Sunday, September 22, 2013

MISS WORLD TANZANIA-Baadhi walalamikia Maandalizi

Newly crowned Miss World Tanzania 2014 Happiness Watimanya
Happiness Watimanya Miss World Tanzania 2014 (C) and her runners-up
 http://beautypageantnews.com/happiness-watimanya-crowned-miss-world-tanzania-2014/
 
BEAUTY PAGEANT NEWS Covering local, national and international beauty contests Photos of Miss Universe 2012 Olivia Culpo

Kwenye kurasa kadhaa za facebook, washabiki wamelaumu ZAWADI na BURUDANI kuwa hazikuwa na muendelezo.

 POST

Hawa waandaaji wa Miss Tanzania inabidi watathmini zawadi zao kwa mamiss.Inakuwaje Miss wa miaka miwili nyuma apewe Jeep ya zaidi ya Mil 50 halafu huyu wa leo apewe IST ya mil 10? Mashindano yao yanapanda thamani au yanashuka?Zawadi zinatakiwa ziwe na consistency au ziwe na trend ya kuongezeka with time.

COMMENTS
  •  nimeona huruma zawadi gani hiyo sasa??

  • By the way. Huu umiss unafaida gani kwa mtanzania? Natamani kuona tukiweka support Kwenye vitu vzr kama dance mia mia.

  •  Jamani this is to empower women.Kama sikosei ni MDG 6.

  • Kutokana na uvivu wa kufikiri wa watanzania, watu wanaweka mkazo mwingiii kwenye mambo ya KIJINGA/KIPUUUZII na kuacha masuala ya MSINGI katika HUMAN DEVELOPMENT...Hata kikija CHAMA kingine...bila wananchi kubadili THINKING PERSPECTIVE...hakutakuwa na JIPYAAA

  • kWA mtindo huu,kuna siku atapewa mtu zawadi ya ipad!

  •  Millennium Development goal? Yusuph be serious.

  • ..nakumbuka kuna mwaka walisema wanamjengea mshindi nyumba...daaaahhh kumbe ilikuwa changa la macho

  • Japo na hela kapewa ila jamani sponsors wote wale IST japo cna ila hapana unatoa lak1 kwenda kuangalia m2 akikabidhiwa IST

  • Ha ha haa! Jeep, Ist 2013, Vitz 2014, Starlet 2015, Bajaj 2016, Toyo 2017, Basket 2018 na PUnda 2019 safi sana Lundenga kwa strategies za kuua umiss.

  • jamani ee waliulizwa wote kabla zwd aijanunuliwa wengi wao wakasema IST ndo wanaipenda ndo ikanunuliwa so walaumuni ao mamiss ila mill 8 cash c mchezo watu wanamkopo bnk yeye walaaaaa..!sielewi wadada wanaipendea nn ist and alonunuliwa jeep kuiaford ni kasheshe wanaishia kupaki

  •  Flora Msolla IST it cost maximum 8M full registered, we are not asking for type of car but does miss Tanzania comittee consider value for money? Huu ni uchakachuaji wa halibut ya juu.. Kwanza anzia burudani wasanii wawili tu? Flora nilishiriki ktk uandaaji wa miss tz 2008 wasanii walikuwa wakutosha pale leaders hii ya Leo ni dalili ya kumaliza umiss lundenga amekaribia kustafu arudi kwa MAHENGE

  •  yah burudan wamechemka wamewekeza steji tu ..ila gari wamejishaua ao watoto wakomeee

  • Mi nahisi waliopewa magari makubwa walilalamikia mafuta wakaona isiwe tabu tutatoa an economic car.

  • mi nasubiri nimwone mwenye talent znazoendana na akina sepetua nianze mikakati mapema kabla bongo movie hawajaniwahi

  • Yaani ..................wewe umeenda nje kabisa ya mada.Sijui nani alikuvuruga dogo?Aaaahhh nimekumbuka, the Saints jana................tuliposema IST hatumaanishi aina ya gari.Tulichomaanisha ni zawadi husika.Hata wale mamiss wengine walipewa pesa pia on top of gari. Issue ni kwamba tulipenda kuona kama alivyosema............... hapo juu kwamba thamani ya kipesa yaani money equivalent ya hao mamiss inaongezeka time after time.Kama mwaka juzi alipewa Jeep ya 50M mwaka huu kama atajengewa nyumba,apewe baiskeli au chochote,basi kiwe na equivalent ya 50+M. Na kusema hawa walichagua zawadi nafikiri logic yake ni ndogo sana.Watoto wa shule hawa leo uwaambie wachague zawadi wenyewe.Zawadi hutathminiwa na waandaaji, wakihusisha watu wenye uelewa mkubwa wa mambo hayo,kutazama itasaidia vipi kunogesha mashindano lakini pia iwe na uhalisia wa kureflect thamani ya shindano lenyewe.Na zawadi hutengenezwa kuanzia kwenye bajeti ya mashindano hivyo lazima ihusishe expected revenue collections and expenditure juu ya tukio lenyewe.Hawa hata kama wliulizwa huenda waliulizwa tu kati ya VITZ na IST mngependa mshindi apewe nini? Lakini ki ufahamu halisi they are degrading the contest. Lwitiko Subi E yeah ni MDG 3, PROMOTE GENDER EQUALITY AND EMPOWER WOMEN. Sasa kwenye empower women kunahusisha kuwapa vitu mbalimbali ambavyo vinafall kwenye fursa za wanawake.Si unajua umiss ni wenyewe tu. Inwachangamsha watoto wa kike. Lakini wote lazima tukubali kuwa kuchagua zawadi ni kazi ya waandaaji.Na si lazima kutoa magari makubwa,toa kitu chenye thamani kubwa in money equivalent to reflect positive trend and the time value of money.

  •   I gave you the hiden sense of MDG! may be it is time you start your own research on the 8 goals! Great analysis, with such ZAWADI! Something is wrong somewhere!

    • Yaani inaniuma watoto Hawa kupewa samaki badala ya ndoano


    Angalizo kutoka TANKINI

    Wasanii wa leo wa Kitanzania sio wa jana. kwa kiasi kikubwa wanajitambua, na kujua kuwa sanaa ni kazi yao ya msingi! Hivyo huwezi kuwaburuza, kitu ambacho pengine kilipelekea wengi wao kutokubali kushiriki onyesho hili kwa bei ndogo! Mfano ni uwepo wa wasanii wengi katika onyesho la FIESTA usiku huo MUSOMA. http://www.cloudsfm.co/profiles/blogs/serengeti-fiesta-2013-musoma-ni-nouma-saaana-usiku-huu-ndani-ya-u

     
    Kundi la Wanaume TMK Halisi likiongoza na msanii nguli Juna Nature wakilishambulia vyema jukwaa usiku huu kwa staili yao mapanga shaa shaa,huku mayowe yakipigwa kutoka mashabiki.
Anaitwa Linah Sanga,kutoka nyumba ya vipaji THT akiimba jukwaani usiku huu
 Wakali wengine wanaokuja kwa kasi katika anga bongofleva-hip hop,Stamina na Youngkiller wakilishambulia jukwaa kwa kushusha mistari mikavu live.
Kama haitoshi, sababu za kijamii kama vile, picha mbaya inayotolewa na baadhi ya WASHINDI wa siku za nyuma onyesho hilo, huenda yakawa yamepelekea kushuka thamani kwa onyesho hilo na hivyo kuwafanya wadhamini kutokuwa tayari kutoa pesa nyingi kwa ajili ya onyesho hilo. Na hatimaye kukosa uwezo wa kuwa uendelevu wa ubora wa zawadi. Ama pengine kukoseakana kwa ushirikiano mzuri baina ya waandaaji wa MISS TANZANIA na vyombo vyenye uzoefu na mambo ya burudani kama CLOUDS NA BENCHMARK, kitu ambacho kimepelekea kuwa kugongana kwa maonyesho kadhaa na hivyo kupandisha gharama za wasanii na vitu kama hivyo.

Pengine pia imefika wakati, ambao WAANDAAJI wa onyesho hilo KUBADILIKA, maana kila kitu, kinafikia hatua fulani huhitaji, mabadiliko MAKUBWA ya kiutendaji,kiundeshaji,kimfumo,kiuzalishaji na kimbinu, na hata ikibidi KIUONGOZI kabisa. Hili kwetu linaweza kuwa jambo gumu, kwa sababu tu ya UBINAFSI wetu,lakini sio jambo la ajabu. Tumejionea mara nyingi vitu vyenye ubunifu mzuri kabisa vinafikia mahali vinakufakwa sababu tu ya kukosekana kwa mwanya wa mabadiliko sahihi. Simba,Yanga,Bongo Star Search, na hata Taifa kwa ujumla, wajiangalie katika hili pia! Japo kwa hatua kadhaa tunazozishuhudia, WAANZILISHI wanastahili PONGEZI kubwa SAAANA. Mfano ni LUNDENGA MADAM Rita.

Lakini, kwa malizia tu kizushi, pengine MAMISS hawana uwezo wa kukataa ZAWADI, hivyo wanaamliwa, mtindo wa "KAMA HUTAKI TOKA", maana siku za mwanzo, lazima UMDANGANYE mtu kwa zawadi nzurinzuri (MACHONI PAKE),hata kama hazina maana sana katika maisha yake ya baadae, na baada ya KUUVAA mtego, mavuno yanaanza. Na pia HUENDA ni sisi tu WABONGO, mabingwa wa kulaumu, KILA KITU. Hata tujengewe BARABARA ya magari yaendayo kasi, na kuletewa TRENI, bado utasikia hakuna kilichofanyika.


5 comments:

  1. This comment has been removed by the author.

    ReplyDelete
  2. Tatizo la watanzania ni; kushupalia vionekanavyo badala ya vimaanishavyo na hivyo vionekanavyo.

    Mfano nikiwauliza hao waliotoa maoni hapo, nini maana ya mashindano ya Urembo? ni wachache sana watakaoona kuwa hilo linaweza kuwa swali.

    Kwa mtazamo wangu, wangeweza kupewa hata baiskeli za magurudumu matatu wakatoe kwa walemavu na bado maana ya hayo mashindano ikabaki palepale.

    Suala la burudani na gharama za kiingilio kwangu sioni kama linamashiko. Hasa tukirudi kwenye maana. Ukiijua maana huwezi hata kwenda kwenye huo ukumbi kunakofanyika huo utambulisho!
    Hii ipo hata katika michezo mingine. Mimi huishia kushangaa.

    Kuna usemi '' THE BEST THINGS IN LIFE ARE FREE ''. Na pia '' UKITAKA KUJUA UMUHIMU WA MKIA, UKATWE ''. Kuna vitu tusipokuwanavyo ndio tutajua namna ya kuwanavyo kiufasaha.

    Kusiwe na zawadi, Tusiwe na mashindano ya urembo, Tusiwe na timu ya taifa. Tujitathmini kwanza, sisi ni nini na ni nani? Huenda tukapunguza malalamiko kwa hoja zisizo nzito.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Wanacholaumu ni kuwa HAKUNA muendelezo, siku kadhaa walimpatia miss gari ya thamani sana, lakini leo wamerudisha nyuma thamani! Kimsingi, wao wangeona vema, kama leo zawadi ni sh 10, basi kesho zawadi iende mbele na kuwa sh 11, na sio sh 9 au 5! hata kama ni baiskeli za walemavu, basi zifikie zaidi ya pesa iliyopita! Burudani, ni sehemu mojawapo ya onyesho hilo, na wanaamini husaidi kupendezesha onyesho! na huku wakiamini kuwa pesa ilikuwepo,iweje kukosekane burudani za kutosha kulingana na siku za nyuma?

      of course, mwanzo wa kitu, huwa nivizuri mtu kujitambua kuwa yeye ni nani hasa, na pengine kupata picha halisi ya uwepo wake duniani, lakini,fikiria kuwa tayari hawa wamepita hiyo hatua, na kuona sasa wanahitaji onyesho hilo, na kisha wakahudhuria miaka miwili mfululizo, na kuona jinsi linavyofana, kisha ghafla leo inakuwa hivyo ilivyokuwa. Ungekuwa na lipi la kushauri, kama unalifahamu onyesho lenyewe!!!!Baraka Nzoshe

      Delete
    2. Nidhanivyo mimi ni; Kuna maana ya mashindano ya urembo, ambayo siioni kuwa ni pesa au mali. Labda nipewe maelezo ya kutosha.

      Delete
    3. Ahahahahaha!!

      OK-FROM
      http://en.wikipedia.org/wiki/Beauty_pageant

      A beauty pageant or beauty contest, is a competition that mainly focuses on the physical beauty of its contestants, although such contests also incorporate personality, intelligence, talent, and answers to judges' questions as judged criteria. .................... Possible awards include titles, tiaras or crowns, sashes, savings bonds, and cash prizes.

      Purpose

      When beauty pageants began, they were viewed as "trivial events whose interpretation required no scholarly effort".[citation needed] Miss America, the first pageant of its kind, has made an effort to ensure that it does not appear as a "stereotypical" pageant.[citation needed]

      ............
      Another stated goal of pageants is promoting self-esteem and public-speaking abilities of the contestants.[citation needed] Winners of these pageants have said that they feel a sense of accomplishment.[citation needed]


      Some pageants award college scholarships, to the winner or multiple runners-up.

      GLOBALLY

      Major international contests for women include the yearly Miss World competition (founded by Eric Morley in 1951), Miss Universe (founded in 1952), Miss International (founded in 1960) and Miss Earth (founded in 2001 with environmental awareness as its concern).[12][13][14] These are considered the "Big Four" pageants, the four largest and most famous international beauty contests.[15][16]

      During the 1950s, pageants thrived to promote county fairs and local products. For example, some of Raquel Welch's titles included " Maid of San Diego County", " Maid of California" "Miss Photogenic" and "Miss Contour." Women from around the world participate each year in local competitions for the chance to represent their country's international title.

      2002 was a year remarkable for its number of winners from countries with a majority Muslim population. In that year Miss Lebanon, Christina Sawaya won the Miss International pageant, Miss Turkey, Azra Akın won Miss World, and the original winner of Miss Earth for that year was Džejla Glavović from Bosnia and Herzegovina (before being replaced by Winfred Omwakwe of Kenya). In 2006, the Muslim nation of Pakistan crowned its first Miss Bikini Universe, Mariyah Moten, which later became a controversy worldwide.

      CRITICISM. Critics of beauty contests argue that such contests reinforce the idea that girls and women should be valued primarily for their physical appearance, and that this puts tremendous pressure on women to conform to conventional beauty standards by spending time and money on fashion, cosmetics, hair styling and even cosmetic surgery. They claim that this pursuit of physical beauty even encourages some women to diet to the point of harming themselves.[18][19][20]

      KWA HIYO, kifupi hata SHINDANO HILO linaangukia karibia SAWA na maelezo haya. Kuwa zamani malengo hayakuwa ZAIDI kwenye PESA, lakini kama ilivyo ada ya vitu vingi huanza kwa KUJITOLEA, na baadae hufuatia MOTISHA mbalimbali, kama PESA n.k. Na kwa maana hiyo leo tulipo, motisha hizo ni pamoja na Pesa AMBAZO zinapaswa kuwa na CONSISTENCY, kwa mujibu wa WAZALENDO hili halikupewa uzito kwene ONYESHO hili KWA MSHINDI wa mwaka huu, tofauti na miaka kadhaa ilyopita.

      Delete