1
Tumlaani shetani, Ubinafsi Shetani.
Hana mpango shambani, Maisha
yake angani.
Akishuka aridhini, Atashinda tu
majini
Maumivu kijijini,Mijini yahusu
nini.
Swali
la kutoka lini, Tajiri ajibu nini.
Tajiri afanye nini, Kitufae
masikini.
Mnyonge tumnyongeni,La Hakiye tumpeni
2
Mkulima
masikini, Uchumi wako ni nini?
Kushinda kwako shambani, Faida
yake ni nini?
Jasho lako la shambani, Hasa
laliwa na nani?
Maisha kwako ni nini, Useme u
kivulini?
Unajipinda shambani, Wanakupunja
sokoni.
Kilimo kwanza ni nini, Maumivu
kilimoni?
Mnyonge tumnyongeni,La Hakiye tumpeni
3
Jadala
kuu bungeni, Si kilimo ni madini.
Pembejeo
si shambani, Zinaliwa tu mijini.
Ujanja
sasa nchini,Siasani si shambani.
Mababu wawe shambani, Vijana jaa
mijini.
Somo kilimo shuleni, Wanafunzi
huwaoni.
Misaada kilimoni,Yaishia
tafitini.
Mnyonge tumnyongeni,La Hakiye tumpeni
4
Wakulima vijijini, Hebu jamani
semeni.
Mafao yao shambani, Mipango
yafanya mboni.
Kodi zote ni shambani, Hadi simu
mikononi.
Kuenda uraisini,Kura upate
shambani.
Chakula kote nchini, Kinatoka
Vijijini.
Wengi wetu wa mijini, Hasa kwetu
vijijini.
Mnyonge tumnyongeni,La Hakiye tumpeni
5
Shambani ni vijijini, Mijini pia
shambani
Ni wapi leo mjini, Hapakuwa
kijijini?
Ufukara mashambani, Umasikini
mijini
Waziri awe shambani, Ubunge si
luningani.
Reli kufika shambani, Nchi iko
duniani.
Waziri daladalani, Mboni yetu ya
mijini.
Mnyonge tumnyongeni,La Hakiye tumpeni
6
Kilimo kikumbukeni, Mnyonge
msitirini.
Jasho
lao masikini, Wabungeni lioneni.
Wasomi
wetu vyuoni, Mkulima mjueni.
Wataalamu
nchini, Faida yenu ni nini?
Sayansi
yetu jamani, Itufaacho ni nini?
Tuache
ulimbukeni, Tujali kwetu nyumbani.
Mnyonge tumnyongeni,La Hakiye tumpeni
7
Elimu ziko mijini, Shambani
abaki nani.
Shamba si usanii, Mkulima ale
nini?
Wajanja si vijijini, Nakana huo
Utani.
Wajinga wengi mijini, Tukibisha
tubisheni.
Loliondo kumbukeni, Babu naye wa
mjini?
Tamaduni tuthamini, Taaluma zi shambani.
Mnyonge tumnyongeni,La Hakiye tumpeni
0 comments:
Post a Comment