1
NATANGAZA
YANGU NIA, YA KWANGU KUWAFANYIA
FUNUNU
NIMESIKIA, URAISI UNAWADIA.
SITAKI
KUNIZUWIA,NI HAKI KWA MWENYE NIA.
MUHIMU
NAULIZIA, KURA MTANIPATIA?
IKULU
NAKIMBILIA, VINONO VILOBAKIA.
KWA RAHA
NENDE JILIA, PASIPO MUULIZIA.
NATANGAZA KWENU NIA, URAISI NAUTAKA.
2
USIDHANI
NI UTANI, UKANINYIMA SUKANI.
MWENZIO
NIKO VITANI, KUKUONDOA GIZANI.
NATAKA
UWE MAKINI, TONGO LITOKE MACHONI.
KUTOKA
UFUKARANI, ONGOZO SIRINI NINI?
WAMKANA SELEMANI, SHIKA HATA UBUDHANI.
MENGI
YANAYO THAMANI, YAMO PIA ANDIKONI.
NATANGAZA YANGU NIA,URAISI KUUSHIKA.
3
MOJA NI CHAKULA BORA, HAKI HADI TORABORA.
SIHITAJI
MAKOMBORA, TELE LIPO DONGO BORA.
TUNAZO
FIKIRA BORA, LAZIMA NI MANYAPARA.
NIMEANDAA
BAKORA, WATOLETA USAKARA.
HAITAKUWA
MIKWARA, TUTASHINDIA MAPERA.
SOTE
TUTASHINDA BARA, PWANI ZIBAKI BENDERA.
NATANGAZA YANGU NIA, URAISI KUUSHIKA.
4
AFYA BORA MUHIMU, HATA WAVUTAO
NDUMU.
HAKUNA
KITU KIGUMU, MUUMBA TUMLAUMU.
AKILI ZETU TIMAMU, DAWA ZIPO HATA NDIMU.
TUNAO WATAALAMU, TABIBU TUTAHESHIMU.
KALUMANZIRA MUHIMU, KWAKE BABU TUTADUMU.
SHUJAA AFIE HOME, HESHIMAYE ITADUMU.
NATANGAZA YANGU NIA,URAISI KUUSHIKA.
5
ELIMU TENA BALAA, SIO ELIMU YA VYETI.
USOMI
UTAKOMAA, THAMANI VIPANDE VYETI.
LUGHA ISO NA LAGHAA, ELIMUNI KATIKATI.
UTASHI NJAA NJAA, HAPA UTASHIKA KOTI.
JAMII NI ULAMAA, AJUA ELIMU NYETI.
SAYANSINI TUTANGĂA, MUUMBA MBELE KWA DHATI.
NATANGAZA YANGU NIA, URAISI KUUSHIKA.
6
WANYONGE NA MSIHOFU, MALAZI
KITU RAHISI.
MNATAKA MAJOKOFU, MHIFADHI FIRIGISI.
UMEME WA HITILAFU, TUMESEMA SASA BASI.
NANI ALO MTUKUFU, NANI SIO IBILISI.
MI SIGUSI SAKAFU, WE ULALIE SIAFU.
HAKUNA KWA WAONGOFU, WOTE MAKAZI YA NYASI.
NATANGAZA YANGU NIA, URAISI KUUSHIKA.
7
DIRA JAMBO DOGO SANA, TUSILETE KUBISHANA.
TUTAFANYA
KAZI BWANA, WATOTO WASOME SANA.
MAMA
TUWAPENDE SANA, JAMII WALEE TENA.
DIRA ILO NA
MAANA, WAZEE WAISHI SANA.
TUACHE KULA
LAANA, NA PAKA WANONE SANA.
TUBURUDIKE
KWA SANA, TUJIPUNGUZE KUNONA.
NATANGAZA YANGU NIA, URAISI KUUSHIKA.
8
KERO KUU YA
AJIRA, NINAIJUA VIZURI.
HAITAKI
MASIKHARA, NA HAITAKI KIBURI.
SITOZIGAWA
AJIRA, HATA MSEME JEURI.
IPO DAWA
BARABARA, WALA SIO YA TUNGURI.
MIUNDO
MBINU IMARA, MISINGI YA WAAJIRI.
ISIISHIE
MTWARA, WAIPATE IKWIRIRI.
NATANGAZA YANGU NIA, URAISI KUUSHIKA.
9
AJIRA KWANGU NI HAKI, JAPO MAMA HATAMKI.
UCHOYO NA UNAFIKI, KUTWA NYUMA TUTABAKI.
UCHUMI WENU SITAKI, MATUMIZI SI RAFIKI.
UFUKARANI KUBAKI, UCHOYO NDIO KISIKI.
UKINUNUA MSWAKI, MWAKA KUTUPA HUTAKI.
UKARABATI
WA LAKI, AJIRA ZIWE MALAKI?
NATANGAZA YANGU NIA, URAISI KUUSHIKA.
10
MIUNDO
MBINU NI NGUZO, NI DAMU NDANI YA MWILI.
NCHINI
TUNAUOZO, MUDA SISI HATUJALI.
FOLENI
KUTWA GUMZO. SI DAR WALA MBALALI.
AKILI SANA
TUNAZO, NI KUU RASILIMALI.
NINATOA
MUONGOZO, NCHI ISAMBAE RELI.
PESA SIONI
KIKWAZO, TUKIJIZILA MIILI.
NATANGAZA YANGU NIA, URAISI KUUSHIKA.
11
TAARIFA
KUPUUZA, HATARI NIMEGUNDUA.
NCHI TUTAJA
IUZA, TUBAKIE NA MAPUA.
HAPA SAUTI
NAPAZA, HAKI YAKO ZITAKUA.
ZISISUBIRI
BARAZA, MABAYA KUYAFUKUA.
ZIYACHUJE
MAVILAZA, UJINGA UJE PUNGUA
ZIHOJI NA
KUCHUNGUZA, UMMA USIJE UNGUA.
NATANGAZA YANGU NIA, URAISI KUUSHIKA.
12
ARDHI SINA
UBISHI, KILA MTU MMILIKI.
SITOLAMBA
MATAPISHI, SHERIA SIIMILIKI.
KATIBA SI
MATAMSHI, KIVIPI HATUANDIKI.
MILELE
SIWEZI ISHI, NCHI VIPI NIMILIKI.
WENGI
HATUNA UTASHI, NI KIPI HASA NI HAKI.
SITOLETA
MAGUMASHI, HII YAKO KURA HAKI.
NATANGAZA YANGU NIA, URAISI KUUSHIKA.
13
WAJIBU
HAKIYE KAZI, KAZI NDIO WETU UTU.
KIPATO HAKI
YA KAZI, VIPI ANALIPWA MTU?
KAZI ZILIPE
WAKAZI, PESA SI KITU CHA MTU.
UZALENDO
NDIO NGAZI, KODI HAKI YAKE MTU.
NIKISHINDA
LA UWAZI, LA GIZANI SIO KITU.
MAENDELEO
NA KAZI, NI KAMA MOYO NA MTU.
NATANGAZA YANGU NIA, URAISI KUUSHIKA.
14
UFISADI NDIO NGOMA, WATOTO HAIWAHUSU.
HILI NINAYO
HEKIMA, KWA NDANI NIMEDURURSU.
TUSIJE
MTUSI MAMA, HAYUPO HATUPO NUSU.
MAFISADI
KWELI NOMA, TANDAO LAO SI NUSU.
HAKIMU
ZINGIRA SOMA, DAWA SIO MAHABUSU.
MAJIMBO
KWAO NI HOMA, FILISI NI LAO BUSU.
NATANGAZA YANGU NIA, URAISI KUUSHIKA.
15
RUSHWA
NDOGO SIO HOMA, HAITABAKI KIGOMA.
HATUITAKI
DODOMA, IMELETA TRAKOMA.
DAWAYE IPO
KWA MAMA, VITABU TUKIVISOMA.
UWAZI
MSINGI MWEMA, TUSIJE KWEPA LAWAMA.
HAKUNA JELA NASEMA, YATUACHIA ULEMA.
MIFUMO FEKI UKOMA,HABARI ZINACHUTAMA.
NATANGAZA YANGU NIA, URAISI KUUSHIKA.
16
KATIBA KWANGU NI BABA, AMPENDAYE NA MAMA.
HAFANYI MCHEZO BABA, NYUMBA IENDE MRAMA.
ATULINDE
SANA BABA, HAPENDI BURE KUHEMA.
UTAMBULISHO
NI BABA, MSINGI BORA UMAMA.
UBORA WAKE
KATIBA, KUTHAMINI TAALUMA.
WAJIBU NA
HAKI TIBA, UBINAFSI UNYAMA.
NATANGAZA YANGU NIA, URAISI KUUSHIKA.
17
MATEJA NYIE
WANANGU, VIPI NIJE WASAHAU.
PENGINE APENDE MUNGU, PIPI ZIWE KAUKAU.
TAIFA LISILO MUNGU, WANAWE LITASAHAU.
MWANA AKILAMBA CHUNGU,CHACHU KATU HASAHAU.
SHIKENI HILI LA KWANGU, MADAWA MTASAHAU.
SITAKI MIA MIZUNGU, NITAWAFANYA WADAU.
NATANGAZA YANGU NIA, URAISI KUUSHIKA.
18
WALE DADA ZANGU POA, UKOMBOZI SIJALETA.
NAANZA NA KAKAPOA, NYIE HASA NDO WATATA.
HAKI YAO
NITATOA, YA KIFO YAO WATATA.
HILO GONJWA
SIO POA, JAMII IKILIPATA.
KARANTINI
NITATOA, MATIBABU WATAPATA.
NAJUA
WANATUBOA, HEKIMAYE PIA TATA.
NATANGAZA YANGU NIA, URAISI KUUSHIKA.
19
NATANGAZA
YANGU NIA, KILIMO KUKIKOMBOA.
MKULIMA
YANGU NIA, LANGU TAMKO NATOA
DIRA BORA
TANZANIA, MKULIMA KUMTOA.
ELIMU BORA NI NJIA,MKULIMA KUTOBOA.
MAKAZI YALOTULIA,TUSIPATE KUKOHOA.
DAWA TEKNOLOJIA, SIYO YA KUJIPODOA
NATANGAZA YANGU NIA, URAISI KUUSHIKA.
20
KATIBA NINARUDIA,UMUHIMU NAUJUA.
IKULU NIKIINGIA, CHA KWANZA NIMECHAGUA
KATIBA YA
TANZANIA, WAANDIKE WANOJUA.
MTAWALA
NILO MIA, HAKIKA MTANIJUA.
SIACHI
KUSIMAMIA, MKULIMA ASOJUA.
KATIBA
NITATUMIA, MTUMWA ALOAMUA.
NATANGAZA YANGU NIA, URAISI KUUSHIKA.
0 comments:
Post a Comment