Wakati wa Kufunga Sherehe |
Nembo Kuu ya MSC |
Mpaju Sports Centre (MSC) ni Taasisi ya Michezo inayopatikana Mbeya-Iganzo, Tanzania. Taasisi hii inaamini katika Nguvu ya Vipawa na Uasilia. MSC imeanzishwa katika misingi ya kuheshimu vipawa na uasili
alionao mwanadamu na mazingira yanayomzunguka popote duniani. MSC inaamini
kwa
kuthamini,kujali na kuutumia kwa ufanisi uwezo wa asili wa mwanadamu na
mazingira yake, Tanzania na ulimwengu kwa ujumla, vinaweza kufanywa sehemu bora
ya kuishi leo na hata kesho. Dira ya
MSC ni kuwa Taasisi Bora ya Michezo Ulimwenguni.
Lengo la MSC ni kuvumbua na kuendeleza vipawa vya michezo mbalimbali Tanzania na
ulimwenguni kote. Maandalizi ya Jogging |
Katika jitihada za kufanikisha dira na malengo ya MSC,
Uongozi wa taasisi, ukiongozwa na Juma Ahmed Mpangule na Abdallah Athumani
Kiumbo umefanikiwa kukamilisha usajili wa Klabu ya Mpira wa Miguu inayotambulika
kama Mpaju Footbal Club. Usajili
wake ni namba 12029, wa siku ya
tarehe 05 Machi 2018. Kupitia Mpaju
FC, taasisi inatarajia Kushiriki kwa
mafanikio mashindano yote halali ya mpira wa miguu, hasa yanayohusisha vijana
na watoto chini ya umri wa miaka 23. Pia Taasisi inaamini itaweza Kuburudisha mashabiki wote wa mpira
miguu duniani na kutoa mchango katika kuboresha
shughuli za kifedha zinahusiana na mpira wa miguu Tanzania na duniani kwa
ujumla.
Mwalimu Abdallah Athumani Jogging |
Tokea juhudi hizi za MSC zianze mnamo mwezi wa Februari
mwaka 2017, maneneo ya IGANZO-MBEYA, kufuatia mwanzilishi ( Raisi wa Taasisi)
kuihamishia ndoto yake ya kumsaidia mwanae Ahmed Juma Mpangule kujiendeleza
katika mpira wa miguu kuwa ndoto ya jamii yote na dunia kwa ujumla, Mpaju FC
imefikisha mwaka mmoja na miezi miwili. Hata hivyo katika kuazimisha sherehe za
kufikisha mwaka mmoja, tokea juhudi halisi za taasisi kuanza, taasisi ilifanya
sherehe ndogo na kuiita MPAJU SPORTS
CENTRE DAY. Shughuli na mambo yaliyofanyika na kufana kama yalivyoelezewa
kupitia katika majedwali hapa chini.
Mwalimu Mpaju Akiongoza Jogging |
Mpango ulikuwa kukimbia kidogo, kufanya usafi na kuzishindanisha timu za Mpaju FC kwa makundi yake, yaani kuanzia Kundi A- ambao ni zaidi ya Miaka 18 mpaka Kundi F ambao ni chini ya Miaka 7. Lakini kutokana na sababu zisizozuilika kama vile baadhi ya wachezaji kutopata ruhusa makwao kutokana na ugeni wa tukio zima masikioni mwa wazazi, ilibidi makundi ya kushindana yaundwe upya na hivyo kupata timu 3, timu ya Dulayo, Mpaju na Mastaa wa Mpaju, yaani wachezaji wa Grupu B la Mpaju FC.
Timu za Mechi ya Ufunguzi-(Mpaju FC D,E &F) |
Kwa kifupi, sherehe zilifana, kama ambavyo picha
zinadhihirisha. Pia zawadi mbalimbali zilitolewa ikiwa ni pamoja na Mwana Mpaju
FC wa Mwaka kupatiwa nafasi ya kunyoa nywele katika saloon ya Mpaju kwa mwaka
mzima. Mechi ya Ufunguzi ilihusisha watoto wenye umri chini ya miaka 9 ambao ni grupu la Mpaju FC D na E, japo pia kwa sababu za kimafunzo walimu na baadhi ya wachezaji wakubwa waliruhusiwa kucheza. Kundi hili lilitoa mchezaji bora kwa nafasi ya uzuiaji, Castrol.
Timu ya Dulayo wa kiwa na Twaha Madodi-Mabingwa |
Mpaju Sports Centre Day, ilishuhudia Uwezo wa Juu wa kusakata soka, kutoka kwa mdau na mzazi wa wachezaji wawili, yaani Nasfari na Ridhwani, ndugu Twaha Salumu Madodi. Pamoja na Mwili wake kuwa wenye umbo kubwa kuliko watu wote uwanjani, bado uwezo wa kumiliki mpira,na kuupeleka sehemu sahihi ulikuwa burudani kwa kila aliyefika uwanjani hapo, na kwa kiasi kikubwa yeye ndiye aliyekuwa mhimili wa tima ya dulayo kutwaa ubingwa wa Bonanza hili. Alimiliki vizuri eneo la kiungo na kuwafnya viungo wa tima ya Mastaa wa Mpaju kama Asajile na wa Timu ya Mpaju mwalimu Mpaju kushindwa kufurukuta kabisa.
MPANGO WA RATIBA YA MPAJU SPORTS CENTRE DAY-31
DISEMBA 2017
|
|||||
S/N
|
TUKIO
|
MUDA
|
WAHUSIKA
|
ENEO
|
DHUMUNI
|
1
|
JOGGING (MAKIMBIZI vYA TARATIBU)
|
0800-0900
|
WACHEZAJI
|
|
KULETA HAMASA YA MICHEZO KWA
JAMII
|
|
|
|
VIONGOZI
|
MTAA WA IGANZO
|
|
|
|
|
WAGENI
|
|
|
2
|
USAFI
|
0930-1030
|
WACHEZAJI
|
MTAA WA IGANZO
|
KULETA HAMASA YA USAFI WA MAZINGIRA KWA JAMII
|
|
|
|
VIONGOZI
|
|
|
|
|
|
WAGENI
|
|
|
3
|
MASHINDANO YA MPIRA WA MIGUU
|
1045-1645
|
MPAJU SPORTS
|
UWANJA WA SHULE YA SEKONDARI YA IGANZO
|
KUJIBURUDISHA NA KUSHINDANIA ZAWADI MBALIMBALI
|
|
|
|
TIMU A
|
|
|
|
|
|
TIMU B
|
|
|
|
|
|
TIMU C
|
|
|
|
|
|
TIMU D
|
|
|
|
|
|
TIMU E
|
|
|
|
|
|
TIMU F
|
|
|
4
|
UTOAJI WA ZAWADI
|
1700-1800
|
VIONGOZI NA WACHEZAJI MPAJU SPORTS
|
UWANJA WA SEKONDARI WA IGANZO
|
KUWAPONGEZA WACHEZAJI KWA UJUMLA
|
|
|
|
|
|
|
Mastaa wa Mpaju FC |
Kulia ni Mchezaji LANGO wakiwa mbele na mwalimu kumalizia Jogging |
Nembo Iliyosajiliwa ya Mpaju FC |
Mpaju FC Picha Ya Pamoja Siku ya Mpaju Sports Centre (MSC) |
MUNGU IBARIKI TANZANIA, MUNGU IBARIKI MPAJU SPORTS CENTRE
0 comments:
Post a Comment