Sunday, July 14, 2013

KANDANDA LA BONGO

Vijana waende ng’ambo, Liwe letu kuu JAMBO.

Fimbo tangia kitambo, Kwao TFF ni wimbo.
Bora wale wa kitambo, Waliweza wetu wimbo.
Wa leo twaona mambo, Na Mengi yao majigambo
Vijana waende ng’ambo, Liwe letu kuu JAMBO.

Raisi kafanya mambo, Sitomlaumu jambo.
Kawaleta na wa ng’ambo, Mliosema wagambo.
Mapesa Rambo kwa Rambo, Mkamnyima na WIMBO
Vijana waende ng’ambo, Liwe letu kuu JAMBO.

Tumeganda na Urimbo, Kandanda laenda kombo.
Nina langu moja jambo, Sitoongea kimombo.
Tubaki kwenye urimbo, Vijana  wafanye mambo.
Vijana waende ng’ambo, Liwe letu kuu JAMBO.

Tuache vyetu vimambo, Kupenda yetu matumbo.
Hata iwe ni kitambo, Yatafika majigambo.
Pesa nyingi sio jambo, Tujali yao matumbo.
Vijana waende ng’ambo, Liwe letu kuu JAMBO.

Taachane na wa ng’mbo, Watuacha kwa urimbo.
Yanawiriyo matumbo, Sina hamu na wang’ambo.
Hatuchukui kitambo, Kwa mafupi majigambo.
Vijana waende ng’ambo, Liwe letu kuu JAMBO.

Tushike yetu mitambo, Tusidekeze matumbo.
Tusiwe na mengi mambo, Tuchague moja jambo.
Turudi kama kitambo, Tuzidi ya kale mambo.
Vijana waende ng’ambo, Liwe letu kuu JAMBO.

Kila wimbi lina chombo, Kiswahili si kimombo.
Vipaji kama ng’ambo, Hatuyaoni makombo.
Hii mifumo ya ng’ambo, Kwetu kivuli cha fimbo
Vijana waende ng’ambo, Liwe letu kuu JAMBO.

Wanawasifu wa ng’ambo, Nyumbani kwaenda kombo.
Onyesheni yenu mambo, Mkiimarishe chombo
Ligi yetu ya kitambo, Tumeitupa na Chambo.
Vijana waende ng’ambo, Liwe letu kuu JAMBO.

0 comments:

Post a Comment