Monday, March 31, 2014

"KABILA"




1
Wangu makini malenga, Wenye kujua kutunga.
Msio wenye kulinga, Wa pwani nako Mafinga.
Kuna jambo lanitinga,  Jibu lanipiga chenga
.
Sitaki kutangatanga, Kusafiri kama ninga.
Shairi dogo natunga, Nijadili na malenga.
Undugu tumeupanga, Hili letu wote janga.
Kunani Kabila hili, Ndiyo yao ni hapana?
2
Mwalimu wao ni nani, Alowafunza yaani.
Fikira yao makini, Huwezi kuibaini.
Nena yao ni laini, Hata penye uhaini.
Mimi huwa taabani, ukweli nikibaini.
Kicheko wao machoni, kilio kimo moyoni.
Uchozi tele usoni,vigelegele rohoni.
Kunani Kabila hili, Ndiyo yao ni hapana?
3
Hawajafahamiana, Lugha hazija fanana.
Hebu uchunguze sana,Wa Kenya hata wa Ghana.
Hata akikutukana, Huruma aona tena.
Asema huna maana, Anakuthamini sana.
Eti sikupendi sana, Ndiyo nakupenda sana.
Nikuja mapema sana, Hiyo usubiri sana.
Kunani Kabila hili, Ndiyo yao ni hapana?
4
Niliwakuta Mombasa, Zenji nilidhani visa.
Rufiji ndio kabisa,Wa Keko sitowagusa.
Tangu zamani si sasa,Kabila lina mikasa.
Latawala kisiasa,Kabila limetunasa.
Welevu na wenye pesa, Wajanja pia asusa.
Kabila lina darasa, Elimu asili hasa
Kunani Kabila hili, Ndiyo yao ni hapana?
5
Malenga nina waasa, Tusi zipende anasa.
Kupenda macho pepesa, Fikira bora kukosa.
Mijadala mingi hasa, Kabila hili hugusa.
Kabila lina fursa, Kwa vinono wanatesa.
Maslahi yao gusa, Ije kupata mikasa.
Msije mkanitosa,Nimehoji chao kisa.
Kunani Kabila hili, Ndiyo yao ni hapana?

„UTAENDELEA“







0 comments:

Post a Comment