Sunday, February 23, 2014

NYERERE

BABA WA TAIFA WA KUJIVUNIA
ulius Nyerere pictured on January 31, 1985 in Dar es Salam, Tanzania. PHOTO | FILE  NATION MEDIA GROUP
"Nadhani hakupaswa Kung'atuka"
Nilibahatika kukutana na (BIBI Theresa) ambaye alitembelea Tanzania kwa muda wa siku mbili mnamo mwaka 1973.Kitu cha kustaajabisha, sio bibi huyu kunipatia Ramani ya Tanzania, ambayo alitumia kutembelea Tanzania ama kunionyesha kitabu cha East Afrika, hasa akinionyesha Picha ya Nyerere
(Kutokana na Mazingira fulani, nilishindwa kuchukua picha ama kicha cha habari cha kitabu), bali jambo lililokuwa la kuvutia na kunifanya niandike kipande hiki cha habari ni dhati aliyoinyesha BIBI huyu juu ya IMANI na Nyerere.
"Afrikana sind nicht bloede, die probleme ist die Abhaengigkeit ,,,,,,,,! Kama nilimuelewa vizuri alikuwa akimaanisha kuwa "Waafrika/ Watanzania sio WAJINGA, bali tatizo kubwa la waafrika ni UTEGEMEZI".
Hakuishia hapo, bali aliendela kwa kusema, TANZANIA KULIKUWA NA KIONGOZI MZURI SANA, na ALICHOFURAHI NA KUMFANYA ATAFUTE NA VITABU VYA KIONGOZI HUYU, ni kwamba alipopita NYUMBANI KWAKE NYERERE MSASANI, hakuamini kama PALE HASA NDIO NYUMBANI KWAKE. Aliyapenda sana maisha ya NYERERE, na kuona kuwa YALIKUWA YA MFANO KWA VIONGOZI WA NCHI MASIKINI.
 Achana na huyu.
Leo wengi tumeona na kusikia Historia ya South Africa siku Raisi Jakaya Mrisho Kikwete alipokuwa akisoma Hotuba ya Salamu Za RambiRambi za Watanzania kwenye Msiba wa Mandela. Ilijionyesha wazi kuwa Tanzania chini ya Nyerere ilifanya kazi kubwa sana katika ukombozi wa Afrika ya Kusini, na Keneth Kaunda alithibitisha hilo
 ( http://www.youtube.com/watch?v=afHf0k9gC7A)

wako waliojaribu kumfiikiria Mwalimu Nyerere kama nabii ama mtakatifu. Hata kama walizidi, ama la , lakini kuna ukweli kuwa inathibitisha kuwa alikuwa ni kiongozi wa kujivunia sana, na kuenzi mambo mengi alaiyo tuachia.
(http://www.youtube.com/watch?v=WJzCwO5d9Ak)

Mwisho siwezi kufika, ila naweza kukatisha makala juu ya Nyerere. Lakini kabla sijafunga ni vema nikaweka maneno ya mmoja kati ya viongozi waliopo madarakani leo, tokea wakati wa Mwalimu, yaani MUGABE, wa Zimbabwe
(http://www.nation.co.ke/news/africa/Julius-Nyerere-Robert-Mugabe-Zimbabwe-Tanzania/-/1066/2218428/-/sribju/-/index.html)

KAMA KUNA KITU, NAWEZA KUMLAUMU MWALIMU
BASI NI "KUNG'ATUKA KWAKE"

kwa sababu kuna mengi aliyokuwa akiyakataa, ndio tunayoyaona na kama yeye alikuwa akiyakataa, basi hata kama ilifika wakati lazima tuyakubali,basi yeye aliyaelewa sana, BASI alikuwa mtu sahihi KUANZA KUPAMBANA NAYO.
MUNGU WEKA ROHO YA MAREHEMU BABA WA TAIFA PEMA PEPONI



0 comments:

Post a Comment