Tuesday, December 31, 2013

Mungu wetu sio pepe.



1
Nataka kata Utepe, Kwanza radhi mnipe.
Mchana kuko kweupe, Machoni nisiwakwepe.
Uone nina Pelepe, Rohoni kwangu mweupe.
Si Madenge si Kipepe,Viongozi msisepe.
Beijingi msikwepe, Wabakie wa visepe.
Tuzishike zetu shepe,Jua yetu enda pepe. 
Mungu awe kwetu pepe, Sababu Bora  Tujipe.
2
Daktari hatumjali, Zahanati mbaya hali.
Vifaa havina hali,Matibabu bora ghali.
Uzazi sasa ajali, Hatuna si afadhali
Masikini kule mbali, Haki haiko kamili
Mtaalamu katili,Utabibu petroli.
Vifo vyatukabili, Siasa haitujali.
Mungu awe kwetu pepe, Sababu Bora  Tujipe.
 3
Elimu sitorudia, Kutwa tumeongea.
Hakuna kwenye dunia, Mjinga kaendelea.
Imani ikitulia, Amani itarejea.
Misingi ikiwa mia, Mipango itatokea.
Walimu wawe na nia, Ujuzi kuendelea.
Someni muwe mamia, Wajinga mtapotea.
Mungu awe kwetu pepe, Sababu Bora  Tujipe.
 
Ulafi tumebobea, Ukuu kugombania.
Kazini tunategea, Shahara tunalilia.
Kilimo kimepotea,Vijiji vyaangamia
Usafiri wachechemea,Ujenzi umeumia.
Uongo tunabobea,Ujinga twaatamia.
Uchafu kuchekelea, Taifa laangamia
Mungu awe kwetu pepe, Sababu Bora Tujipe.
5
Muumba kweli hupanga, Manani mwenye kujua.
Mkono mimi naunga, Kuhoji ili kujua.
Kila kifo akipanga, Muumba tunomjua?
Maradhi yetu kapanga, Watabibu hatotambua.
Ugomvi wetu apanga, Na Vyama kavichagua.
Umasikini kajenga, Tupigwe sisi na jua?
Mungu awe kwetu pepe, Sababu Bora Tujipe.
 6
Imani kutozipenda,Sayansi hutoipata.
Ukweli ukiuponda, Uwongo utafumbata.
Leo Mungu akipenda, Asante mama kupata.
Manani pia kapenda, Sifuri sisi kupata.
Ajabu Mungu kupenda, Sisi kutomfuata.
Labda ndio kapenda, Furaha si kutopata.
Mungu awe kwetu pepe, Sababu Bora Tujipe.













Related Posts:

  •  MPAJU WEEK 2020(Disemba 15-22)Uwanja wa Magereza Chuo-Ruanda Mbeyanani kufungua Dimba timu za wasichana?MPAJU FCVS SUPER EAGLES Mpaju FCSUPER EAGLE… Read More
  •  MPAJU WEEK 2020“JAMII YETU-KIOO CHETU” Kauli mbiu ya Mpaju Week 2020 ni JAMII YETU NDIO KIOO CHETU. Mpaju SC inaamini changamoto zinazoizunguka jamii yetu zinatokana na kushindwa KWETU kuzitatua. Mpaju SC inaikifikishi… Read More
  • Mpaju Week 2020-YAWA CHACHU KWA SOKA LA WANAWAKE MBEYAMpaju Week 2020 yaleta matumaini ya SOKA LA WANAWAKE MBEYA: Tamasha hili lenye KAULI MBIU YA JAMII YETU NDIO KIOO CHETU, lilifikia tamati siku ya Jumanne tarehe 22 Disemba 2020 pale Uwanja wa Chuo cha Magereza Mbeya, kuwakari… Read More
  • LIGI YA MPIRA WA MIGUU KWA WANAWAKE- MKOA WA MBEYAMPAJU FC (a.k.a ATINISU) WAANZA KWA KUKUBALI KIPIGO CHA MAGOLI 9 KWA 1 Tarehe 01 Machi 2021 kulifanyika tukio la kihistoria kwa wanasoka wa Mkoa wa Mbeya. Ligi ya Mkoa kwa Mpira wa Miguu wa Wanawake ilianza ras… Read More
  • LIGI YA MPIRA WA MIGUU KWA WANAWAKE - MKOA WA MBEYA MPAJU ATINISU WATISHA SANAWAWACHABANGA TUKUYU QUEENSNA KUSHIKA NAFASI YA TATUSiku ya Jumapili ya tarehe 07 Machi 2021, historia iliendelea kuandikwa kwa Mkoa wa Mbeya na kituo cha michezo cha Mpaju Sports Centre. H… Read More

0 comments:

Post a Comment