Saturday, December 28, 2013

UTANDAWAZI na BIM, havitaki ubinafsi!!!!!



                       DUNIA ni kweli kijiji, "UBINAFSI" UTATUUA, TUUBORESHE haraka.
KUNA hisia kuwa WATANZANIA wengi, hatuna TABIA YA KUFANYA KAZI NJE YA NCHI. Sidhani kama ni JAMBO BAYA, pengine TUMEJITOSHELEZA. Lakini HOFU yangu, ni kuwa Hatuna UTAMADUNI wa kufanya KAZI zetu katika KIWANGO cha KIMATAIFA. Na kama
HATUSHIRIKIANI KWA SABABU za kijinga KAMA UBINAFSI,basi, hii maana yake, tunajichimbia kaburi KIMATAIFA. Kwa sababu, kwenye SOKO LA KIMATAIFA, tutachemsha. Na kama UTANDAWAZI haukwepeki, maana yake HATA SOKO LA NDANI PIA tutachemsha. Kama hatushirikiani na wenzetu, basi sababu isiwe UBINAFSI. KUUACHA KABISA, sio rahisi na pengine sio SAWA, kwa zababu za KIZALENDO NA UMAKINI, basi, TUUBORESHE UBINAFSI WETU, utufae, uweze kutufaa KATIKA DUNIA YA LEO.
(The Guardian news paper of Wednesday, March 17, 2004, in Tanzania quoted President Benjamin Mkapa in Dar-es-salaam when launching his report on the World Commission on the Social Dimension of Globalisation (WCSDG) that;

“Increased terrorist incidents, war, chaos and lack of good governance in some countries in the world and multinational companies indicate that the time is ripe to reform the global relations”.

On the same newspaper but on Friday March 26, 2004, speech by President of the United republican of Tanzania and co-chair of the (WCSDG) as presented to the governing body of the International Labour Organization (ILO), Geneva,24th March was displayed. From the report;

“Globalisation begins at home, and someone must be accountable for this. Individuals, communities and countries have the primary responsibility to create a conducive environment that would build local capacity to access opportunities for self-advancement that Globalisation presents”.

Globalisation is not a proposal or a policy of choice; it is a fact. The commission pointed out that how it is responded to, will make a lot of difference. We must respond in a way that can maximize the potential of the market, without rejecting accountability for social justice and our sense of community.) (SOURCE:A Dissertation Report, Mpangule,Juma Ahmed 2004,B.Sc BE 2004,UCLAS-UDSM.)

MANENO YA VIONGOZI WENGI, sijui kama tunayatendea HAKI. Miaka kumi sasa, sijui kama WATANZANIA utandawazi, upo MIDOMONI ama VICHWANI na MATENDONI mwetu.Tanki limeonelea vema kutoa USHAURI kama sehemu ya KUTAKIANA HERI YA MWAKA MPYA wa 2014, ikiwa ni miaka KUMI, tokea KAULI HII ITOLEWA NA Raisi. TUUWEKE UTANDAWAZI MATENDONI SASA, si kwa njia yeyeto zaidi ya KUBORESHA UBINAFSI,  ama KUSHIRIKIANA kwa manufaa ya WOTE.

Vile vile, kwa upande wa WAJENZI, BIM imekwisha GUSA maeneo KADHAA (Angalia Picha chini) na pengine kwa sasa ni ZAIDI. Sio, maana yake tukimbilie KUSHIRIKIANA KIMATAIFA,KICHWAKICHWA, ila ni MUHIMU sisi KUWA wataalamu WA KIMATAIFA, hata kama TUNAFANYA KAZI NYUMBANI. Building Information Modeling (BIM) ikikubalika NCHI zilizoendelea,basi kwetu, ni heri TUAKAITAMBUA kama UTANDAWAZI, na kuifanyia kazi kuliko, kuamini kuwa inakwepeka, halafu ikawa kinyume. Kwetu kama ambavyo utandawazi haukwepeki, BIM, pia haikwepeki, labda kama tunaamua kuendelea na UGONJWA wetu wa UBINAFSI. BIM na ubinafsi ni vitu VIWILI tofauti. Yaani, BIM inaweza kutusaidi Watanzania kupunguza UBINAFSI, kitu ambacho pengine ndio kikwazo cha mafanikio yetu kuanzia kwenye FAMILIA, mpaka KITAIFA.


KIBONGOBONGO, nduguyo akiharibikiwa, kwako furaha. Na hakuna uwezekano wa kufanya BIASHARA na ndugu yako, MAANA akila PESA sio KOSA. Na zaidi, huwa UNDUGU ni kusifiana ya KIJINGA, ama KUSAIDIANA kwenye MAMBO YASIYO ya msingi ZAIDI ya yale ya MSINGI. kama haitoshi, michango mingi INALENGA KUSHUSHA KASI YA MAENDELEO kuliko kuongeza KASI hiyo, na hata mtu akisema KUWA HIYO SIO sawa, aatitwa MFITINI, MBINAFSI, na pengine kuonekana hafai katika jamii, na kama ni mdogo, ndio kabisaaaaaaaa. Haya ni mambo kadhaa yanayoonyesha kuwa KUNA UMUHIMU wa kuboresha UBINAFSI wetu, kwa sababu KUUACHA, inaweza kumaanisha KUTHAMINI WENGINE KULIKO SISI KWANZA, kitu ambacho PIA sio UHALISIA wa DUNIA ya LEO. 


UBINAFSI wetu, sasa uwe unaotuweza kushirikiana bila KUMUUMIZA MMOJA wetu, na HATA ikibidi KUMNUFAISHA kulingana na MCHANGO wake. Kama anachangia kikubwa basi ANAOKOA WENGI, na hivyo anastahili KUSONGA ZAIDI, SIO KURUDI NYUMA HUKU TULIKO, hiyo inatupelekea wote kurudi nyuma. Hayo hayaishi kwenye FAMILIA TU, hata katika JAMII kadhaa, kuna IMANI kuwa mtoto wa MTU akiendelea ama KUMJENGEA nyumba NZURI mzazi wake, tayari kajichongea moto, atapigwa vita za KILA AINA, ili mzazi wake nae awe kama wengine. HII inaaminika kurudisha NYUMA maendeleo ya JAMII kubwa sana ya WATANZANIA, hasa vijijini. 

DAWA, TUBADILIKE KITABIA NA KIFIKRA.Dunia ya LEO, kufanya kazi na MTAALAMU mwenzio SIO kupunguza KIPATO, bali KUONGEZA uwezo WA KUMUDU Utandawazi, ama KUFANIKIWA KATIKA UWANJA WA VITA YA KIDUNIA. Yaani, SIKU ZA USONI, itakuwa AMA USHIRIKIANE NA WENZIO AU UTOKE SOKONI. Kifupi ni kuwa TUACHE UBINAFSI, kwa sababu HAUNA NAFASI KATIKA DUNIA YA LEO. Pia kijamii, hivyohivyo, kuna UMUHIMU maneno kama "mtoto wa mwenzio ni wako" yawekwe kwenye matendo sasa. Tuboreshe ubinafsi wetu.

.

BIM around the World (From (WSP Group Limited, 2013))

0 comments:

Post a Comment