Monday, March 3, 2014

SIMBA

UJASIRI NDIO SILAHA YETU YA KWELI

 Kujitegemea na Kuthamini MASHABIKI ndio MSINGI wa mafanikio ya KWELI ya timu YETU.
Lazima tujifunze kuanzia PALE TULIPO. Tuanze na uwezo wetu, ili tuinuke kwa pamoja, WASHABIKI
NA TIMU ZETU.Simba ni hazina kubwa kwa maendeleo ya TAIFA pia, lakini bila ya DIRA MADHUBUTI, kila siku itakuwa HADITHI ZA TULIFANYA VIZURI MIAKA KUMI ILIYOPITA.
MWANZO MGUMU, KILA MTU MWENYE NIA YA DHATI NA SIMBA ANAPASWA KUTIA SAHIHI KATIKA HISTORIA HII MPYA NA YA KUDUMU KWA SIMBA SPORTS CLUB


 Mashabiki wa Timu ya Simba wakiwa katika Eneo linaloaminika kuwa ndio lililotengwa kwa ajili ya Uwanja wa timu yao. Hii ni picha inayoonyesha mashabiki hao waliochoshwa na ubabaishaji wa viongozi, wakidhihirisha hilo kwa kuamua kuandaa uwanja wa timu ya hata kwa mikono, kuliko kuendelea kuwa timu isiyo na uwanja.

TANKI LINAUNGA MKONO JUHUDI HIZI
Vitendo ndio huongea na kueleweka kwa ufasaha kuliko malalmiko ya maneno na magazetini.

Baadhi ya VIKOSI vilivyowahi kufanya vizuri, SIMBA, ni vya mwaka 1974,1993,2003. Ukiviangalia, havina mchanganyiko mkubwa wa WACHEZAJI KUTOKA NCHI ZA NJE. Lakini, kwa sasa, SIMBA, inaonekana bila wachezaji kutoka nje haitaweza kufanya chochote. HII NI KASUMBA TU, na ni KUTUPA ASILI, kitu ambacho KIMEKUWA KIKITUDHULU SANA WAAFRIKA. 

Simba Sports Club 1993
Simba Sports Club 2003

"KUFIKA TUTAFIKA ILA CHA MOTO TUTAKIONA"

MSIMBAZI DAIMA

0 comments:

Post a Comment