Friday, October 30, 2015

HAPA KAZI TU



NI "MSEMO" WENYE MANUFAA KWETU VIJANA.
Tusiutupe na Tuutendee Haki.
 Ni kauli ya Raisi Mteule wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Dr John Pombe Magufuli (Kuanzia tarehe 29 Oktoba 2015). Hongera sana mheshimiwa kwa kuchaguliwa. Kama ilivyo ada, kila mtanzania ana lake la kusema, kutokana na mchakato mzima wa uchaguzi,matarajio na matokeo. Tanki halina hoja juu ya mambo yahusuyo sharia za uchaguzi na siasa zake. Lakini kwenye suala zima la KAULI MBIU YA HAPA KAZI TU, Tanki lina machache ya kuongelea kama sehemu ya kuunga mkono kauli hiyo.Hii haina maana kuwa
kuwa kauli mbiu zingine sio sahihi, bali haya maoni ni kuunga mkono tu kuwa kaui mbiu hii ikitumika na mtu yeyote, inaweza kufaa.


Watanzania wengi wanaamini kumkomboa mkulima wa jembe la mkono ni kukomboa Taifa. Kimsingi,imani hii inaashiria kuwa Mtanzania hutegemea sana NGUVU YAKE ili kuweza kujikwamua na maisha yake. Pia, siku hizi kuna misemo inayotumika na watanzania pengine kila siku iendayo kwa MUNGU. Mfano, “NIKO BUSY”, wakimaanisha “NIMEBANWA NA KAZI au SHUGHULI,HIVYO hivyo SINA MUDA wa kutosha” au kwa wale wafanyao kazi za kuajiriwa, utasikia maneno kama “MUDA WA KUFANYA MAMBO YANGU”, wakimaanisha “KUWA NA ZIADA YA MUDA WA KUSHUGHULIKA NA KAZI ZAIDI au BINAFSI ZA KUJIONGEZEA KIPATO” .Hii yote inazunguka katika sentensi moja ya Mheshimiwa Magufuli, HAPA KAZI TU. Yaani sasa hayo yote yawe YANA MAANISHWA KIMATENDO na kwa MANUFAA YA JAMII NA TAIFA.

KAZI katika mtazamo wa kifizikia ni zao la NGUVU ikizidishwa na MUDA uliotumika. Kauli mbiu ya mheshimiwa Magufuli, ni ya KISAYANSI HASA na ina uhusiano na “mtanzania wa kawaida” kwa sababu mtanzania yeyote anaujua msemo wa MTAJI WA MASIKINI ni NGUVU ZAKE MWENYEWE.Msemo unaashiria kutambua kuwa mtanzania anahitaji kusaidiwa na kuongozwa katika KUFANYA KAZI kwanza kuliko kitu kingine, maana NGUVU ANAZO KAMA MTAJI WA MSINGI. MUDA hakuna anaeumilika ISIPOKUWA MUNGU mwenyewe.

Zaidi ya hilo, kauli hii ya Mheshimiwa, inaonyesha kuwa na undani juu ya kile ambacho WATANZANIA WENGI pengine hatukitendei haki kuliko vyote. Yaani, KUTO UTUMIA VIZURI MUDA NA NGUVU/JITIHADA zetu. Ni wepesi kutamka maneno MUDA na JUHUDI kuliko kuonyesha kwa MATENDO KUWA TUNAJUA NA TUNAJALI HAYA MANENO. Ni kawaida kwa Mtanzania, kumwambia mwenzie, “NINA PESA kidogo hapa, hebu twende tukapoteze MUDA KIDOGO pale”. Au Kumwambia “UNAJITUMA UTADHANI KAZI YA BABA YAKO HIYO”, kisa ni kazi ya serikali.Kadri siku zinavyozidi, tunashuhudia KIZAZI ambacho kinajua KULALAMIKA, kuliko KUFANYA KAZI VIZURI, na mbaya Zaidi kizazi hiki si cha elimu ya chini wala ya juu. Vijana wanazidi kuwa MABINGWA wa KUCHAGUA KAZI NA KUKIMBIA MATATIZO YA FAMILIA ZAO, mpaka WAZAZI NA WAZEE NDIO WANALEA WAJUKUU NA VITUKUU. Kwa nini Matatizo yasiziandame familia zetu za KITANZANIA? Mheshimiwa anasema HAPA KAZI TU SASA. Kama KWELI kauli hii inalenga KUMKOMBOA MTANZANIA, maana yake inalenga kumfanya MTANZANIA, ASICHAGUE WALA ASITAFUTE KAZI tena, bali KAZI IMCHAGUE na KUMTAFUTA YEYE. Mtanzania, ASIKIMBIE TENA MATATIZO NA SHIDA ZA FAMILIA, bali ATAFUTE SHIDA NA MATATIZO YA FAMILIA YAKE mpaka MATATIZO NA SHIDA ZA FAMILIA YAKE vimuogope na kumkimbia YEYE. Mtanzania, awe hasemi tena “NIKO BUSY”, bali awe anauliza “UNA MUDA, TUKAPOTEZE PESA KIDOGO NDUGU YANGU?” Ndiyoooooooo!

HAPA KAZI TU, japo kibongo-bongo, Porojo Muhimu. Kama Mtanzania mwenzangu; utapata nafasi ya Kusoma hizi porojo, basi mungu akusaidie uielewe kuwa TANKI hili linachomaanisha ni kuwa, hii kauli mbiu imebeba mambo mengi sana,PENGINE KAMA KAULI ZINGINE TULIZOZISIKIA. Kuanzia aina ya ufikiriaji wa raisi mpaka mwanga wa wapi angependa TAIFA LETU lielekee kwa sasa. Tanki linaamini kauli ina Fikra Zenye Utamadumi wa Ubora ndani yaki,zinazopaswa kuleta chachu ya MABADILIKO YA MTU BINAFSI NA HATA TAIFA ikitendewa HAKI. Si vema ukaitupa kwenye maisha yako BINAFSI.  Hata Baniani MBAYA kiatu chake kinaweza kuwa DAWA kwako pia.

KAZI NI UTU, KAZI INA MUDA NA NGUVU NDANI YAKE. Mwenye NGUVU muache apite, UMOJA ni NGUVU,MUDA ni MALI, ASIYEFANYA KAZI ASILE,,, na misemo  kibao ya WAHENGA yazunguka kwenye neno KAZI,,,,,,,,! Hii ni KAULI SAHIHI kwa watanzania kwa sasa! Ni hatua katika kufikia tunako taka, kama katiba (rejea kiungo: http://mpaju.blogspot.de/2013/06/maoni-juu-ya-rasimu-ya-katiba-mpya-1.html)
HAPA KAZI TU, MTU WAAAAAAAANGU!





2 comments: