Friday, June 21, 2019

Mpaju FC yaanza Kuitikisa Tanzania

Mpaju FC imetoa dalili nzuri kwa mafanikio ya kituo cha michezo cha Mpaju baada ya vijana wake watatu kufanikiwa kuwakilisha kituo kwa kushiriki mashindano ya kusaka vipaji ya TFF kupitia mkoa wa Mbeya. Vijana Emmanuel Mbwilo, Lango Mkomola na Ipyana Kakwale
ndio waliofanikiwa kuiwakilisha Mpaju FC katika hatua hiyo ya Mashindano kupitia Mkoa wa Mbeya. Mpaju FC inapenda kuwapongeza kwa uwakilishi mzuri wa wachezaji hawa pamoja na kuondolewa kwa timu yao katika hatua ya makundi.

Emmanuel Mbwilo ambaye Golikipa Mzuri lakini Pia alikuwa Mshambuliaji wa Kutumainiwa akipokea maeelekzo na Maji
Ipyana Kakwale (Fundi wa Mpira) akiingia kuonyesha uwezo wake na kwa Mbali beki wa Kushoto Lango Mkomola akiomba mpira kutoka kwa Golikipa

Mlezi wa Mpaju akiwa na Wachezaji wa Mpaju FC
Mdau wa Mpaju Hamisi Kopa akiwa na Wachezaji wa Mpaju FC


Waliochuchumaa kulia ni Ipyana Kakwale, waliosimama watatu kutoka kushoto ni Emmanuele Mbwilo, wa nne ni Kocha Paul ambaye alikuwa na timu katika mashindano hayo ya TFF na wa Tano ni Lango Mkomola. Wengine ni wachezaji kutoka timu zingine jijini Mbeya walioungana kuunda kikosi hicho wakiwa katika picha ya pamoja na mlezi wa mpaju baada ya kuwatembelea uwanja wa Karume Dar Es Salaam

Kocha Paul akitoa maelekezo wakati wa mapumziko

Picha kabla ya mchezo

Salamu kabla ya mchezo

0 comments:

Post a Comment