NANI ANAIHITAJI ZAIDI?
Mjadala wa Building Information
Modeling ni miongoni mwa mijadala mikubwa kwa wakati huu kwenye sekta
zinazohusu Majenzi Duniani kote.
Unaweza kuona mfululizo wa makongamano ya BIM
Uingereza, ikiwemo lijalo la tarehe 21 Septemba 2017, (http://www.bimconference.co.uk/why-attend.php). Mwaka huu
2016 swala kuu lilikuwa kuongelea nadharia ya BIM, na hii ya mwaka kesho
inaendeleza kuanzia hapo kwa kuonyesha jinsi utekelezaji na utumiaji wake
katika uhalisia wa Majenzi. Ujerumani nao hawako nyuma. Wao wana juhudi
mbalimbali na makongamano kama inavyoonyeshwa kwenye kiungo hiki (https://www.bim-world.de/), ambapo
Miaka miwili mfululizo sasa kongamano kubwa la BIM linafanywa,yaani kwa mwaka
2016 na 2017. Umuhimu wa BIM kwenye kuweka wazi taswira ya kazi za majenzi,
ushirikiano baina ya wadau wa ujenzi na kuboresha utendaji wa kazi za majenzi
umejadiliwa ikiwa ni pamoja na kujadili miongozo iliyoandaliwa kwa ajili ya
kuhakikisha utekelzaji wa BIM Ujerumani unafanikiwa.
Sio kwamba Tanzania haina habari
kabisa kuhusu BIM, la hasha. Bali juhudi Zaidi zinahitajika ili kuifanya iwe
kitu cha kawaida katika utendaji wa kila siku katika majenzi. Makongamano ya
Bodi ya Wasanifu na Wakadiriaji majenzi yameshudia baadhi ya wataalamu
wakisisitza umuhimu kuipa nafasi BIM katika seta yetu ya ujenzi nchini. Mfano
ni mtaalamu kutoka nchi za kiscandinavia, ( Broberg, 2014), aliyetoa mtazamo wake katika kongamano
la Uboreshaji Endelevu wa Utaalamu Continous
Professional Development (CPD) lililofanyika mnamo tarehe 21-23 march Mbeya
Tanzania. Mtaalamu huyo, alieleza kuwa matumizi ya BIM yamewanufaisha sana wao
katika miradi yao ya ujenzi, kuanzia kupunguza gharama, ufanisi kwenye
kudhibiti muda, kuongeza ubora na kuongeza ufanisi wao kama wataalamu wa
usanifu wa ujenzi.
Kwa mara ya kwanza unapoisikia BIM,
unaweza kusema sio kitu cha kuweza kufanyika leo wala kesho kwa nchi kama
Tanzania. Inakuwa kama ni dude Fulani kubwa sana linalohitaji mabilioni ya pesa
na maandalizi ya kimasomo kwa hali ya juu. Wengi wa wataalamu wamesikika
wakisema hiyo ni ya Ulaya, huku baaado sana. Hawa ni wale ambao hata kufanya kazi vizuri, pia huwa wanasema hiyo si
kwa Tanzania, labda nchi za watu huko (Yaani Ulaya na kwingineko). Wapo pia
ambao huwa wanajiuliza kuwa “Hii BIM hasa ni nini? Inaongeza nini kwenye mfumo
wetu? Isijekuwa ni makompyuta tu.” Mimi napenda kuwa kwenye hili kundi. Lakini
pia wapo wale ambao wanasema BIM ni kwa ajili ya Architects tu. Na Zaidi wapo
ambao wanahisi BIM itaondoa umuhimu wa baadhi ya taalamu kama Quantity Surveying, ama ukadiriaji wa
ujenzi. Mara kadhaa kumezuka fununu kuwa Utaalamu wa ukadiriaji utapungua
umuhimu kwa kuwa kumeongezeka teknolojia ambayo inaonekana kuwa na uwezo wa
kupiga hesabu automatiki. Hilo limekuwa pia gumzo kwa ujio wa BIM. Lakini kuna
misemo mingi sana inaonyesha kuwa akili ya mwanadamu bado inastahili heshima
Zaidi ya teknolojia. Mmojawapo wa misemo hiyo ni “Computers
are useless. They can only give you answers” Wa ― Pablo Picasso.Lakini kama
haitoshi katika kitabu cha (Moran, 2015)
imesisitizwa kuwa
“Process plant design is an art, whose practitioners
use science and mathematics, models and simulations, drawings and spreadsheets,
but only to support their professional judgment. This judgment cannot be
supplanted by these things, since people are smarter than computers (and
probably always will be). Our imagination, mental imagery, intuition,
analogies and metaphors, ability to negotiate and communicate with others,
knowledge of custom and practice and of past disasters, personalities, and
experience are what designers bring to the table.
If more people understood the total nature of design
they would see the futility of attempts to replace skilled professional
designers with technicians who punch numbers into computers. Any problem a
computer can solve isn’t really a problem at all—the nontrivial problems of
real-world design lie elsewhere.”
Kifupi ni kuwa Utaalamu wa
mwanadamu una thamani kubwa kulinganisha na msaada wa teknolojia katika utatuzi
wa matatizo ya kitaalamu kwa sababu mwanadamu
ana nafasi ya kujiuliza,kujifunza,kufikiri na hata kuomba msaada juu ya
jambo analotaka kulitatua. Maamuzi yake yananafasi kubwa ya kuwa bora kuliko teknolojia
yeyote. Hata BIM iwe na maendeleo ya kiteknolojia kwa kiasi kikubwa sio rahisi
kuondoa umuhimu wa wakadiriaji,labda kama haukuwa Utaalamu halisi unaohitaji
utashi wa mwanadamu. Hivyo mtaalamu hata uwe na kiasi gani cha teknolojia,
tafadhali usidharau kusoma na kusikiliza kutoka kwa binadamu mwenzio. Hebu
angalia na hiki kiungo (http://www.goodreads.com/quotes/tag/technology) kwa
kuona maneno kama yafuatayo;
“Please, no matter how we advance technologically,
please don't abandon the book. There is nothing in our material world more
beautiful than the book."(Acceptance speech, National Book Award 2010 (Nonfiction),
November 17, 2010)” Patti Smith
Japokuwa natamani kuongelea wadau
wote wa majenzi, ila navutiwa Zaidi na kuanza na Architect Technologist, kwa
sababu nina uhusiano nao binafsi na hivyo ningependa kushauri kuwa pengine
wanapaswa kuipa nafasi ya kwanza BIM kwenye maisha yao ya kitaaluma. Wengine ni
Architects, ambao mimi nawaita mabosi zangu kwa sababu kama mkadiriaji wa
ujenzi nategemea kupata kazi nzuri kutoka kwao ili niweze kufurahia kazi yangu.
Na pengine inaweza kuwa ni kuwapa heshima stahili kwa sababu katika ujenzi hasa
wa majengo, Architects au Wasanifu huwa mara nyingi ni wataalamu wa mwanzo sana
kuongea na mteja ili kujua hasa anahitaji nini. Na baadae wataalamu wengine
huungana ili kukamilisha kile walichoanzisha kukishauri kuwa ndio kinamfaa
mshitiri wa mradi huo. Na ukiangalia maandiko kadhaa kama la ((McGraw-Hill, 2010) na (Monko & Roider, 2014)) yanaonyesha kuwa
pia Architects wanaonyesha kuwa katika hatua za mbele katika utumiaji wa BIM.
Hivyo sio mbaya kuwapendelea na kuanza kuwaongelea kama ambavyo itakuwa sawa
pia kuwalaumu pia pale tutakapoona Tanzania haisongi katika BIM wakati wao
walianza kuijua mapema.
Architects Technologists (ATs) na
Architects kwa Tanzania wakati fulani huniwia vigumu kuwatofautisha wakati wa utendaji mtaani. Sitazigusa sana
taalamu hizi kwa sababu ki ukweli sizijui kihivyo.
Lakini Bodi kuwa moja naamini ni uchanga tu wa nchi ama muda bado wa
kuzitenganisha,maana hata Wakadiriaji mpaka sasa wako bodi moja na Architects
ama wasanifu. Sijui manufaa kama bado yapo ama ni uoga wa kujitegemea wa
wakadiriaji (QS). Kwa hapa, ATs ni wale ambao kimsingi wanapaswa kubobea katika
KUHAKIKISHA USANIFU UNAJENGEKE KWA UBORA NA UFANISI wa kisayansi na SAHIHI kwa
mujibu wa taratibu,sharia na taaluma. Architects ama Wasanifu ni wale ambao
wanapaswa kubobea kwenye KUHAKIKISHA UBUNIFU NA SANAA SAHIHI NA ENDELEVU KWA
HITAJI LA MAJENZI VINAPATIKANA KULINGANA Mahaitaji ya MSHITIRI NA JAMII.
Ninachomaanisha, ni kuwa kwa nini
TUNA SEBULE YA NJE nyumba nyingi za USWAHILINI PWANI, ni swali analojibu Architect.
Lakini kama KISEBULE KIMEJENGWA kiasi cha kuleta kiwango sahihi cha UPEPO MWANANA, ni swali
ambalo Architect Technologist anapaswa kulijibu kwa uthabiti zaidi. Lakini pia
kuna wale ambao wanapaswa kuona usiadizi wa wote hao katika kuhakikisha
uchoraji na vifaa VYA KISEBULE uko TAYARI kama inavyotarajiwa KIUTARATIBU NA
HATA KISHERIA, hapa wao ni ARCHITECT TECHNICIANS (ATTs). ATs ni wanasayansi wa
Usanifu wakati As ni Wabunifu wa Usanifu. Wasanifu wanapaswa kuiona picha kubwa
ya kwa nini Mradi wa Majenzi katika Jamii na uendelevu wa jamii hiyo, wakati
ATs wao wanapaswa kuziona hali mbalimbali za uhalisia wa ujengekeji wa vipande
vya mradi huo wa majenzi katika taratibu na sharia za jamii na taaluma. Wakati
ATTs wao watapaswa kuiona na kuionyesha picha maalumu ya kipande cha mradi huo
wa majenzi katika taratibu zake za kitaaluma na kuiwakilisha kama
wanavyoelekezwa.
Ukiangalia maandiko mbalimbali, BIM
ni uwakilishi wa kidijitali wa taarifa za majenzi na taswira ya majenzi kuanzia
mwanzo mpaka mwisho unaowafanya wataalamu wote kuweza kufanya maamuzi sahihi.Kimsingi
bado kuna debate kubwa juu ya hasa BIM ni nini. Ila mambo makuu ni pamoja na
USHIRIKISHAJI WA WAHUSIKA WOTE WA MRADI,UWASILISHAJI WA TAARIFA NA MAELEZO YA
MAJENZI KATI YA WAHUSIKA NA MTAZAMO WA MRADI WA MAJENZI KUANZIA USANIFU MPAKA
UBOMOAJI NA PENGINE UJENZI MPYA. Haya ni kati ya mambo makuu ambayo BIM
inayafanikisha. Japo ziada ni pamoja na uwepo wa MIFUMO THABITI YA KIDIJITALI
ambayo, sio kama ilivyozoeleka. Kwenye BIM uwezo wa kiautomatiki ni mkubwa kwa
kuwa vifaa na vipande vya majenzi vimehusishwa na tabia husishi na kuvifanya
view tabia za kiakili. Mlango ukiondolewa,ukuta utarudi kuziba peng kwa sababu tayari
uhusiano kati ya ukuta na mlango ulikwisha wekwa kuwa penye mlango ukuta haupo.
Pia usanifu katika BIM unaanzia kwenye KITU CHENYE MIRABA MITATU (3D Objects).
Hivyo Mradi wa majenzi ni muunganisho wa vipande mbalimbali vyenye tabia
husianishi kama ilivyoelezwa.
BIM is an acronym for Building Information Modelling.
BIM describes the means by which everyone can understand a building through the
use of a digital model which draws on a range of data assembled
collaboratively, before during and after construction. Creating a digital
Building Information Model enables those who interact with the building to
optimize their actions, resulting in a greater whole life value for the asset.
(https://www.thenbs.com/knowledge/what-is-building-information-modelling-bim)
Kwangu mimi, BIM NI UBUNIFU,
UUNDAJI, UWAKILISHAJI na UONGOZI wa KIASI NA KIWANGO CHA MAELEZO CHA MAJENZI
KATIKA MAISHA YA MRADI. Yaani, kwa kutumia mfano wa sebule la pwani ulioelezwa
hapo juu BIM kiasi cha MAELEZO YA KISEBULE ambacho wataalamu wataweza kuunda,
kuwakilisha na kuongoza kitakachoweza kuwapatia majibu yao KWA MAISHA YOTE YA
MRADI. Kwa kutazama maana zilizotolewa
hapo juu za watalaamu BIM itawafaa wataalamu wote, yaani ATs,As na ATTs. BIM
itawasadia ATs kujaribu na kuchunguza KIASI CHA UPEPO, IDADI YA WATU WANAOWEZA
KUKAA na kadhalika KATIKA KISEBULE. BIM inatoa majibu ya majaribio mbalimbali
ya MUUNDO WA SEBULE NA KIASI CHA UPEPO kinachopatikana. Architects wao BIM
mbali na kuweza kuona kama Taswira yao iko sawa na anachofanya AT kupitia BIM,
pia wanahitaji BIM kuona muunganiko wa UPEPO, SEBULE NA JAMII husika kwa ujumla.
ATTs nadhani ndio kabisa BIM inaonekana jinsi inavyoweza kuwapatia vipimo vya
SEBULE kwa shepu zote na kwa picha kamili ikiwa ni pamoja na vipimo vya mradi
mzima. Lakini kikubwa kabisa katika BIM hapa ni kuwa wote hawa sio tu wataweza
KUONGEA NA KUELEWANA WAO; bali sasa WATAWEZA KUWAHUSISHA WATAALAMU WENGINE
KIRAHISI NA KIUFANISI MKUBWA KULIKO ZAMANI,kwa sababu KIMSINGI BIM inawafanya
WAWEZE KUONGEA LUGHA MOJA (WAHUSIKA WA MRADI WANAPATA MAWASILIANO NA UELEWA
SAHIHI WA MAELEZO YA MRADI NA KUWEZA KUCHANGIA KATIKA MAAMUZI KWA UFANISI NA
UBORA SAHIHI), huku wakitofautiana hekima na busara YA MATAMSHI TU. Nadhani
vitabu vya DINI vinalieleza hili vizuri kwa kusema wajengaji wa mnara wa babeli
hawakuendelea kwa sababu walianza kuongea lugha tofauti.
Kwa ufupi kabisa ninachojaribu
kukisema, ni kuwa TUNAHITAJI BIM kwa nafasi zetu za kitaalamu na kwa ujumla
kama TIMU moja katika mradi wa Majenzi.
Kwa maisha ya SASA usiposhirikiana inawezekana ukawa unamaanisha hutaki kubaki
katika soko. In a networked world,
collaborate or perish (Bratton & Tumin, 2012).Utandawazi
unataka ushirikiano. Tuungane kuipokea na kuitathmini BIM maana haiondoki leo
wala Kesho. Njia bora ya kupambana nayo ni kuamini IPO na ITAKUWEPO, hivyo
kuifahamu na kujiandaa nayo kutatunusuru na madhara yake kuliko kuikwepa halafu
ikatulazimu kuikubali kwa kulazimishwa na mazingira magumu wakati ukifika. Hili
sio swala la mtaani tu, bali hata vyuoni, wataalamu waanze kuandaliwa kuifanya
BIM kama sehemu ya maisha yao ya kila siku. Kama ambavyo tunashauriana
kuifundisha Katiba mashuleni, tuifundishe BIM mavyuoni pia.
Taaluma kuweza kufanya vizuri
kitaifa na kimataifa inahitaji utafiti na mazoezi. Taratibu na sera pia muhimu,
lakini kuna ni vitu vinavyoweza kufuata kulingana na matumizi ya taaluma hiyo
yanavyopanda chati. Bila kufundisha, kujadili na kutafiti hatuwezi kujua kama
BIM ni nzuri kwetu ama mbaya na kibaya Zaidi hatutaweza kufahamu kuwa tufanye
nini kunufaika ama kuikwepa. Kwa sasa BIM imeshaanza kufundishwa elimu za juu,
maana yake si muda mrefu itafundishwa elimu ngazi za chini. Ushauri wangu ni
wewe na mimi tuwe waalimu wa kwanza kwa kuijadili na kuifikiria pindi
tunapofanya shughuli zetu za ujenzi. Ikumbukwe ujenzi ni sekta muhimu kwa
taifa, hivyo inapobaki nyuma kiufanisi, maana yake taifa linasonga polepole kwa
sababu sekta zingine pia zinadorora kwa kuwa nyingi zina uhusiano Fulani na
Ujenzi.Sisemi maendeleo ni kujenga nyumba ama lah, bali nasema miundo mbinu
ikikosa ubora endelevu, basi uchumi, afya,kazi, kuishi na kadhalika vinapungua
ufanisi na hivyo kuathiri maendelo ya nchi kwa ujumla. Kwa utaratibu wetu
tunaweza kujenga majumba, mabarabara na kila kitu, ila kwa kutumia BIM tunaweza
kujenga JAMII ENDELEVU.
Architects Technologists, kama
wanapaswa kuyabadili mawazo ya Architects ili yaweze kujengeka kiufasaha,kisheria na “kisayansi”, basi BIM
kama teknolojia inawahusu sana. Lakini kama ni ujumla wa taarifa inayotakiwa
kuyabadili maelezo ya majenzi ili kutoa sio tu taswira ya wataalamu bali pia
kuiboresha ili kuendana mahitaji endelevu ya jamii, Architects, Architects
Technologists na Architects Technicians hawana
jinsi ya kuikwepa BIM. Lakini Zaidi kama BIM inamaanisha kuongeza UWEZEKANO WA
KILA MSHIRIKI WA MAJENZI KUELEWA TAARIFA ZA MAJENZI NA KUSHIRIKI KWA
UFASAHA KWENYE kutoa maamuzi juu ya MRADI, basi CLIENTS (WASHITIRI) wanapaswa
KUIKIMBILIA BIM. Kama ilivyo kwa Architects, ni hivyo pia kwa designers wengine na hivyo pia wataalamu wengine. Swali la nani anaihitaji zaidi naomba kukuachia msomaji.
0 comments:
Post a Comment