Wednesday, April 24, 2013

BUNGENI NA WABUNGE



Wakati Kikao cha 11 sijui, kikiwa kibichi kabisa,tayari kumekuwa na mambo kibao kutoka Bungeni, ambayo unaweza kuyatafsiri vyovyote utakavyo. na Watanzania kama kawaida yetu, KILA mmoja anachagua wa kumtetea. Ili mradi mtu utoe HOJA. Tanki linaomba kuchangia kidogo, katika mijadala yetu mbalimbali juu ya mwenendo wa BUNGE letu, NA TANKI NALO NI LA BONGO VILEVILE, hivyo ulisome KI-BONGO BONGO.

Ukiangalia Kifungu cha 63 (2) cha Katiba ya Juamhuri ya Muungano wa Tanzania, kama sehemu ya pili, Bunge

           “………… chombo kikuu cha Jamhuri ya Muungano ambacho kitakuwa na           madaraka, kwa niaba ya wananchi, kuisimamia na kuishauri Serikali ya           Jamhuri ya Muungano na vyombo vyake vyote katika utekelezaji wa           majukumu yake kwa mujibu wa Katiba hii.” Sehemu ya kwa nza ni ya Bunge inamuhusu RAISI. Simo.

Tanki linaona kama inanitosha kuona kuwa BUNGE kazi yake ni Kuwasaidia wananchi kuisimamia serikali katika kuwaongoza kuyatafuta maendeleo yao. Yaani kuwakagua WATAWALA na TARATIBU ZAO, NA KUWASHAURI JUU YA YALE YANAYOWAFAA WANANCHI, IKIWEMO KUHOJI JUU YA YALE YAENDAYO KOMBO. Hii ni muhimu ili  kuhakikisha, WANANCHI wananufaika na NCHI yao,kama walivyoona iwe kupitia KATIBA. Linafanyika kupitia utungaji wa sheria.

Hivyo, njia nyepesi ya kulipima BUNGE letu, ni kufikiria kuwa TUNATAWALIWA na watu tofauti ( Mfano Waingereza/WAKOLONI ) halafu, wabunge/mawaziri wetu wawe wanachangia mambo ambayo wangependa serikali ya WAINGEREZA ifanye na yale ambayo isifanye! Na hivyo hivyo ukitaka kumjua MBUNGE wako kama anafanya kazi sahihi, angalia kama anayoongea/kufanya ambayo yanafaa chini ya UTAWALA huo wa KIKOLONI.

Kwa mtazamo huo, pia unaweza kupima hata, uongozaji wa BUNGE, kama je uongozaji unapelekea WABUNGE kuwafikishia UJUMBE sahihi WAKOLONI/WAINGEREZA? Kama haitoshi, ukitaka kujiona kama, unatoa hukumu sahihi kwa yanayotokea BUNGENI na kwa WABUNGE, jiangalie kama ungeamua hivyo hivyo kama ingekuwa ni chini ya UTAWALA wa kikoloni?

Njia nyepesi ya kupima ubora wa sheria unayoitaka, ni kupitia kuandaa sheria ambayo ungependa imuongoze adui yako. Hivyo MTU SAFI ataandaa sheria hiyo kwa kungalia jinsi inavyoweza kumbana yeye kwanza. JE,tunaye mtu safi? Hapana. Ubora wa bunge utapatikana kama wabunge wetu watakuwa na mtazamo wa namna hiyo. Lakini Kubwa zaidi, kama SISI wananchi tutakuwa na FIKRA BORA za kulitazama hili. UBORA wa BUNGE, liwe kama TUNATAWALIWA NA ADUI ZETU. MBONGO , JIULIZE KAMA UNAYEMUONA ANAFAA, UNGEMUONA ANAFAA KAMA ANGEFANYA HIVYO CHINI YA UTAWALA HUO. 

USIJIBU.

0 comments:

Post a Comment