Tuesday, May 13, 2014

NDOTO YANGU 2014




Nini hasa yako ndoto, Yangu niwepo Khatari

Leo nimeota ndoto, Niko nchini Khatari
Bado damu yangu moto, Napiga pamba hatari

Sema yako wewe ndoto, Ona Mbali tafakari
Wengi wetu tuna ndoto, Utajiri tukithiri.
Tuselebuke na toto, Wajue chetu kiburi.
Wafe kama viroboto, Sisi tuzidi nawiri.
Nini hasa yako ndoto, Yangu niwepo Khatari

Miaka nane si mbali,Bulata kisha kubali.
Yeye ndiye lijabali, Ya rushwa sitajadili.
Niwaone Brazili,Laivu naikubali.
Hilisitaki jadili, Uswahili sikubali.
Nikivua kandambili, Jua ninaenda mabli.
Ndoto kanipa jalali, Sijapata kwa kamali.
Nini hasa yako ndoto, Yangu niwepo Khatari

Sitaki kuabudiwa,Kesho niwe kwenye moto
Ama mfisadi kuwa, Nchi kuitia moto.
Vyao watu kunyakuwa,Kulimbikiza vipato.
Sito yauza madawa, Kinga wakose watoto.
Sitaki mimi chachawa, Dunia mengi mapito.
Hata kama nimenawa, Chakula bado cha moto.
Nini hasa yako ndoto, Yangu niwepo Khatari


Mungu atupe neema, Kipato kilicho safi.
Tupate Hija salama,Roho zizidi usafi.
Timize ndoto karima, Nyunyiza wake usafi.
Tuziote ndoto njema, Ziso utaka Ulafi.
Tusibaki kukoroma, Vitambini tusosafi
Tuwaote Wakulima,Wasovuna Mikomafi.
Nini hasa yako ndoto, Yangu niwepo Khatari













0 comments:

Post a Comment