Saturday, September 21, 2013

MBEYA CITY AGAIN

Kile kilichokuwa kikisubiriwa na wapenda soka wengi Tanzania leo kimetimia. Matokeo ya mchezo kati ya mabingwa kutandaza Soka nchini Tanzania, Simba Sports Club na Vijana machachari kutoka Mbeya, yamedhihirisha kuwa Mabingwa watetezi Dar Young Africans hawana haki ya kuidharau timu ya Mbeya City
pamoja na ukweli kuwa ndio msimu wao wa kwanza katika Ligi kuu nchini Tanzania. Shaffi Dauda,kam kawaida iliendelea kutuletea mchezo huo hatua kwa hatua,http://www.shaffihdauda.com/, huku ikitoa taswira sahihi kabisa ya mchezo kuwa ulikuwa mgumua na wa vuta nikuvute, mpaka kufikia matokeo ya 2-2. Mbeya City sasa wamethibitisha kuwa WANASTAHILI KUBAKI LIGI KUU, na kugombea UBINGWA wa TANZANIA.

Mbeya city ni timu, iliyotabiriwa kufanya vema kutokana na historia yake katika ligi daraja la kwanza, ambapo, likuwa ikionyesha mchezo mzuri sana na kuongoza makundi yake japo, haikufanikiwa kupanda daraja kwa msimu 2012/2013,sababu ikiwa ni kukosekana kwa uzoefu na zaidi ikiwa ni mfumo mbaya wa vituo ambao unadhaniwa kuwa ulipelekea mara nyingi baadhi ya timu KUBEBWA. mwaka uliofuata, kukiwa na mabadiliko ya mfumo,na kurudishwa mfumo wa ligi,Mbeya City, waliongoza tena kundi na kujihakikishia kupanda daraja, kabla ya mechi kadhaa, ikisaidiwa na uzoefu wa wachezaji WAKONGWE kama AMANI SIMBA na MANDANJE, waliongezwa ili kuondoa upungufu wa kukosekana kwa UZOEFU katika timu.

Kikubwa hapa,cha kujiuliza ni kama mafanikio ya Mbeya City ni Endelevu? ukizingatia kuwa ni timu iliyo chini ya Halmashauri ya Jiji? Na ni nini siri yake? Je Wananchi wa Mbeya ni kweli wamedhamiria kuwa mfano kwa Taifa zima, kuacha kuwa washabiki wa SIMBA NA YANGA, bila faida kwa mikoa yao? Tanki linaahidi kufuatilia haya pia.

Pia, ni VEMA TFF wakajiuliza na kupima matokeo ya TIMU zilizopanda msimu huu na zile za misimu kadhaa,kutokana na MFUMO wa makundi. Hii itasaidia kutafakari soka na mafanikio yake. LIGI BORA ndio siri ya MAFANIKIO ya soka katika nchi ya TANZANIA.

Mwisho, ni kwa Simba, vyovyote iwavyo,Kuswazishiwa GOLI mbili na timu kama MBEYA CITY, ni MUSHIKERI kidogo, nivema wakajiuliza hasa tatizo ni nini, UWEZO wa Mbeya City? Upungufu wa Simba? Wapi, pumzi kama siku kadhaa nyuma?Mbinu hafifu ama? N.K. na je vipi ikiwa Enyimba ama Al Ahli?
Vijana wa Mbeya City wakitoka nje ya uwanja, Picha na Gabriel Mwang'onda!

Shabiki la Mbeya City!Picha na Gabriel Mwang'onda!

Baadhi ya mashabiki wa Simba wakiwa hawaamini kilichotokea,Picha na Gabriel Mwang'onda!


Mashabiki wa Mbeya City walivyochafua Uwanja wa Taifa
Mtiririko wa mechi kwa mujibu wa Shaffi Dauda Blog!http://www.shaffihdauda.com/
Full time Mbeya City wanalazimisha suluhu na Simba.

DK 90: Simba 2 - 2 Mbeya City

Dk 85 Betram Mwombeki anakosa bao la wazi akiwa ndani ya eneo la hatari la Mbeya City 

Dk 79 Sub: Simba inafanya mabadiliko ametoka Amri Kiemba ameingia Ramadhan Singano 

DK 75: Simba 2-2 Mbeya City

DK 65: GOOOOO Mbeya City wanapata bao la kusawazisha.

DK 55: Simba 2-1 Mbeya City

Mpira ni mapumziko 

DK 45: Simba 2-1 Mbeya City

DK 37 Paul Nonga anaipatia Mbeya City bao la kwanza. Simba 2-1 Mbeya City

DK 31: Tambwe anafunga bao lake la sita katika mechi mbili - Simba 2-0 Mbeya City

DK 29: Amis Tambwe anaipatia Simba bao la kuongoza

DK DK 10 - Simba SC 0-0 Mbeya City

Mpira umeanza katika dimba la uwanja wa Taifa Simba 0-0 Mbeya City

0 comments:

Post a Comment