Sunday, August 25, 2013

JE BAGAMOYO STARS ITATUVUSHA HAPA?

Swali kubwa kwa wanabagamoyo, ni nini kifanyike ili waweze kucheka ZAIDI ya walivyocheka siku za Timu za zamani kama Mwenge, Chai na Kurugenzi, ama zaidi TUKUYU STARS maarufu kama
Banyambala walioweza kupanda daraja na kutwaa ubingwa wakiwa na wachezaji na Kocha mzawa wa Tanzania. Tanki lina hili la kuchangia.


Mi  si wa enzi za mwenge, Ila namjua Mwenge.
Alipenda atupange, Kwa pamoja tujijenge.
Mbiu yetu tuitunge, Tuijue  tuichunge.
Tukuyu na tujipange, Turudi enzi za mwenge.





MHESHIMIWA DIWANI, BASHIRU MADODI (BASAHAMA-KUSHOTO KABISA) AKIWA NA KIKOSI KAMILI CHA BAGAMOYO STARS. (MAJINA MENGINE BADO YANASHUGHULIKIWA)

Umoja si tuujenge, Lengo kuu lake Mwenge.
Kurudi enzi za mwenge, Kwa hitaji tujipange.
Chai  pia kama Mwenge, Kurugenzi  kama Mwenge.
Tukuyu na tujipange, Turudi enzi za mwenge.

Aje diwani tupange,Waje  wabunge turinge.
Ni nini hasa tupange? Na Tukuyu tuijenge.
Wazo  bora tulitunge, Tukuyu yetu tujenge.
Tukuyu na tujipange, Turudi enzi za mwenge.

WALIOSIMAMA: Kelvin Haule,Yusuf Kamba,Karabi Mrisho,Ali Kimwaga,Danford Ngessi,Mbwana Makata,Athumani Juma(Coach). Lamliki Patel(Kaka).  

WALIOKAA: Kipa?,Richald Lumumba,Justin Mtekele,Selemani Methew,John Alex,Danny Chundu,Aston Padon. (MAJINA YAMETAJWA NA Imani Rajabu Mpangule)
Wazo langu mlipinge, Mkiliona si tenge.
Moja Uchumi tujenge, Tuubebe kama Mwenge.
Tupende kwetu tujenge, Tupeleke na vitenge.
Tukuyu na tujipange, Turudi enzi za mwenge.

Wageni pia wajenge, Tuwafanye wasipange.
Chai yetu tuichunge, Timu yetu iijenge.
Pili  shule tuipange, Michezo yetu ichunge.
Tukuyu na tujipange, Turudi enzi za mwenge.

Iwe moja kama mwenge, Tuipende tuijenge.
Akili yangu ya kenge, Najihisi siko tenge.
Na jihisi nikapenge, Niwaache  muyapange.
Tukuyu na tujipange, Turudi enzi za mwenge.

Madiwani na wabunge, Mawazo ,wapi? Tujenge.
Tuanzie kwake Page, Tusimuache Kapange.
Walio kwa Kaijage, Mje wote tuyapange.
Tukuyu na tujipange, Turudi enzi za mwenge.

Na mlio kwa  Kitenge, Hima njooni  tujenge.
Msaidie tupange, Nyumbani  tusikutenge.
Na Vijana tujipange, Wazee wawashe mwenge.
Tukuyu na tujipange, Turudi enzi za mwenge.

Na Udini tuupinge, Ukabila tuutenge.
Mbeleni sana tusonge, Kwa mwanga wa wetu mwenge.
Wa vijembe tuwatwange, Hata awe Mwakitwange.
Tukuyu na tujipange, Turudi enzi za mwenge.

Ania  tusimpinge, Kwa pamoja tumkinge.
Cha mno sisi tuchunge, La asiwe na Ukenge.
Wote mikanda tufunge , Pamoja nyumba tujenge.
Tukuyu na tujipange, Turudi enzi za mwenge.

Muhimu vyetu vihenge, Kaka kuuwasha mwenge.
Timu mpya muipange, Mawazo yake mchunge.
Aseme  vipi tupange, Turudi enzi za Mwenge.
Tukuyu na tujipange, Turudi enzi za mwenge.


BILA KUJIPANGA, VICHEKO HIVI NI SIKU MBILI TU

Related Posts:

  •  MPAJU WEEK 2020“JAMII YETU-KIOO CHETU” Kauli mbiu ya Mpaju Week 2020 ni JAMII YETU NDIO KIOO CHETU. Mpaju SC inaamini changamoto zinazoizunguka jamii yetu zinatokana na kushindwa KWETU kuzitatua. Mpaju SC inaikifikishi… Read More
  •  MPAJU WEEK 2020(Disemba 15-22)Uwanja wa Magereza Chuo-Ruanda Mbeyanani kufungua Dimba timu za wasichana?MPAJU FCVS SUPER EAGLES Mpaju FCSUPER EAGLE… Read More
  • Mpaju Week 2020-YAWA CHACHU KWA SOKA LA WANAWAKE MBEYAMpaju Week 2020 yaleta matumaini ya SOKA LA WANAWAKE MBEYA: Tamasha hili lenye KAULI MBIU YA JAMII YETU NDIO KIOO CHETU, lilifikia tamati siku ya Jumanne tarehe 22 Disemba 2020 pale Uwanja wa Chuo cha Magereza Mbeya, kuwakari… Read More
  • Udhibiti wa Idadi ya Wachezaji wa Kigeni Ligi Kuu Tanzania Bara Maamuzi ni vema Yakazingatia vizuri WAKATI WETU. Kama nimeelewa hoja, ni kuwa kwa kuwapunguza wachezaji wa kigeni walau kwa asilimia walau 50, kuna uwezekano tukaongeza nafasi ya wachezaji wa nyumbani kupata nafasi katika ti… Read More
  • Ziara ya Mpaju SC Shule ya Msingi Mpolo 2020 haitasahaulikaKwa mara nyingine, Siku ya Jumamosi tarehe 29 Agosti 2020, Mpaju SC walitembelea shule ya Msingi Mpolo iliyopo Mbalali na kufanya michezo kadhaa ya kirafiki. Hii shule yenye hazina kubwa sana ya Michezo ya nchi hii. Mpaju ime… Read More

0 comments:

Post a Comment