa muongeaji yeyote, Mheshimiwa Mkapa, B "No Investigation No right to speak", lakini hata tafiti zinaweza kuanzia kwenye ULOPOKAJI, basi kwa kutumia haki ya UHURU WA KUELEZEA JAMBO, watu waachwe waongee (Naisifu Serikali Yetu Kwa Hili). Sasa wataalamu wa tafiti wachambue yanayaofaa kufanyiwa tafiti. Pengine bila Aristoto na Newton, Einstein asingefanya baadhi ya vitu. Zamani wazee hawakupuuzia hata ndoto, na ziliwasaidia kuepuka baadhi ya matatizo, kama ambavyo leo tunaweza kuenzi maneno ya wazee wetu, pengine hata kujali kama walifanya utafiti au laa!

Hoja ya BANGI ifanyiwe UTAFITI sahihi na kuwekwa bayana, ili tusiisikie tena BUNGENI. Mbunge asilaumiwe kwa kutoa hoja alaumiwe kwa kutofanyia utafiti sahihi hoja yake.

0 comments:

Post a Comment