Mechi baina ya MBEYA CITY ya jijini Mbeya na YANGA yenye
makao yake jijini Dar Es Salaam, zimetoka uwanjani na kukubali kuambulia pointi
moja kila moja baada matokeo halali ya 1-1.
“Timu za Yanga na Mbeya City leo zimetoka sale ya goli 1-1 katika mchezo
mkali na wa kusisimua uliofanyika katika uwanja wa Sokoine Jijini Mbeya. Timu
ya Mbeya City ndiyo ilikuwa ya kwanza kupata bao katika dakika ya 50,
liliofungwa na Mogani..............................................
Timu ya Yanga ilisawazisha goli katika dakika ya 75 goli lililofungwa
Kavumbagu kwa kifua na kumuacha golikipa wa Mbeya City akigalagala bila
mafanikio ya kuokoa mpira uliokuwa ukienda wavuni polepole.......................................................................................................................
Timu ya Yanga ndiyo iliyokuwa ya kwanza kuingia uwanjani saa 9:15, timu
hii iliingia kwa mbwembwe huku basi lililobeba wachezaji likipita upande
walikokuwa mashabiki wa Mbeya City, shabiki asiyejulikana wa Mbeya City
alililirushia chupa ya bia basi hilo na kuvunja kioo cha pembeni cha
mlango wa dereva na kumjeruhi dereva wa basi hilo, hali iliyoleta
mtafaruku mkubwa kwa viongozi wa timu ya Yanga.” http://basahama.blogspot.de/
Tanki, lina mawili matatu juu ya matukio yote ya mchezo kama
ifuatavyo:
1. Mtazamo wa mechi
Kifikra
Washabiki wengi wanaonglea mchezo
kuwa ulikuwa mkali, kitu ambacho ni kawaida sana kwa Tanzania. Japo, kwa kuyatazama
matokeo, jambo hili linakribiana na ukweli sana. Yanga moja kati ya timu kongwe
nchini, ikiwa ni pamoja na watani zao Simba (ambao wao wamefanikiwa kuwalaza
Mtibwa 2-0), ina rasilimali nyingi sana (Ikiwa ni pamoja na kuwa Bingwa
mtetezi) ukifananisha na Mbeya City. Hivyo, ukali wa mchezo huo kwa kiasi
kikubwa unachangiwa na ukweli kuwa MBEYA CITY, wamekuwa wakijaribu kuthibitisha
uwezo wao. Jambo hilo,bila shaka vijana hao wa Kocha maarufu Mwambusi,
wamefanikiwa kuuonyesha, na hasa ukizingatia baadhi ya matokeo yao ya
kuridhisha waliyopata siku za nyuma. Japo,kukataliwa kwa goli moja la Yanga
kuna paswa kuwafanya MBEYA CITY, watambue hasa wapi walipo kisoka,na
kutojisahau na kulewa sifa.
Mambo mengine kadhaa yanayoweza
kuambatana na matokeo haya, ni aidha Ligi ya Tanzania bado ni dhaifu, ndio
maana vinara wa soka hawana uwezo wa kuzifunga timu ndogo, ama pia kinyume
chake,yaani ligi sasa inaanza kuwa bora, kwa timu ndogo na ngeni kutoa
ushindani sahihi kwa mabingwa watetezi. Lah pengine ubabaishaji wa mambo kama
vile uzalendo na kupenda timu au rushwa za kijinga, umepelekea timu moja wapo
kutotoka na ushindi.
Jambo kubwa, la kulitazama pia
katika mechi hii ni swala zima la uzito wa timu hizi mbili. Mbeya City haijai
kwenye KIGANJA cha Yanga. Lakini kuna washabiki kadhaa, wamefurahishwa na uwezo
ulioneshwa na vijana wa MBEYA CITY. Hili linatufundishwa kuwa UWEZO UPO, sio
mpaka tutafute wachezaji NCHI za watu, wakati mafanikio hatuyaoni, ZAIDI ya
kuwapatia PESA nyingi sana. Tuthamini vyetu, ili VITUFAE jamani. Na Zaidi, ni
kuwa hizi TIMU zetu kubwa zinazoonekana kama ndio msingi wa soka zinapaswa
kujifunza hilo sana,zinaweza kutanua wigo wa miliki zao na kupta wachezaji toka
mikoani. Na Zaidi TFF, kujifunza kuwa SOKA la BONGO, kwa ujumla haliishii JIJI
la DAR, kuna umuhimu wa kuboresha MAONO yake na kuzikia timu za mikoani, badal
ya kuzifanya wasindikizaji wa SIMBA NA YANGA.
2. Mtazamo wa TUKIO Kifikra
Mechi imekuwa gumzo, na
shamrashamra nyingi sana katika jiji la mbeya. Kuna mengi mazuri ya kufurahisha
na mabaya ya kusikitisha yaliyojitokeza kama ambavyo picha zimeripotiwa na Basahama.kila
mtu ananafisi ya kuyachambua haya kwa jinsi anavyoweza, lakini Tanki lina haya machache
kwa Watnzania na Wana Mbeya, walio mashabiki na wasio mashabiki wa SOKA la
BONGO.
·
UMUHIMU WA MICHEZO
Ni vema
sasa wana MBEYA, tukaona umuhimu wa michezo, kuwa ni Zaidi ya ajira za ualimu
ama kazi nyingine amabzo tumekuwa kila siku tukizipa kipa umbele, kwa sababu
MPIRA humgusa kila mtu kuanzia mpiga debe mpaka muuza juice. Mabil na vijana
wetu wenyewe na pengina faida mbalimbali za kiafya na kadhalika. HUU ni UCHIZI
wa DUNIA, sasa TUCHIZIKE NAO. Timu zetu zipewe kipaumbele, na mipango
madhubuti, iwekwe. Isije ikawa Mbeya City, kesho akiondoka Fulani,inaanza
kusuasua, kama vile ilikuwa inamnufaisha yeye, wote tulishuhudia uwanja wa
sokoine ulivyodolola siku kadhaa tulipokuwa hatuna timu katika LIGI KUU. Hata
JIJI pia lililala kabisaaaaaa! Leo hii, watu kutoka Tunduma, Chunya na Tukuyu
wanaungana uwanja wa SOKOINE, nafikiri wanauchumi wanaweza kutueleza ni kiasi
gani mechi hiyo imeinufaisha MBEYA nzima, mbali na YANGA, MBEYA CITY na WALE
AKINANIHII wanaotuzuilia maendeleo ya SOKA.
·
UWANJA WA SOKOINE
Jamani,
tumeona jinsi gani UWANJA ulivyombovu, kuanzia kweny sehemu ya kuchezea, mpaka
sehemu za kukaa. Hivi haya nayo tunasubiri AFUFUKE MWALIMU aje aseme WANAMBEYA
rekebisheni uwanja wa SOKOINE. Hata kupigwa chupa kwa gari la Yanga ,ni
kukosekana kwa usalama wa kisasa, ambapo wachezaji wanaingia uwanjani kwa
usalama kabisa. Sisi si wendazawazimu wa soka kiasi hicho, ukilinganisha na nchi
fulanifulani duniani. Ukiuliza utaambiwa, uwanja ni wa FULANI, hivyo, sijui
kikaenda kikarudi,siasa tupu. Kama FULANI ndio mwenye uwanja,basi atambue ni
kiasi gani, amekalia pesa, na ni kiasi gani analiumiza jiji na ni kiasi gani
anawanyima wananchi wa Mbeya maendeleo ya kweli, lakini zaidi huu ni UZEMBE WETU
WANA MBEYA tu. Tunashindwa kukarabati
uwanja, na hata IKIBIDI KUJENGA uwanja MPYA wa maana ukabadili na SURA ya jiji
letu?
Chochote,
kinachotuzuia WANAMBEYA kuwa na UWANJA bora wa SOKA, tukichukie kama UKOMA.
PESA ZIPO, WATAALAMU wapo, na UWEZO UPO kabisa. Kinachokosekana ni FIKRA BORA
TU, na NIA. Ubinafsi, umetujaa, hakuna anayeangalia watoto wetu kesho wanahitaji
nini, tunakula mpaka kile tutakachokihitaji wakati wa uzee wetu! Kila kitu,
tunaamini kinatakiwa kiwe DAR!
BAADHI YA PICHA ZA TUKIO ZIMA NI HIZI HAPA (CHANZO: BASAHAMA BLOG)
BASI LA YANGA |
MASHABIKI WA MBEYA CITY |
MASHABIKI WA YANGA |
MASHABIKI WA YANGA WAKITOKEA TUNDUMA |
WANA HABARI MBALIMBALI MBELE YA SEHEMU MAALUMU YA UWANJA |
KIKOSI CHA MBEYA CITY DHIDI YA YANGA |
GARI LA YANGA,SEHEMU ILIYOPIGWA TUPIWA CHUPA NA KUMJERUHI KIONGOZI MMOJA |
VIKOSI VIKIKAGULIWA |
MAKAPTENI WA TIMU WAKIPATA PICHA PAMOJA NA WAAMUZI |
KIKOSI CHA YANGA DHIDI YA MBEYA CITY |
0 comments:
Post a Comment