Friday, July 26, 2019

Safari ya Mpaju FC- Mbalali (Meta- Shule ya Msingi Mpolo)

Kama ilivyo kawaida ya Mpaju Sports Centre,mwaka huu pia walifanya ziara ya Mechi za kirafiki katika Kijiji cha Meta,Mbalali Mbeya ili kucheza michezo kadhaa ya kirafiki na timu za Shule ya Mpolo waliokuwa wenyeji wao na Timu ya Timba Timba ya Kijijini Hapo waliocheza na Mpaju FC-
U20. Mambo kwa kifupi yalikuwa kama zinavyojieleza picha.

Tunamshukuru Mungu kwa kuwezesha safari yetu na kutulinda. Kwa mara ya kwanza wachezaji wote waliwahi na kutufanya tuanze safari kwa wakati kabisa. Kwa Mpaju FC, swala hili la kuwahi, lilimaanisha mafanikio makubwa sana ya safari hii.
Tulifika kwa wakati kabisa Shule ya Msingi Mpolo katika kijiji cha Meta na mapokezi yalikuwa mazuri ikiwa ni pamoja na kupewa Darasa kwa Ajili ya Maandalizi yote
Vijana wa Mpolo U-12 wakipasha misuli moto tayari kuwakabili Mpaju FC U-12.


Vijana wa Mpaju U-12 wakipasha misuli moto tayari kuwakabili Mpolo U-12


Mwalimu Kocha Nsyani wa Mpolo Shule ya msingi(Blue T shirt), na Kocha wa Mpaju Abdallah Athumani (a.k.a Dulayo) wakikagua timu za U 12 kabla ya kuumana vikali na kutoa burudani ya hali ya juu

Picha ya Pamoja kwa U-12 Mechi, na kama picha inavyojieleza, mchezo ulishuhudia vipaji hatari kutoka kwa mabinti kadhaa wa timu ya Mpolo shule ya msingi. Hongera sana Kocha Nsyani kwa jitihada zako

Vijana wa Mpolo U-15 wakiwa katika piha ya pamoja tayari kuwakabili Mpaju FC U-15

Vijana wa Mpaju U-15 wakipasha misuli moto tayari kuwakabili Mpolo U-15

Mwalimu Kocha Nsyani wa Mpolo Shule ya msingi (Blue T shirt), akichukua matukio wakati timu za U 15 zikikaguliwa kabla ya kuumana vikali na kutoa burudani ya hali ya juu

Picha ya Pamoja kwa U-15 Mechi, mchezo ulishuhudia vipaji hatari kutoka kwa vijana kadhaa wa timu ya Mpolo shule ya msingi,pamoja na kuwa na maumbile madogo bado vijana wa Mpaju walishindwa kabisa kufurukuta. Hongera sana Kocha Nsyani kwa jitihada zako

Vijana wa Mpaju U-20 wakielekea kujiandaa na mchezo dhidi yatimu ya Timba Timba ya kijijii cha Meta

 Timu ya Timba Timba ya kijijii cha Meta wakiwa wanajiandaa kupambana na Mpaju U 20

Mechi iliyosubiriwa kwa hamu iliwadia, kati ya Timbatimba na Mpaju Fc U-20.  Baada ya Kukaguliwa picha ya pamoja ilipigwa kuashiria urafiki wa wa kudumu

Timu zikisalimiana, huku mashibiki wakionekana kutotaka kupitwa na jambo lolote

Mpaju U 20 wakisali kabla ya mchezo

TimbaTimba wakipongezana baada ya kusali

Picha ya Pamoja baada ya Mchezo kuisha salama, huku matokeo yakiwa ni suluhu ya magoli 2-2. Mpaju FC U 20 wanapenda kuwashukuru sana wachezaji wa timbatimba kwa mchezo mzuri na uwezo ulionyeshwa kwa ujumla. Hakika taifa lingeweka mkazo wa mchezo wa mpira kwenye maeneo yote pengine tatizo lililopo la washambuliaji wafungaji lisingeonekana kabisa.

Michezo iliisha salama na kati ya matukio muhimu ilikuwa ni lile zoezi la kupata chakula cha uhakika lililosimamiwa vema kabisa na mwali na kocha Nsyani. Vijana walifurahia sana huduma hii na vyote kwa ujumla wake. Mungu awazidishie wananchi na Viongozi wa Meta na shule ya msingi Mpolo.

3 comments: