1
ZENOPHOBIA JAMANI, UGONJWA AMA USAHA?
AFRIKA YA KUSINI, MISIBA NA MAJERAHA.
WEUSI WAWE TABUNI, WEUPE WALA MARAHA.
NAKITAFUTA KIINI, NITIBU LAO JERAHA.
SINA SHAKA
NA VICHWANI, JAPO WANA MAJERAHA.
NA MBONA
HAWAFANANI, NA TULOWAPA SILAHA?
ZENOPHOBIA JAMANI, NI GONJWA AMA USAHA?
2
NI GONJWA
KALETA NANI, WATABIBU NA SEMENI
WALE WAO
MAFANANI,TULIWAFICHA VYUMBANI.
UJINGA
AWAPE NANI, HATUNAO MAJUMBANI.
HAIPO YETU
ZAMANI, YENYE UJINGA USONI.
WEUPE WAWE
NI MBONI, WEUSI KUNI JIKONI?
MALENGA
NIKUMBUSHENI, HUU UJINGA MAKINI.
ZENOPHOBIA JAMANI, NI GONJWA AMA USAHA?
3
USAHA AINA
GANI, LAZIMA UKAMULIWE
KAMA JIPU
LA ZAMANI, SASA NA LIKAMULIWE
MUHIMU NI
UMAKINI, TIBABU LIFANIKIWE.
CHANZO
CHAKE SI PEMBENI, FUMBOLE LIFUMBULIWE.
YA MOYO
TUYATENGENI,AKILI ZIFUNGULIWE.
WEUSI TU KULIKONI,
SWALI KUU LIJIBIWE
ZENOPHOBIA JAMANI, NI GONJWA AMA USAHA?
4
KILA
KUKICHA MISIBA,KUKICHA JIPYA LIJAMBO.
AFRIKA HANA
BABA,NA MWANA KAWA MTAMBO.
WASO RANGI
WANAIBA,WENYE RANGI NDIO CHAMBO.
KAMZIDI
BARNABA, ABEBA HATA UTUMBO.
HALI
CHAKULA NA BABA, MWANA HASHIBI MAKOMBO.
UTAMBULISHO
NI BABA, WA MWANA JELA YA NGĂMBO.
ZENOPHOBIA JAMANI, NI GONJWA AMA USAHA?
0 comments:
Post a Comment