Monday, December 16, 2013

Kama "Mapera",Fikra hizi nazo Feki!

Zamani, Tukuyu-MBEYA kulikuwa na vyakula na matunda mbalimbali pengine kuliko leo. Kulikuwa na aina ya “MAPERA” iliyofahamika kwa jina la “KALUNGA-MUNYU”. Mtu alikuwa hanunui MAPERA, zaidi watoto waliyachezea kama wachezeavyo GOLORI watoto leo (Kama Wapo). Mapera yalikuwa na radha Fulani iliyokuwa kati ya CHUMVI, LIMAO, ACHALI, SUKARI, ASALI na vitu vya namna hii. Na kwa kweli kupata PERA la KALUNGA-MUNYU ilikuwa ni bahati sana! Haikuwa rahisi kula zaidi ya KALUNGA MUNYU 10, katika miaka 15.

LEO, MAPERA yanauzwa Tukuyu, na si rahisi kuuziwa KALUNGA-MUNYU. Kupata MAPERA yakiwa yameivia VICHAKANI AU MITINI,imekuwa tabu kidogo, maana watu mapema wamekwisha “JISEVIA”. Hata uende sehemu za VIJIJINI zaidi,si rahisi kupata “PERA ORIJINO” na KALUNGAMUNYU,ndio kabisa huwezi kupata. MAPERA pia yamekuwa FEKI kama ambavyo tuonavyo vitu vingine vingi nyakati hizi.

Kama kuna kitu kinadumu DUNIANI huwa ni MABADILIKO, hatuwezi kuyakataa. LAKINI mabadiliko mengi yatokanayo na maendeleo DUNIANI yanaonekana kuambatana na kuondoa UBORA na UASILI wa DUNIA na VIUMBE vyake, tukiwemo BINADAMU. UBORA WA UASILI unaondoka NA unakuja UBORA FEKI yaani UBORA WA KUTENGENEZWA. Tunaweza kuliona hili, si kwenye VYAKULA TU, bali hata katika MIILI na AFYA zetu. Kumekwishaanza maneno kuwa karibia tutaanza kupata MVUA ya kutengenezwa,hivyo pengine tutarajie mengi yatokanayo na maendeleo YAO, ambayo hasa ndio mwanzo wa kupungua kwa UBORA WA ASILI. Mfano mzuri ni ongezeko la wasomi na UBORA WA ELIMU, ni kama FEKI hivi.

YOTE tisa, KUMI ni KUPOTEA kwa UBORA WA ASILI WA FIKRA ZETU.Ni kama hata FIKRA ZETU ZINAKUWA KAMA ZINATENGENEZWA. Kila iitwayo siku, watu tunazidi, kuamini kuwa yale MAZURI, ambayo tumeagizwa na MUNGU au WAZAZI, kuwa hayawezekani,ila yale yatokanayo na maendeleo YAO, sisi huona ndio hayakwepeki.Hatuyaamini kabisa yetu, na kukumbatia ya wenzetu, hata tuyaonapo kuwa yanatudhulu. Eti! Sababu KUU ni UTANDAWAZI au NGUVU YA SOKO HURIA. HIZI sababu nazo sio FEKI kweli?

Kila ukimuuliza MTU kwa nini anafanya HIKI AU KILE, jibu ni NDIO UTANDAWAZI UNAVYOTAKA. Hata haya niyasemayo,nayo nahisi kama ni yatokayo na FIKRA ZENYE UBORA FEKI. Na pengine msomaji nawe utayasoma kwa FIKRA ZENYE UBORA FEKI, na kuishia kupuuzia ukiamini KILA FEKI NI FEKI na kubaki na FIKRA FEKI. Huo ndio mwelekeo wetu kwa sasa,TUNA MAMBO MENGI FEKI,TUNA WATU WENGI FEKI, TUYAONAYO MENGI NI FEKI, TUYASOMAYO NI FEKI,TUYATENDAYO NI FEKI, TUYASIKIAYO FEKI,TUYASEMAYO NI FEKI,…………FEKI!

Tunahitaji FIKRA ZENYE UTAMADUNI WA UBORA, kuweza kutambua UBORA HASA NA FEKI ,ili walau kuweza kupunguza madhara ya UFEKI unaotuzunguka katika maisha ya kila siku.

0 comments:

Post a Comment