Saturday, December 7, 2013

MSHAHARA, nani apewe zaidi, MENEJA au MFAGIZI? Kwa nini?



Moja kati ya masomo, ambayo wanafunzi siku kadhaa hapo nyuma tulikuwa tukifeli kwenye KIDATO cha SITA, ni UCHUMI. Ukisoma maswali yake, unaona kama tayari umefaulu, lakini majibu yakitoka unashangaa, alama kubwa ni “C”,pengine hata kitaifa. Sijui mambo yakoje kwa sasa. Lakini, badala ya
kuwalaumu wanafunzi, wengine walijiuliza na kupata majibu kuwa, wengi wa walimu waliokuwa wakifundisha uchumi, walikuwa ni walimu ambao hawakuchukua somo hilo kama la MSINGI wakiwa vyuoni,ila kwa sababu ya uhaba wa walimu wa uchumi mashuleni, ikawa inawalazimu kufundisha hivyohivyo kwa KUJISOMEA kwanza. Kwa kweli ilisaidia lakini, tatizo likawa ni wanafunzi kuelewa visivyo na kuona rahisi kupindukia. Mfano, mzuri ulikuwa matumizi ya nadharia ya “MARGINAL”, yaani marginal productivity,marginal utility,marginal value na kadhalika.Na baraza la taifa a mitihani,wao waliuliza maswali kwa kuamini mmefafanuliwa hadi matumizi ya kimtaa,japo walikuwepo wakali walioweza kuelewa zaidi ikiwa ni uwezo wao wa kuzaliwa. Jamani elimu ni ya taifa sio ya wachache.


Kifupi wanauchumi hutumia hii nadharia kusoma matokeo baada ya kuongeza rasilimali kwa kiwango Fulani,hasa kimoja. Yaani, mfano ukiongeza mtu mmoja shambani, nini ongezeko la magunia ya mazao, kama yameongezeka kumi, basi ndio unasema huyo mtu kaongeza kumi, kama yamepungua matatu, basi pengine kaleta hadithi za LIVERPOOL  NA  MAN U, AMA SIMBA NA YANGA, kama sio majungu,na kupelekea hilo. Ulichokijua ndio MARGINAL, “ONGEZEKO ZIADA litokanalo na kiwango kimoja cha ongezeko la rasilimali”. Hii inatumika kwenye mambo kibao,ikiwemo hata kuridhika kutoka na unachokula au kutumia, na zaidi hadi, hufikia hadi kufananishwa na nia ya watu kulipa pesa kwa ajili ya huduma Fulani. Inaaminika kiuchumi kuwa mtu analipa kulingana na kiasi cha kurudhika anachotegemea ama kiasi cha  msukumo cha kutaka kulipa akilinganisha na kiasi cha pesa anachoweza kutoa. Hapo ndio hasa tanki linalenga, yaani,uthamani ambao mtu anawiwa kuulipia. Kwa kweli kuelewa sana uchumi,inabidi tutafute wanauchumi. Japo kuelewa kidogo, kunaweza kutusaidi sana kwenye maisha yetu ya kawaida. Lakini kujadili hakuanzushwi na wanaoelewa sana,bali wanaotaka kuelewa.

Kama mtu analipa kulingana na anachotarajia, maana yake,mtu akipewa mshahara mkubwa anategemewa kutoa ongezeko la thamani kubwa Zaidi ya anayelipwa kidogo. Hii inajionyesha sehemu nyingi,hasa kwenye SOKA LA BONGO,japo sijui makazini,hasa Tanzania. Lakini bado ukweli,unajidhihirisha kuwa meneja akipiga simu moja,inaweza kuingizia ama kuindalia,ama kuiokoa kampuni kwa kiasi kikubwa kuliko mfagizi, hata kama anachafuka sana. 

Tukiachana na porojo hizi, tukajikita kwenye UJENZI, eneo mlengwa, maana WABONGO, hawakawii kusema mpaju blogu imekuwa ya kisiasa sasa, imeingilia madai ya kutangazwa mishahara maraisi, kama itasaidi kifikra kulifikiria hilo basi vema. Katika Ujenzi kuna taaluma kama UBUNIFU, UHANDISI, UKADIRIAJI NA KADHALIKA ambazo hasa huwa ziko katika muundo wa huduma, na zina taratibu madhubuti, kutokana na unyeti wake kiutendaji na kijamii. Mteja hapa, wakati mwingine hutoa pesa kisheria, na sio kiupimaji wa thamani yake yeye mwenyewe. Na hata kama kwa namna moja au nyingine akiwa anapima, bado kuna maswali,yanayojitokeza,kutokana na kuwa na washiriki kibao,katika kukamilisha huduma na mjengo wenyewe. Kwa kweli,kuna wakati mteja eneo hili hubaki kama MBONGO akiwa hoi mbele ya daktari, lolote litakuwa ndio. Bora ujamaa unatuokoa na bei za madaktari. Japo kuna vigezo vingi vya uthamani katika uwanja huu wa ujenzi, lakini sijui kama wateja huzingatia vyote kwenye kuamua, na sijui hasa kama sheria zilizopo zilizingatia vigezo vyote kwa kumtazama mteja mwenyewe au kutazama duniani, na Zaidi sijui kama upimaji wa thamani iendayo kwa mteja hauathiriwi na mabadiliko ya kiteknolojia ama la!

Sasa, uthamani wa mteja wa namna hii chimbuko lake liko wapi? Na je huwa chimbuko hilo ni la kudumu, ama hubadilika? Nini kipo ndani ya ujenzi na thamani ya malipo kwa wataalamu wake au hata pamoja na wajenzi? Tanki limeona kuna kitu cha kukichambua japo kwa upeo kidogo uliopo kwa sababu, ujenzi unaligharimu taifa pesa nyingi sana,hivyo kuna umuhimu wa kuhakikisha thamani sahihi inapatikana na inaenda kwa mhusika sahihi. Bila hivyo, hata utaalamu hautakuwa na changamoto za kimaendeleo.

Ujenzi kama ununuzi wa simu mtaani, tunaweza kusema, mtu anaita wamachinga anawaambia nataka simu aina fulani. Wamachinga wanakimbia madukani a kuleta simu kama kumi hivi,na yeye anachagua moja na kuinunua. Tofauti ni kuwa kwenye ujenzi, mnunuzi husika huwatumia wataalamu wa simu kumshauri aina na kuwaita wamachinga na kuhakikisha kama simu waliyoleta ndio yenyewe,na ikibidi kusimamia malipo ya simu hiyo. Mchakato huo ukiufafanua kwenye mazingira halisi,unaweza kuchanganyikiwa,kiasi cha kuona ni vema wataalamu hao waongezewe miaka ya kusomea hizo taaluma. Sasa, nani hasa anayepelekea kumpatia MNUNUZI thamani ya simu yake kati ya wale mafundi, labda (Architect-Msanifu, anayesema simu iwe hivi, na nivema mkononi ijae hivi), (Engineers-Wahandisi,wanaosema lazima ihusishe chombo hiki,waya huu na kadhalika iwe madhubuti), (Quantity Surveyor-Mkadiriaji, anawafafanulia kuwa simu hii itacheza kati ya bei hizi, na hata kama kaleta kwa mtindo huu, bei haizidi hii) ama (Contractor-Mkandarasi, anayesema usijali, pesa yako kaa nayo kwanza, utanipa nikileta simu na baadae anaomba nyongeza kidogo kwa ajili ya taksi ama ndege,akidai kazunguka kote ili kuleta kitu bora kwa bei nzuri,kama simu yake ndio iliyochaguliwa).

KIBONGOBONGO,unaweza kujibu unavyoona, lakini ni vema sana kujua hasa Uthamani ama VALUE, yenyewe ndio nini kwa huyu MNUNUZI au CLIENT? Ili tukichanganya na uchumi wetu kidogo, tunaweza kuona kuwa anayestahili kupewa kipaumbele kimalipo, ni nani kati ya kundi tajwa hapo juu, yaani yule ambaye MCHANGO wake unapelekea ONGEZEKO kubwa la UTHAMANI huo. Ama, tukitaka kufanya maisha magumu zaidi, tunaweza kuanza kuona UMUHIMU wa kuwepo, kitu AMBACHO sheria imeturahisishia kwa kusema wote wanatakiwa kuwepo kwenye UJENZI. Kama ilivyo ada, japo mada haijaisha, wengine watahoji,mbona mwandishi hakugusia, aina zote za ujezi, na mambo kibao yaneye uzito mdogo, kuliko HOJA yenyewe. huo ndio utanzania,wenyewe tunajuana, kikubwa ni kuwa iwe civil works,building works,or any other special works of construction, what exactly is the value the clients get? And are we real proportionally reflecting the value contribution by participants to fees earned, or this  economic concept has place in construction. Nimejaribu ung'eng'e,pengine nimeharibu maana kabisa,badala ya kuweka msisitizo. Tutafika ila cha mot tutakiona.

...................................................................Itaendelea..................................................................................

0 comments:

Post a Comment