Saturday, August 17, 2013

BAGAMOYO STARS-TUKUYU (MBEYA)


Kutoka http://www.basahama.blogspot.com. Tanki, linapenda kutoa pongezi za dhati kwa wahusika wote walioweza kufanikisha suala la KUANZISHWA kwa TIMU ya MPIRA wa MIGUU-BAGAMOYO STARS. Washabiki wa soka wa kitongoji cha bagamoyo,Tukuyu na TANZANIA kwa namna au nyingine watakuwa wamefarijika sana kwa taarifa hii pia.

Lakini kuna ANGALIZO, kidogo kutoka TANKINI. Hii bendera imeandikwa WASHINGTON DC. Pengine kuna sababu za msingi, lakini, sidhani kama hii ndio BENDERA ya TIMU, neno hili litakuwa na UZITO na UHALISIA wowote wa kuwapo hapo. Na kama upo basi ni vema. Pia hili neno, STARS, na alama ya nyota yenye kuzungushiwa alama mbalimbali zittumikazo kwenye mchezo wa KARATA, nazo ni vema zikiwa na maana fulani. Pia mwisho, kwa upande wa pembeni, kunaonekana alama ya UPANGA/JAMBIA na kadhaika, sijui navyo ni viashiria vya nembo ya TIMU au la? 

Kutokana na hayo, ni vema wahusika wakatuelezea kidogo washabiki tulio mbali na BAGAMOYO, ili tujue hasa timu yetu iko katika mtazamo gani! Maana bendera ya timu inapaswa kutoa mtazamo fulani au filosofia fulani ya kikundi cha watu! Lakini, kwa ujumla PONGEZI nyingi kwa hatua. Tanki linapendekeza jina LIWE BAGAMOYO SPORTS CLUB, na malengo yasiishie kwenye SOKA tu. Mengine Tuujadili baada ya maoni yenu wadau wengine wa TIMU hii!.


NB: PICHA ZOTE ZIMEPIGWA NA BASAHAMA
Hawa ni Mashabiki wa Bagamoyo Stars wakishangilia ushindi baada ya mchezo dhidi ya Juhudi katika kombe la Ng'ombe kumalizika na timu Yao kuibuka na ushindi wa goli 2-1 (Picha zote na Bashiru Madodi, Ijumaa 16, Agosti, 2013:   www.basahama.blogspot.com), kwa habari zaidi tafadhali tembelea blogu hiyo.














     Hapa chini ni Kikosi cha timu ya Bagamoyo Stars





0 comments:

Post a Comment