Sunday, February 17, 2013

Kilimo Kwanza: Ni Kauli Mbiu ya Msingi kwa Taifa?



 Watanzania tunahitaji kufahamu Imani na Misingi ya Taifa Letu.
Misingi ya Taifa letu ndio Roho ya Taifa Letu.
Kuilinda na Kuboresha Misingi Yetu,Ndio Kulinda na Kuboresha Taifa Letu


Umuhimu wa misingi sio tu kwa taifa, bali hata mtu binafsi na familia ama ukoo. Lazima kuwa na misingi ambayo ndio dira ya matendo na maamuzi yako au yenu. Mara nyingi tunapokosa kuwa na Misingi Bora huwa tunaishia kuyumba bila kujua chanzo hasa cha kuyumba ni nini. Hatujui mchawi hasa ni nani!



Mwalimu (Baba Wa Taifa) Julius Kambarage Nyerere: Kati ya hotuba zake 1982

 Alisema
Kwa sababu ya umuhimu wa kilimo katika maendeleo yetu ingetegemewa kuwa kilimo na mahitaji ya wakulima yangekuwa ndio chanzo na kupewa kipaumbele katika utayarishaji wa mipango yote ya uchumi wetu. Badala yake tumechukulia kilimo kama sekta ya pembezoni au kama shughuli nyingine yoyote ya kawaida ambayo inatumiwa na sekta nyingine bila yenyewe kupewa umuhimu wowote ule……………Tunakipuuza kilimo; kama tungekuwa hatukipuuzi, basi Wizara zote, mashirika ya umma yote na mikutano yote ya chama ingekuwa inafanya kazi kushughulikia mahitaji ya wakulima. Ni lazima sasa tuache kukipuuza kilimo. Ni lazima tukifanye kilimo ndio shina na mwanzo wa mipango yetu yote ya maendeleo. Kwani kwa hakika, Kilimo ndio msingi wa maendeleo yetu.

 Hotuba ya (Baba Wa Taifa) Mwalimu 1970, Bungeni.
 Said
"We are not in the position of choosing between luxuries and essentials. We are still so poor that we are choosing between the essentials themselves, and therefore leaving some of them undone.

In our situation, all that we can do is make sure that we use whatever resources we do have to good effect. We have to strive to increase our output by using properly what we already have. And if we do achieve an increase in production we have to resist the temptation to spend it all on personal consumption. First we have to put aside enough to buy the equivalent of the farmer's seed and replacement" jembe." Second, we must use some of the wealth to increase the availability of things like water, schools, hospitals and so on.

And it is essential also that we should devote some of our increases in wealth to investment in new production capacity -- that is buying machines for new factories, producing more electricity etc., because the number of Tanzanians able to work in the fields or in factories is increasing every year".

Jamhuri ya Indonesia

From Google search: en.wikipedia.org/wiki/Indonesia

Jamhuri ya Watu wa Indonesia ni mkusanyiko wa visiwa vipatavyo 17,508 hivi. Na idadi ya watu inazidi milioni 238 na ni kam nchi ya Tano kwa wingi wa watu duniani. Kuna mengi ya kuvutia, kama maamuzi yao ya kutumia lugha yao baada ya uhuru, mwaka 1945, lakini kilichofanya makala hii ndogo iwepo ni kuwepo kwa Imani na misingi iliyowekwa na Mtawala wa mwanzo kama Baba wa Taifa lao, Raisi Sukarno, yaani Pancasila, ikiwa na maana ya Kanuni Kuu Tano au Misingi Mitano. Hii waliamua kuwa itakuwa ni misingi ambayo ndio kiini cha nchi!

“Pancasila is a creed that Indonesia's first leader, President Sukarno, presented on June 1, 1945. To this day, it remains the philosophical basis of the Indonesian state.
Pancasila is based on two Sanskrit words: panca, or "five," and sila, which means "principles." It stands for the five inseparable and interrelated principles at the heart of Indonesia”.

Misingi yao ni

1. Belief in the one and only God
2. Just and civilized humanity
3. The unity of Indonesia
4. Democracy guided by the inner wisdom in the unanimity arising out of deliberations amongst representatives
5. Social justice for the whole of the people of Indonesia

Hii misingi ni vema kila mtu akajaribu kuitafsiri mwenyewe.Kikubwa hapa ni kuwa Waendonesia, walikubaliana kuwa hiyo misingi ifuatwe kama dira ya nchi yao tokea wakati wa Uhuru wao. Hivyo kila serikali inayoingia madarakani kimsingi inajua nini cha kufanya, japo inaweza kuja na njia tofauti au nyongeza.Pengine Hata nchi kubwa hufanya kitu kama hiki!Kama kauli mbiu Ya Kilimo Kwanza, inavyotumiwa na cham tawala cha CCM. Ili Kauli mbiu hii iwe Bora Na kupitishwa lazima iwe kwenye mtazamo wa Misingi na Imani ya Taifa.Tanzania Misingi hii pengine ni ile ya kwenye Katiba, ambayo iko kwenye mchakato wa marekebisho.

Umuhimu wa kuwa na Misingi ya Kitaifa ni kuweza kuwa na mwelekeo ambao mnaweza kuona bayana ni  wapi mnatoka na wapi mnakoelkea. Pia kufahamu yale ambayo ndio hasa ya msingi, na kutoyachanganya na yenye umuhimu kidogo. Kwa kuwa na Misingi mnaweza kujikagua kirahisi na kujirekebisha kirahisi. Na kwa kweli ingewezekana hata katiba ingeundwa kutokana na Imani na Misingi hii Hii misingi na imani inapaswa kutokea kutokana na mazingira halisi ya taifa kwa wakati inapoandikwa, na iweze kudumu kwa vizazi hadi zizazi kwa nyakati zao.

Umuhimu wa misingi sio tu kwa taifa, bali hata mtu binafsi na familia ama ukoo. Lazima kuwa na misingi ambayo ndio dira ya matendo na maamuzi yako au yenu. Mara nyingi tunapokosa kuwa na Misingi Bora huwa tunaishia kuyumba bila kujua chanzo hasa cha kuyumba ni nini. Hatujui mchawi hasa ni nani! na ndio hata mitazamo,itikadi au kauli mbiu zinaweza kutafsiriwa kama ni msingi na kuharibu kabisa mwenendo mzima wa taifa au familia. Fikiria, Familia ambayo msingi wao ni kudumisha dini yao,halafu anatokea mmoja wao na kwa tamaa tu ya pesa, anashauri kuhakikisha wanadhulumu nyumba akidai iwe ya familia kwa ajili ya ibada.Huyo anakuwa hayupo tena kwenye msingi ya kudhulumu, waliondaa misingi walichagua kudumisha dini ili dhuluma isiwepo kwa kuwa haina manufaa makubwa kwa familia.

Sasa, leo hii kama tunakubaliana kuwa KILIMO KWANZA ni kauli mbiu kuu, tufahamu na maana yake nini. Mwalimu alieleza wazi kabisa,kwamba maana yake kuanzia vyama mpaka taasisi za serikali zielekeze mipango yake kwanza kwenye KILIMO. Hapa hasa ni Mpaka fikra za wananchi zinapaswa kuwa na mwelekeo huo.Yaani Dira yetu ionekane sio tu kwa maneno yetu, bali pia kwenye vitendo vyetu vya kila siku na fikra zetu popote tulipo. Mfano: Mzee Majuto, alipokuwa katika kipindi cha Mkasi, (Google serach: you tube/ mkasi by salama jabri) aliomba asaidiwe Tractor aweze kuboresha Kilimo.Lilikuwa wazo hasa linaloendana kauli mbiu yetu na wazo hilo linapaswa kuwa pia linaendana na Misingi yetu ya Taifa, Kwa Mfano: Kama Msingi wetu ni utu ni kitu, maana yake Majuto hapaswi kupewa, lakini kama kuna msingi wa ujamaa na kujitegemea,anapaswa kusaidiwa pale alipofikia ili, mambo yawe safi kwa wote!

Kwa kuangalia umuhimu wa kuwa na Misingi bora, utagundua kuwa si jambo la mchezo kuamua juu ya Misingi na Kuamua juu ya jinsi ya kuisimamia misingi hiyo. Hapo ndipo,unakuja umuhimu wa kuwa na wale watakaowakilisha katika maamuzi juu ya Misingi ya Taifa (Soma zaidi Katiba ya Tanzania: Maamuzi yetu ndio Hatima yetu). Na hata katika Familia, lazima kuwe na mtu au watu ambao wanaweza kusema huu ndio mwelekeo au maamuzi yetu. Mara nyingi, inafaa awe BABA/MAMA. Kitaifa, BABA/MAMA/DOLA (soma zaidi juu ya BABA/MAMA katika makala ya “Mtanzania acha mipango ya Ujanjaujanja”), pia anahitaji kuulizwa kama anasimamia vema Misingi hiyo ya Kitaifa na kama taratibu zake zote zinalenga Misingi hiyo ya taifa? Chombo hiki chenye kuweza kuiongoza Dola kuhakikisha Misingi inasimamiwa vizuri hasa ndio kimeshika Roho ya Taifa, na kinapaswa kuwa  Sauti ya wananchi na uwawakilishi wa wananchi wenye FIKRA ZENYE UTAMADUNI WA UBORA wa kuweza kulitekeleza hilo.Tanzania kama tunacho, huenda ni Bunge Letu. Naamini linafanya kazi ya Chombo hiki au linapaswa kufanya kazi ya chombo hiki.

Kwa sasa Tanzania iko kwenye mfumo wa vyama vingi, imani juu ya misingi ya taifa haiwezi kuwa tofauti baina ya chama na chama.Na kama ipo, kauli mbiu kama KILIMO KWANZA vyama vingine navyo vinapaswa kuwa vinatambua.Na ikitokea chama kingine kinachukua nchi, kinapaswa kuwa na kauli mbiu ambazo zitaendeleza na kuwa ndani ya Misingi na sio kuanza upya. Haya yote yanatuonyesha umuhimu wa kuwa na chombo cha kitaifa chenye utaifa mbele, ambao utakuwa ni dira ya kila Mtanzania.Chombo ambacho kitaundwa huru na kufanya kazi huru,bila kusikiliza,kupendelea wala kuhusishwa na upande wowote kati ya Vyama,Bunge,Serikali,Mahakama na hata Wananchi pengine. Na kwa kupitia Chombo hicho tutaweza kuijua na kuratibu Misingi hii na hata tunaweza kuchagua miongozo sahihi ya hatma ya nchi yetu. Kizazi chetu cha akina “Dady I am Going I want to use your Car” Darasa, Msanii kizazi kipya,bila kujua Imani na Misingi ya Taifa kwa kweli tumekwisha.


Lakini, Tujiulize Watanzania:
 Imani na Misingi ya Taifa letu ni Ipi?
Chombo Gani Kinaratibu na Kusimamia? Dola, Bunge, Mahakama,Vyama vya Siasa,…..au Ni Kipi?

0 comments:

Post a Comment