Tuesday, June 11, 2013

MAONI JUU YA RASIMU YA KATIBA MPYA-1



KWANZA TUNAIPONGEZA HATUA NZURI NA KAZI NZURI ILIYOFANYWA NA TUME YA KATIBA MPYA. 

LAKINI MAONI YA MABORESHO PIA MUHIMU. NA KAMA ADA, NI VEMA KUWEKA WAZI KUWA MAONI HAYA YANAWEZA KUWA NI SABABU TU YA UPEO MDOGO WA KUIELEWA RASIMU, ILA NI VEMA KUTOA KULIKO KUJA KUJILAUMU KWA KUTO KUTOA MAONI. 

WANASHERIA NA WADAU WENGINE WENYE UJUZI ZAIDI TAFADHALINI TUONGOZENI KATIKA HILI


KUTOKA TANKINI

LUGHA YA TAIFA NA LUGHA ZA ALAMA
4.-(1) Lugha ya Taifa ya Jamhuri ya Muungano ni Kiswahili na itatumika katika mawasiliano rasmi ya kitaifa na kiserikali.

(2) Bila ya kuathiri masharti ya Ibara ndogo ya (1), lugha ya Kiingereza inaweza kutumika kuwa lugha rasmi ya mawasiliano ya kiserikali pale itakapohitajika.
(3) Serikali itaweka mazingira yatakayowezesha kuwepo kwa mawasiliano ya lugha mbadala zikiwemo lugha za alama na nukta nundu kwenye sehemu muhimu za umma na katika vyombo vya habari
vinavyotangaza habari zake kitaifa kwa ajili ya watu wenye mahitaji maalum.



Kiswahili kitumike kwenye SHUGHULI ZOTE ZA KIOFISI, ZA KISERIKALI NA BINAFSI KAM LUGHA YA KWANZA. Hii itangeza UMUHIMU wa Kiswahili na kukifanya kikue na kuheshimika, na huku ikiongeza UFANISI KITAIFA.

5. Jamhuri ya Muungano itaenzi na kuzingatia Tunu za Taifa
zifuatazo:
(a) utu;
(b) uzalendo;
(c) uadilifu;
(d) umoja;
(e) uwazi;
(f) uwajibikaji; na
(g) lugha ya Taifa.

Hizi Tunu ndio nini hasa kwetu, na zinatoka kwa nani, pia tunazipimaje?

Je! Fikra Bora, Rasilimali,Vipaji,Ukweli, Utashi navyo vinaweza kuwa Tunu?

MAMLAKA YA WANANCHI
6. Jamhuri ya Muungano ni nchi inayofuata misingi ya demokrasia inayozingatia haki ya kijamii, na kwa hiyo:
(a) wananchi ndio msingi wa mamlaka za nchi, na Serikali itapata madaraka na mamlaka yake kutoka kwa wananchi ambao kwa umoja na ujumla wao wanaimiliki na kuipatia Katiba hii uhalali;
(b) lengo kuu la Serikali litakuwa ni maendeleo na ustawi wa wananchi;
(c) Serikali itawajibika kwa wananchi; na
(d) wananchi watashiriki katika shughuli za Serikali kwa mujibu wa masharti ya Katiba hii.

Sijui kama MAMLAKA YA WANANCHI YAKO WAZI SANA HAPA.


MALENGO MAKUU
11.-(1) Lengo Kuu la Katiba hii ni kulinda, kuimarisha na kudumisha udugu, amani, umoja na utengamanowa wananchi wa Jamhuri ya Muungano kwa kuzingatia ustawi wa wananchi na kujenga Taifa huru lenye demokrasia, utawala bora na kujitegemea.
(2) Bila ya kuathiri masharti ya Ibara ndogo ya (1), lengo hilo kuu litaendelezwa na kuimarishwa katika nyanja zote kuu, ikijumuisha nyanja za kisiasa, kiuchumi, kijamii, kiutamaduni na
kimazingira

Lengu kuu liwe Kuboresha Jamii ya Tanzania kwa kupitia shughuli zinazowanuafaisha na kuwagusa  Watanzania wengi


MARUFUKU BAADHI YA VITENDO

21.-(1) Mtumishi wa umma aliye katika ajira ya kudumu hataruhusiwa kuingia katika ajira nyingine yoyote yenye malipo ya mshahara.
(2) Mtumishi wa umma haruhusiwi kuchaguliwa au kuteuliwa kushika madaraka katika chama cha siasa.
(3) Mtumishi wa umma aliyestaafu na anayepokea malipo ya pensheni kutokana na fedha za umma haruhusiwi kuwa mwenyekiti, mkurugenzi au mtumishi zaidi ya vipindi viwili katika:
(a) shirika au kampuni inayomilikiwa au kuendeshwa kwa fedha za umma; au
(b) chombo chochote cha umma

BADO KUIELEWA VIZURI HII ( Hasa namba 1),hapo tunalenga nini, na mishahara yenyewe haitoshi?

HAKI ZA BINADAMU, WAJIBU WA RAIA NA MAMLAKA ZA NCHI
SEHEMU YA KWANZA
HAKI ZA BINADAMU

HAKI: Hapa mimi naona bado hapako sawa

  1. Kwanza, kuwe na haki za Mtanzania, halafu kuwe na haki za Binadamu
  2. Lugha iwe wazi kuwa Mtaznania  ana HAKI YA KUPEWA…………!
  3. Haki ya Elimu iwe Mpaka elimu ya chuo Kikuu
  4. Vitu kama Chakula Bora, Afya Bora,Makazi Bora,Elimu Bora,Ajira na Ujira Sahihi,Ulinzi wa aina zote na kadhalika view ni HAKI YA WATANZANIA WOTE  na sio makundi Fulani tu. Na ISIANDIKWE SERIKALI ITAWAPATIA FURSA YA KUVIPATA, BALI IWAPATIE KAMA HAKI YAO.



WAJIBU: Hapa pia kama panahitaji maboresho

  1. Wajibu wa kufanya na kutafuta na kutambua kazi na majukumu yake halali
  2. Wajibu wa kulipa kodi bila kushurutishwa na kusaidia ukusanyaji wa kodi
  3. Wajibu wa kuheshimu na kuzijua sheria za nchi
  4. Wajibu wa kulinda kuheshimu haki za HAKI za watu wote.
  5. Wajibu wa kujituma katika kuahakikisha ANAPATA vigezo vya KUPEWA HAKI zake.

MENGINEYO MPAKA HAPA

Kuna vitu ni kama havijapewa kipaumbele

  1. Uwepo wa mchakato wa KUIPATA TUME  ITAKAYOKUWA INAFANYA MCHAKATO WA KATIBA. Ni vema katiba ikatamka ili kuhakikisha TUME hiyo inakuwa na utaifa Daima.
  2. Umuhimu wa kuwa Chombo/Mfumo Huru na Maalumu kwa Ajili ya Ushauri huru wa mambo ya kitaifa na UBORESHAJI wa rasilimali ZETU.
  3. Msingi sahihi wa Kuchunguza MAZINGIRA YA RUSHWA na KUIDHIBITI rushwa bado hauko wazi. Mfano, kutaifisha mali ya MTOAJI AU MPOKEAJI, kwa manufaa ya Taifa endapo mazingira vidhibiti havitatosha kumtia hatiani mtuhumiwa.


TUSICHOKE KUTOA MAONI, KATIBA NI HATMA YETU WADAU!
CHANGIA MABORESHO TUYAVUGUMISHE TENA

0 comments:

Post a Comment