Monday, September 14, 2015

Kölner Zoo-Hifadhi Ndogo ya Wanyama ya Kölner, Koloni-Ujerumani



Siku ya tarehe 12 September 2015, nilibahatika kutembelea Kölner Zoo! Hapa ni mahali ambapo Wanyama mbalimbali wa porini wamehifadhiwa pale Koloni-Ujerumani, ili watu waweze
kutembelea na kuwafahamu na kujifunza ama kuburudika kutokana na wanyama hao. Kuna wanyama wengi kwa kweli. Tiketi, ilikuwa ghali kidogo, hasa kabla hujajua ni kiasi unaweza kujifunza utakapofika humo ndani.Wahenga walisema "Kama Elimu ni ghali, basi jaribu Ujinga". Namshukuru sana rafiki yetu, Christian na Anita waliofanikisha utalii huu mdogo. Kiingilio, ni wastani wa shiling za kitanzania 40,000/=  (Euro 17.5) hivi kwa mtu mmoja mzima.
Ramani ya Kölner Zoo, ambayo nilipatiwa mara tu baada ya kukata tiketi
Lakini moja ya vitu vilivyonivutia ni kuona jinsi gani wenzetu wanaweza kutumia kitu kama hiki kufikisha naadhi ya vitu vya kisayansi. Kuna maonyesho kadhaa kama ya ndege mbalimbali wanavyoweza kuwasiliana na wataalamu husika.Zaidi ya hayo,pia kulikuwa na vitu kama vile kuzungusha sarafu kwenye kitu na kusubiria mpaka kitumbukie shimo dogo lililo katikati. Hii ilikuwa kwa ajili ya kutoa mfano wa BLACK HOLE- SHIMO JEUSI. Hii ni sehemu ambayo kwa lugha ya mtaani, ni mahali popote ambapo pesa inapotelea pasipo uwezekano wa kuipata tena. Wazo hili ni la kisayansi, likiwa linamaanisha ni eneo la kianga (space) ama kisayari ambapo kuna mvuto (graviti) kiasi kwamba kitu kinachoingia hakiwezi kutoka tena. Hii inaonyesha jinsi gani, sayansi inavyopelekwa kwenye maisha ya kila siku ili iweze kupokelewa na kueleweka na jamii!

Kama haitoshi, kuna sehemu ya kujaribu kupampu maji kwenye bomba ambalo limeunganishwa na picha ya Twiga.Lengo la hili zeozi ni kutka kujionea ni jinsi gani, moyo wa mnyama huyu Twiga unanguvu ya kuweza kusukuma dama kulingana na kiasi chake cha urefu! Haya yote ni mambo ambayo mbali na kuona wanyama, pia ni mafundisho kwa jamii inayokuwa imetembelea eneo hili.

Nadhani kwa nchi kama Tanzania, hii inaweza kufanyika pia.Kwa sababu ni zaidi ya watu kuburudika,kufurahia ama kutalii, bali ni sehemu ya elimu,tafiti na hata hifadhi ya aina ya wanyama wanaopatikana nchini, kwa urahisi bila kuwafanya wananchi wafunge safari kuelekea mbugani ama wasubiri maonyesho ya sabasaba na nanenane, ambayo mara nyingi huwa hayawezi kufikia kiasi hiki cha maandalizi.
Heroe (Flamingo) ni kati ya vivutio vinavyopatinakana Kölner Zoo.
  ANGALIZO: Hebu angalia Picha ya Ramani ya Koelner Zoo, kisha jaribu kumfikiria Mbunifu wa Eneo hilo inawezekana alikuwa DHANA gani kichwani? Hilo nalo lilinipa fundisho fulani kwenye hii Hifadhi.

0 comments:

Post a Comment