Friday, December 20, 2013

SIMBA ACHENI UYANGA, WATANI YANGA MAJANGA



1
Hao hasa ndio yanga, Kwao ndio kujipanga.
Okwi sifa sitapinga, Tano wakumbuka Yanga.
Wakongo waende yanga, Nonda alivyowapanga.
Wageni Yanga mapanga, Kuwamaliza wachanga.
Lengo kubwa lao Yanga, Eti Simba kuwatwanga.
Kelele leo za Yanga, Okwi waona Mganga.
SIMBA ACHENI UYANGA, WATANI YANGA MAJANGA
2
Wageni waende Yanga, Kwetu Simba si Uganga.
Wageni Yanga Uganga,Simba tano kutufunga.
Mogela aliwaganga, Hakupenda kutufunga?
Kenya haikuwaganga, Uganda watawaganga?
Waghana sio waganga? Kagame mkatufunga.
Nurdini hakuwaganga, Chuji ameshatufunga?
Ngasa acheza Kiyanga, Simba aweza ifunga.
SIMBA ACHENI UYANGA, WATANI YANGA MAJANGA
 3
Simba kweli kama Yanga, Japo yanga ni majanga.
Uzalendo zero yanga. Pesa nyingi na Ujinga,
Usajili wa kijinga, Lengo Simba kuifunga.
Acheni saka waganga, Mchawi wenu Ujinga.
Sasa eti wajipanga, Mbeya City Kuifunga.
CAF Villa yawafunga, Enyimba Mtaifunga?
SIMBA ACHENI UYANGA, WATANI YANGA MAJANGA
4
Ujinga watani Yanga, Uswahili wawafunga.
Sio Simba si wajinga, Mmetuzidi Ujinga.
Jangwani Hamujajenga,Bora ya wetu ujinga.
Miaka nane mwafunga, Pesa lukuki ni Yanga.
Makabati mmefunga, Hatua mbili Majanga.
Kagameni mwatufunga, Ndio mwisho wenu Yanga.
SIMBA ACHENI UYANGA, WATANI YANGA MAJANGA
 5
Simba yangu sio Yanga, Japo tunao Uyanga.
Mwaga hela kama Yanga, Misri tunawafunga.
Sita kwao watufunga, Saba nyumbani twafunga.
Mpira kweli si chenga, Msingi hasa kufunga.
Simba ni noma kwa chenga, Magoli bora twafunga.
Soka Simba, Mbio Yanga, Bora goli ndio Yanga.
SIMBA ACHENI UYANGA, WATANI YANGA MAJANGA
6
Haka katimu ka Yanga, Yangu Simba kaifunga?
Lunyamila kweli Yanga, Hata Simba kuifunga.
Kizota sibishi Yanga, Kalimagonga ni Yanga.
Chambua  alitufunga,Bila mamia waganga.
Homa la jiji Mganga?, Na Simba alitufunga.
Yanga rudieni Yanga, Tupeni Yanga majanga
SIMBA ACHENI UYANGA, WATANI YANGA MAJANGA
 7
Nje chachu sitopinga, Wageni sifa Ujinga.
Simba acheni Uyanga, Simba yangu sio Jinga.
Zambia tuliporinga, Nani mgeni mganga?
Pawasa Aseke ifunga, Ngapi wakongo waganga?
Matola kuto kufunga, Na Masha hawakulonga!
Simba acheni ujinga, Kuiga mambo ya Yanga.
SIMBA ACHENI UYANGA, WATANI YANGA MAJANGA
 8
Bongo leo ni majanga, Soka katawala Yanga.
Nchini kuna ujinga, Ukweli tunaupinga.
Fikira PEVU za Yanga, Yetu Simba Kuifunga.
Kweli Kandambili Yanga, Kichawi unatufunga.
Uongozi wote Yanga, Macho Simba kuifunga.
Tanzania mwembeyanga,Soka mwisho la mchnga.
SIMBA ACHENI UYANGA, WATANI YANGA MAJANGA







0 comments:

Post a Comment