Monday, May 19, 2014

"Penye UONGO, UKWELI pia HUJITENGA"

Baada ya kuona maswala ya SIASA siyaelewi kabisa (Hasa kwenye mchakato wa katiba), nikaona nifungue kidogo Falsafa na Sayansi ya mambo ya Kisiasa. Nikajifunza mengi tu na kwa kifupi, nikaona kuwa mambo yahusuyo taratibu tulizonazo kama KUUNDA KATIBA wanaweza kutusaidia wataalamu hawa kabisa,
ikiwemo na kutupatia muongozo wa nini kifuate baada ya kipi, kama tutaamua kwenda kwa stepu!

Baada ya kuuliza hapa na pale, nikasikia wataalamu walipewa nafasi wakatoa mawazo mengi likiwemo la MUUNDO WA SERIKALI/MUUNGANO UNAOTUFAA KUWA NI -WA MOJA-:

Sasa, kila kukicha Mara UKAWA,mara MBILI, mara TATU! Jamani, kwani hatuwezi KUWAITA TENA wakatuelezea wananchi MBELE YA BUNGE ili, wanaobisha nao wawabishie KWA hoja! Kuna maana gani ya kukaa tunapoteza PESA ZA WAKULIMA, kusomesha watu halafu wakiwa tayari kutumikia taifa, tunawaambia WABAKI na mambo yao ya VITABUNI? Kama wanatudanganya, waadhibiwe basi!

Wakati umefika, tuheshimu ya VITABUNI, hata kwa kujitahidi KUYAKARIBIA TU. Naamini, Hivyo ndivyo wenzetu walivyofanya na kufanikiwa. Mimi naamini kama kweli SIASA ni UTAALAMU, lazima JIBU LIKO MOJA LINALOTUFAA, NA kushindwa KULIPATA, ndio kunapelekea mabishano, kwa SABABU kama penye UKWELI UONGO HUJITENGA, basi penye UONGO, UKWELI pia HUJITENGA. Sasa kwenye mambo ya MAANA hatupaswi kucheza PATAPOTEA, tufuate watu wenye HIYO TAALUMA kwanza!



0 comments:

Post a Comment