Sunday, July 6, 2014

TUJENGE MIJI NA JAMII ZAIDI YA MAJENGO YA MIJI


CHA KWANZA kunivutia nilipofika DORTMUND kilikuwa ni "SEMI CIRCULAR GLASS ROTUNDA" ya Architect Mario Botta, Lugano.Pengine ndio maana nimeongeza UUMINI wa "KUJENGA JIJI LA MBEYA" badala ya
"KUJENGA MAJENGO YA MBEYA". Sizungumziii uwezo wa Architects,ama wanataaluma wa ujenzi, la hasha, hapa nazungumzia AINA YA MAJENGO YA NCHI YETU. Kuna Umuhimu wa kuutazama UJENZI WETU kwa MIONO ya MBALI Zaidi ya hivi tufanyavyo. 

"Jamii inayoshindwa kusimamisha majengo ya nguvu yaliyosanifiwa na wajuzi wa hisabati  zilizopangiliwa wakishirikiana na wana sanaa wanaojua kuuunganisha kilichoimara na kinachopendeza, jamii ya namna hiyo itakuwa ya kubabaisha kila siku, itakuwa inatafuta vitu rahisi, vyepesi na visivyodumu. Vitu vya mpito",alisema Jenerali Ulimwengu kwenye kiungo http://www.raiamwema.co.tz/hapa-kwetu-tunakimbilia-wapi#sthash.zbFwEf3t.dpu

Mbali na mambo kama HISTORIA na TAMADUNI zetu zinazoweza kuhifadhiwa kupitia ujenzi, ama shughuli zingine ambazo bila ujenzi haziwezi kufanyika, bado kuna swala kimahusiano kati ya FIKRA zetu na MUONEKANO wa mazingira yetu. Mfano mtu, mtu akiwa na barabara mbovu, ni dhahiri anaweza kuhalarisha kuchelewa kazini, ama kutokamilisha biashara au shughulli yeyote kwa kuwa miundo mbinu ni mibovu. Na hatimaye ni kuwa na jamii isiyojali muda!

Kama haitoshi afya ya binadamu ni kitu cha thamani sana, na ukiangalia muda ambao binadamu anautumia akiwa katika eneo lililojengwa, unaweza kupata picha ni jinsi gani eneo hilo, likiweza kumpatia mazingira mazuri ya kiafya litakuwa limechangia katika maendeleo ta Taifa! Watu, hutumia masaa kati ya 4-6 kwa siku wakiwa shuleni,vyuoni,maofisini ama kwenye maeneo ya michezo. Wengi wetu hutumia masaa kama hayo tukiwa tumepumzika majumbani. Hivyo, kama majengo yetu hayana mazingira muhimu kwa ajili ya afya yetu, hata kama si leo basi kesho kwa kiasi kikubwa yanatudhulu na kuzuia maendeleo yetu bila wenyewe kufahamu.

Afya tu haitoshi, upo umuhimu wa furaha na raha kadhaa ambazo pia husababisha mtu kuweza na kuamua kufanya shughuli za kiuchumi kwa ufasaha zaidi.Mtu KUJISIKIA YUKO NYUMBANI, kimsingi ni msemo unaoashiria amani na furaha ya UNYUMBANI, ambao mbali na upendo, pia utulivu wa kifikra. Kuupata huu utulivu, ni lazima NYUMBA ama JENGO liwe na MANDHARI safi na ENDELEVU.Sio tu kuwa jengo liwe na mwanga, hewa na vifaa sahihi, bali pia liwe na mvuto na urahisi wa kutumika kwa matumizi mbalimbali kulingana na wakati. Kama watu hubadilika kwa nini MAJENGO yasibadilike NAO. Jana mlango wa MNINGA leo ALUMINIUM, juzi MGAHAWA kesho kutwa MGAHAWA NA CHAKULA. Vyote hivyo vinamaanisha mabadiliko ya vifaa kama majiko, muonekano na kadhalika! Haya hayapaswi kuwa tatizo ama mwanzo wa eneo linalozunguka kuharibika, bali kuboreka. JENGO lishangazalo hufundisha na kubadili fikra za mtu na ndio maana shepu ya kanisa ama msikiti sio sawa na nyumba ya kulala wageni. Kimsingi, wataalamu wafikirie pia kuijenga JAMII, na sio MJI tu kwa kupitia  MAJENZI yao.

Kombe la dunia 2014 BRAZILI, litakapokwisha, viwanja vitatakiwa kuendelea kutumika kama sasa ama zaidi ya sasa, vinginevyo vinaweza kupelekea hasara zaidi ya faida tarajiwa!Mfano ni Uwanja wa Taifa Tanzania, gharama ya kuendeshea TV wakati wa mechi, huonekana ni kubwa, na hivyo washabiki kukosa raha ya kuutazama mchezo  huku ukiendelea. Kwa hiyo kama matumizi ya uendeshaji uwanja ni makubwa kuliko marejesho, na timu zinaendelea kutotumia uwanja na timu ya taifa inaendelea kupunguza umaarufu na ushiriki katika mechi za kimataifa, maana yake tunapunguza faida ENDELEVU, yaani kutoharibu kesho kwa ajili ya faida za leo tu, kama ilivyosisitizwa kwenye kitabu cha
Forbes, L. H., & Ahmed, S. M. (2010). Modern construction: Lean Project Delivery and Integrated Practices. Boca Raton, FL, CRC Press,London-New York: CRC Press (an imprint of Taylor & Francis).

Kutokana na kuvutiwa na ART iliyowekwa pale MKABALA na STESHENI kubwa ya MATRENI, niliona ni vema kuGOOGLE kidogo, ili kuona walau nani msanifu na ilikuwaje aweke vioo vile vyenye umbo la KONI. Baadhi ya maelezo niliyoyakuta ni

1."The development of the land was not easy to conceive. The south-facing city edge which was taken back should be maintained as a building line, as well as the character of the train station square"
MUNICIPAL LIBRARY DORTMUND
2."Mario Botta from Lugano in Ticino was emerged in 1995 as the winner of a limited competition, to which the city had invited six internationally renowned architects".

3."The modern architecture is an expression of progressive thought and reflects the use of the building, it signals transparency through the glass rotunda while the main.

 [http://www.dortmund.de/en/about_dortmund/news_en/news.jsp?nid=301134]

Nikajikuta ninajifunza mambo mengi kuliko nilivyotarajia:

YAANI:
1. Majengo yana uhusiano, hatupaswi kuyatazama kiubinafsi binafsi





2. Ushindani ni muhimu kwenye kila sekta
3. Tunapofikiria KUJENGA ni vema kufikiria MILELE kuliko siku mbili za USONI. Kuhusisha FIKRA za wajao pia, maana ndio watakao tumia zaidi yetu sisi.
4. Majengo yetu yana kazi nyingi zaidi ya kutuhifadhi, na mafanikio ya wahusika wa ujenzi ni kwenye kuzifanikisha hizi kazi zingine, maana ndizo nyingi na hasa ndio sababu ya kuwepo kwa jengo hilo.


N.K

Kwa kweli kwa mtazamo wangu, kitendo cha kuweka ART hii KIMEJENGA JIJI kwa maana ya kuyafanya hata MAJENGO mengine kuwa na HADHI tofauti na ile iliyokuwepo mwanzo. Kulifikia Hili sio rahisi kama WASHITIRI hawatakuwa mstari wa Mbele Kuwaacha Wataalamu wafanye kazi, na Pia tunahitaji mazingira sahihi ya kuyaweza haya.


JENGO LINAVYOINGILIANA NA MENGINE NA KUYABORESHA KIMUONEKANO
....................Itaendelea......................

0 comments:

Post a Comment