Monday, December 31, 2012

ELIMU BORA NDIO NGUZO

ONDOA  BORA ELIMU  WEKA      ELIMU BORA      MAMBO YAKIMBIE

According to The Education Act of 2002(2)(1) of Tanzania, “Education means the instruction or
training of people of all ages in various fields of learning designed to contribute to the spiritual,moral,mental and physical development of the community and the attainment of the wider national goals”. 


Kwa ujumla tu kwetu sisi Watz, kwa sheria yetu wenyewe, nafikiri ya kiswahili pia ipo,ni uvivu tu wa kuitafuta! Maana ya Elimu ni maelekezo or mafunzo wanayopatiwa watu katika marika tofauti na nyanja mbalimbali yaliyosanifu kuweza kutoa mchango wa maendeleo Kiroho,Kiutu,Kifikra na Kifizikia/muonekano wa kisura katika jamii na kufanikisha kufikia malengo ya Taifa kwa mapana yake! UBORA ELIMU HUO, Kwa nini kiswahili iwe shida kwa Mtanzania? Kama hatuwezi kubadili tulichosoma kutoka lugha tuliyotumia kusoma kwenda kwenye lugha yetu, ni vipi tuweze kunufaika kama jamii na elimu hiyo tuliyoipata kupitia lugha hiyo! Ah nafikiri inawezekana!

Tayari kujigonga huku,
Utasikia huyu Yanga kaanza na Njano na Nyeusi! Mwingine huyu atakuwa Simba mbona Nyekundu na Nyeupe ndio kubwa! Hadi Ba Rizi najua atajiuliza tu kimoyomoyo!

Tukiachana na Utani huo wa jadi,
Muelekeo wa elimu yetu sio mzuri, hasa kwa upande wa ubora. Ripoti mbalimbali zinaonyesha hilo,na sio tu sisi bali na wenzetu nchi za jirani,lakini hayatuhusu sana huko!Tokea muda
mrefu suala la elimu bora limekuwa likiongelewa na wadau mbalimbali, lakini haina maana haliwezi kuongelewa leo! Na kufuatia ombi la President’s Office, Planning and Commission (POPC),kuchangia maoni juu ya suala hili, Tanki nalo limo!

Usibishe kabla hujasoma, utamaduni wetu mbaya kabisa ni kutosoma! Wanasema UKITAKA KUMFICHA KITU MTANZANIA, WEKA KWENYE MAANDISHI! Pengine ndio
chanzo cha makosa kwenye kuingia mikataba mbalimbali, na kupenda kuongea Saana kuliko kutenda. Na may be, I think, Inawezekena, Unajua,Inabidi na mungu akipenda , nyingi! kwenye kila kitu!

Soma Mdau! Acha utamaduni mbovu  wa kukimbia maandishi!
 According to the[(World Bank. (2000), Higher Education in Developing Countries: Peril and Promise. Washington D.C: The world Bank.]report, of  all levels Higher Learning Instutions provide fertile grounds for cross-pollination of representatives of all disciplines into a single place .It stressed that, developing countries can hardly benefit from the global knowledgebased economy,unless the Quantitative effort being made, get the help of qualitative effort and in relevance to local conditions.  

Mpaka sasa ni miaka zaidi ya kumi! Kama Hatuja pata suluhu ya Ubora wa Elimu,inaashiria kuchelelwa,lakini Chelewa ufike, ah hapana, msemo mzuri hapa ni Heri Nusu Shari Kuliko Shari Kamili!

Hiyo ni ripoti ya Benki ya Dunia iliyoandikwa mwaka 2000, ndio,tafiti tunafanyiwa kwa sababu zetu hata  kwanza ngumu sana, proposal ipite upewe hela, weee! Na tukifanya kwa hela zetu kimtindo, atazisoma nani kwa kupitia wapi wakati hazina sifa! Unataka kusifiwa,wakati za profesa wako hazijapita,zimewekwa kando zinasubiri budget ijayo,na ndio maana wakati mwingine zinawanufaisha watu wa mbali kabisa! 

HATA KAMA RESEARCH YAKO YA ‘KATI YA MVUA NA JUA BORA NINI?’ HAINA PROPOSAL,TUTAISOMA TUONE ULICHOTUFUNZA AU MAPUNGUFU ULIONAYO,ILI TUJUE TUKUSAIDIAJE!

 Ripoti hii YA BENKI YA DUNIA ilionesha wazi kuwa bila jitihada za dhati kupandisha UBORA WA ELIMU,HASA VYUO VIKUU,AMBAMO WANAKUTANISHWA WATU KUTOKA MAENEO MBALIMBALI NA WANAOTEGEMEWA KWENDA KUTUMIKIA TAIFA KATIKA NYANJA MBALIMBALI, BASI NCHI ZINAZOENDELEA ZISAHAU KUNUFAIKA KWA LOLOTE KATIKA DUNIA YA UTANDAWAZI.

Actually, University Education as a key representative must be excellently fit for the society,otherwise it is worthless and dangerous to the country’s development. 

Na kuongelea Vyuo vikuu, sio tu kunarahisisha uongeaji,bali ni rahisi hata kufanyia majaribio mapendekezo yatakayotolewa huku tukitaraji matokeo kuligusa haraka sana taifa! Wanafunzi wa vyuo vikuu wanatarajiwa kukamata nyadhifa au nafasi fulani sehemu mbalimbali za kiutendaji, AMA KUJIAJILI KAMA AMBAVYO HALI INAONEKNA KWA SASA, SAAFI SERIKALI YETU!, hivyo basi kweli kabisa wakikosa elimu bora ni hatari kubwa pengine kuliko hata kama wasingesoma. Maana ni bora kuwa na mtu usiyemuamini (Utakuwa makini) kuliko kuwa na unayemuamini kumbe hastahili kuaminiwa! Na kibaya zaidi ni pale inapotokea anaongeza ufanisi kuelekea kwenye kukudhuru. Yaani; Mfikirie Msomi ‘mbovu’ anapoamua kutumia elimu yake kwa ajili ya kukutapeli, si ni afadhali asingesoma?

Is The Government aware of this poor quality of education? Yes Of course.WENYEWE WANAJUA? NDIO?

Katika ripoti ya (President’s Office, Planning and Commission (POPC) (October 2012)), mtandao wa taifa, imeelezwa waziwazi kuwa hali yetu katika eneo la idadi ya rasilimali watu na hata ubora kwa ujumla si ya kuridhisha! Hivyo Serikali ina mikakati madhubuti ya kuboresha elimu ili walau tuweze kuendana na ushindani na uhitaji  wa soko la utandawazi.

Baadhi ya changamoto zilizoguswa na ripoti hii ni

  •   Wanafunzi kutojiunga na masomo ya sayansi;
  • Matumizi kidogo ya teknolojia ya mawasiliano ICT
  •  Kutojitosheleza kiubunifu, ushindani na kadhalika katika utendaji wa kila siku!


Upambani wa hayo umeonekana unaweza kuwa kupitia:

  • Vyuo maalumu na shule maalumu kwe ajili ya sayansi na technolojia
  •  Kuweka mpango madhubuti wa ushirikiano wa sekta binafsi na umma kwenye uendeshaji wa shule na vyuo hivyo maalumu
  •   Na pia kujidhatiti kwenye soko huria la pamoja la Afrika Mashariki
  • Kuongeza idadi wanafunzi kujiunga vyuoni
  • Kuboresha mazingira ya ufundishaji na kuwabakisha walimu katika kila ngazi
  • N.k


MPAKA HAPO UBISHI HAKUNA, TATIZO LIPO, NA TAIFA LINAJUA NA LINATUHITAJI TUCHANGIE MAWAZO JINSI YA KULITOKOMEZA TATIZO HILI,TUTOE MAONI SIO KESHO TUNALAUMU KUWA WADAU HATUKUSHIRIKISHWA. KAMA KWENYE KATIBA, KAZI YETU KUONGEA NA VYOMBO VYA HABARI TU! CHANGIA MAONI YAKO YA KATIBA SEHEMU HUSIKA,HASA WALE AMBAO KWA MUDA WAO MWINGI WAKO NJE YA NCHI,LAKINI NDUGU ZAO TUPO NCHINI NA PENGINE WATARUDI SIKU MOJA,TUPATIENI MAONI KULINGANA NA UHALISIA WA HUKO,MSITUACHE TUDANGANYWE NA WANAO KUJA KUWASALIMU SIKU MBILI TU!


So, the need for the qualitative effort in Tanzania Education is as urgent as it is.Tunaipongeza Serikali kwa kuliona hilo! Ila Tanki lina mchango kidogo katika hili.

“Kikwazo cha Maendeleo ya Tanzania kwa sasa
SI IDADI YA WASOMI
BALI
NI KUTUPWA KWA UBORA WA ELIMU”.

Elimu kuwa bora ni lazima iwe na zao la uzalendo ndani yake!Bila hivyo ni ngumu elimu hiyo kulinufaisha taifa husika! Hata ukiangalia maana ya elimu kwa mujibu wetu wenyewe, na ukafananisha na tunayo yafanya si tu makazini,hata katika familia zetu,unaweza kuona ni WANGAPI AMBAO TUNA BORA ELIMU NA WANGAPI TUNA ELIMU BORA. HIYO HIYO ULIYONAYO,NI BORA KWELI?

Ukitumia  mfano wa Mwalimu Nyerere (Baba Wa Taifa), kuwa wote mnaweza kula rushwa,lakini mmoja kazi ikafikia ubora na mwingine hata isionekane.Mwalimu alituagiza kuwa rushwa zote tuzichukie kama ukoma, japo sisi huchukia zaidi pale ambapo kazi haikuonekana. Nafikiri ni vema basi tuchukie kazi kutoonekana na tuchukie zaidi kazi kuonekana lakini bila kufikia kiwango, maana sio tu kumetupotezea rasilimali,kodi zetu,muda, bali pia ni hatari kwa maisha kutumia kitu  kibovu! Na mara nyingi watu wanaotupatia Vitu vibovu huzaliwa na BORA ELIMU,ambayo huwa haina KUHESHIMU MIIKO WALA UZALENDO ndani yake! Na inakuwa na upandikizi wa MTAZAMO wa UBINAFSI saana! 

WE BISHA LAKINI HATA ALIYEFUNDISHWA KUPIKA AKIPUUZIA MIIKO,KELELE TU MEZANI! SIO MEZA HIYO! AHSANTE BA RIZI !

AU
“Kuna kitu kinaitwa mali ya UMMA. Kila mtu kichwani anamini kula ni sawa ila mbaya kukutwa! Ni kwa sababu mtu kaambiwa kuna mali ya UMMA bila hata kumjua UMMA ndiye nani HASA,basi hata kitu cha UMMA kinapoharibiwa mpaka akatafutwe UMMA aje azuie uharibifu huo,hata kama mamia ya waTz tunaona,elimu tuliyonayo haikutuambia UMMA NDIO SISI, haikutupatia fikra zenye UZALENDO na zenye  kuheshimu MIIKO ndani yake!”

BORA ELIMU HAITUFAI KABISA, TUPAMBANE NAYO ZAIDI YA TUNAVYOPAMBANA NA UKIMWI
NA
‘Kama elimu huikusaidii wewe na jamii yako kwanza ,maana yake ubora wake una mushikeri!’

Ubora kwa zama hizi, ni kama upendo,si kitu cha kusema utakigusa au pengine kukiona tu bali inatakiwa ukihisi kutoka rohoni! Hebu mfikirie fundi nguo anayekupatia nguo yako nzuri ya kuvaa harusini, baada ya siku yako ya harusi! Unafikiri ni fundi bora,hata kama nguo hiyo imefikia kiwango ulichokitarajia? Hata akikuambia amekusamehe malipo, bado hisia yako haitakuwa nzuri! Nyakati hizi huyo sio fundi bora. ‘UBORA WA KUNG’AA NA UDHAHABU UWEMO’,usitafute kwenye kamusi nimetohoa SI KILA KING’AACHO NI DHAHABU,na msemo huu hautoki kwenye mtihani.

Kukosoa mikakati iliyowekwa na serikali utakuwa uongo,yaani ni Ubongo Man”, kama Sharo alivyotuambia, Mungu aweke roho ya marehemu pema peponi! Ila kuchangia tu nafikiri ni muhimu na haswa ndio ushiriki wenyewe!

Shule na Vyuo maalumu nafikiri vitatusaidia, na pengine isiwe tu kwa ajili sayansi na teknolojia, bali iwe maeneo yote japo hata kwa baadae!Hawa Wanasayansi kwanza kwa sasa hawafui dafu kabisa kwa wanasiasa , sasa ni visuri tuboreshe na Siasa/Uongozi kwa ujumla au huko mambo safi?

Tutake tusitake utofauti upo,hivyo wenye vipaji vya madarasani wapewe nafasi yao kuvionyesha kama wale wa viwanjani na kumbini! Ukweli ni kwamba, tunapaswa kulinda na kuheshimu akili zetu kama tunavyolinda migodi ya Geita na kwengineko!

Kwa sababu hata migodi inahitaji akili na fikra za watu kwanza ili kutunufaisha! Tulianzisha Shule maalumu! Tujiulize Ziko Wapi? Zinaishia Wapi? Kwa nini? Matunda yake yako Wapi? Hatuwezi kutegemea kufanya mambo makubwa kwa juhudi ndogo? Kula bila Jasho mara nyingi kuna madhara makubwa kuliko faida!

Vyuo na Shule maalumu, vinaweza kujenga ushindani, na kuibua utamaduni wa ubora bila hata kutumia pesa nyingi. Nafikiri waliopitia shule hizo maalumu,hasa kati ya mwaka 1993 mpaka 2003 wanaweza kutoa ushuhuda wa hili. Na itakuwa rahisi kwa serikali kuona ifanye nini na kundi hilo dogo na maalumu kwa manufaa ya wengi! Upendeleo kama una maanisha manufaa ya wengi ni mzuri tu!Usiwanyime wanao wote kusoma,kisa anayeelewa sana darasani ni mdogo na mkubwa,atajisikia vibaya! Mpeleke mkubwa kwenye anachoweza zaidi,nani kasema kipaji cha uwezo darasani ndio bora kuliko vingine! Mbona Kuna walichukia darasa kwa sababu ya kuulizwa kila swali wao na wakafanya vizuria maishani kuliko waliofanya presentation mpaka za tafiti za kitaifa

Hatuwezi kuwa sawa, hivyo hatuna haja ya kuukwepa utofauti wetu ,bali tuubariki na kuuboresha,ili utuboreshee maisha badala ya kutuharibia.Ila MUENDELEZO NI MUHIMU SANA,SIO UMAALUMU MWISHO A’LEVEL/DIPLOMA TU! SIO SAWA HIYO.

Changamoto nyingine zilizoorodheshwa zinaweza kujibiwa na nguvu ya soko, kama vile,kwa nini matumizi ya Ngamizi yako chini!Waafunzi hawajiungi na masomo ya sayansi kulinganisha na  wanavyojiunga fani zingine. Ubunifu na ushindani katika ajira. Yote haya yanauhusiona wa moja kwa moja na kama soko la ajira na utendaji wa kila siku unahitaji hayo mambo kiasi cha kumlazimu mtu kuyatafuta au hata kupigia kelele kuwa apatiwe?

Nchi jirani Ngamizi na Simu za mikononi pengine ni bei rahisi kuliko Tz, kwa sababu zinasaidia sana kwenye masomo,sisi tunahitaji zaidi kitakachotusaidia kwenye FB,TWT na vingine kama hivyo!Hivyo hata ukiondoa ushuru wa kuingizia Kompyuta (neno rahisi kuliko Ngamizi,kweli vya wenzetu vizuri jamani) bei ishuke, sijui kama tutanunua zaidi  kuliko simu,ambayo full time kuchart na ‘mafacebook gal/boi/mumy/dady/bro/sis/cou…..’!

Juu ya Soko Huria La Afrika Mashariki! NO COMMENTS TODAY! Walimu waongezwe na idadi ya wanafunzi vyuoni iongezeke,HIYO 100 MZEE, ila vyote hivyo ni hatarishi kwenye ubora hivyo ni lazima viambatane na mfumo sahihi, kwa sababu HAVIKWEPEKI.

Na ieleweke kuwa Wanafunzi Tz na labda duniani kote kwa sasa sio tu kuwa hatutaki kujiunga na masomo ya sayansi, bali hata tuliosoma sayansi tunakimbilia Siasa na Biashara. Uliza SOKO LA AJIRA NA UJIRA, utapata jibu zuri tu huhitaji kundi kubwa kutafiti kwenye mataasisi.

Tena afadhali Serikali ilivyoleta mpango wa kupata mkopo ukiingia sayansi,sasa nitafanyaje?HATA HIVYO, jamaa shahada ya kwanza anapiga mambo ya Kilimo,(Mkopo) anaona kumbe dili ni kufanya kazi kwenye taasisi za kibiashara, anakopa mwenyewe sasa,  anasoma shahada ya pili biashara/sijua CPA na akimaliza tu anagundua kumbe mambo yatakuwa rahisi kwenye kampuni yake akiwa ndani ya siasa,hivyo anajiandaa kwenda Ph D / shahada ya Uzamivu sijui kwenye eneo hilo. Unafikiri nani anapenda kuona anaumia sana halafu analipwa kidogo, na umri wa kufa unazidi kushuka?



NGUVU YA SOKO IMESHIKA HATAMU, uelewe mitaa, la sivyo utakuwa unaona wenzio wanapita we hujui pa kuanzia wala pa kutokea,SIJUI alimaanisha hivyo, FID Q. Nguvu ya Soko inaongoza rasilimali zipi, wapi na jinsi gani zigawanywe. Kijana mwenye AAA katika PCB na PCM anashauriwa na mzee wake (Pro wa Hesabu/Dakt) kuwa mwanangu soma Masomo ya Uhasibu/Sheria usije ukawa kama mimi! Huu ni WITO! Swali ni Nani akasome Hizo Hesabu na Upasuaji? Mwenye AAA ya KLF?

Ni yaleyale tu ila kwa mtindo ungine, zamani wazee walichezea madini bao wageni wakaja wakawapatia gorori wakachukua madini, sasa pia tunachezea akili kali tulizopewa badala ya kuzalishia na wageni watakuja,watatuletea makopo ya Kompyuta na TV halafu wanandoka na akili kwenda kuzalishia kwao! ASUBUHI MPAKA JIONI TUNAHANGAIKIA JINSI GANI TUTAWAINGIZIA PESA WAO TU Wakati umefika Serikali ithamini Akili Kali na kuzitunza na kuzitumia kwa manufaa ya UMMA japo za wachache! Kama huoni umuhimu wa akili, Jiulize; mimi ningekuwa raisi wa kwanza TZ ingekuwaje leo? Sio mimi Wewe?

SULUHISHO LA HILI

Tiba ya haya ni pamoja na Kubadili Mtazamo juu ya Elimu, Tuufanye ubora kuwa utamaduni wetu kuanzia majumbani, mashuleni mpaka vyuo vikuu! Ni vipi? Tutumie mfumo wa menejimenti kwa kuangalia ubora utokanao na ujumla wa ushiriki wa wahusika (Total Quality Management). Katika mfumo huu, mteja anapewa nafasi kwanza ya kuamua juu ya ubora unaopatikana, na nafasi ya pili kuwa kila muhusika ana jukumu la kusaidia kuupata ubora huo,bila hivyo ni ngumu kuufikia huo ubora na tatu ni kuwa katika utendaji, kila mtu ni mteja wa mwenzie,na kila mtu ana jukumu la kuhakikisha mteja wake anaridhika kabisa na anachokipata.

Mfumo si mgeni duniani, umeanzia kwenye viwanda huko Jepu,umesaidia hadi Yuesiei tokea mpaka kwenye ujenzi, na sasa sekta za elimu zinanufaika pia!

Mfikirie mwalimu wa darasa la kwanza anapowafundisha watoto kama wateja wake na huku akimchulia mwalimu wa darasa la pili kama mteja wake wa ndani wa pili. Kwa kuhakikisha mwalimu wa darasa la pili asipate shida hata kidogo atakapowachukua wanafunzi hao mwakani,na wengine vivyo hivyo, vipi matokeo ya la saba! WATOTO WENYE ELIMU BORA YA MSINGI na SIO BORA ELIMU YA MSINGI.Na kikubwa kabisa swala hili ni endelevu kwa kuwa mfumo huu unaamini kuwa siku zote kuna mahali panahitaji uboreshaji hata uwe katika mafanikio kiasi gani,ndio maana leo hii hata maanchi makubwa bado yanatafiti nap engine ndio maana sio ajubu kuona matajiri wanaendelea kupunguza muda wa kulala wakati mafukara tunaongeza muda wa kupoteza.

Kwenye elimu,mteja mkuu ni jamii nzima, na wateja kwa ndani ni mwanafunzi na mwalimu,kila mmoja ni mteja wa mwenzake! Na hivyo zao la shule  ni wanafunzi wanaomaliza,jamii ndio itatoamajibu kama inaridhishwa na ubora au la! Hivyo mwanafunzi anayemaliza na kufaulu vizuri huku ni mwizi wa kupindukia jamii itasema hatufai,ikimaanisha hana ubora wa kuifaa jamii! Marekebisho yatarudishwa mpaka chuoni. Wakati kwa  ndani,kama mwalimu atakuwa kila wakati anahakikisha mwanafunzi wake ni mteja kwake, maana yake yeye hayupo kama mwanafunzi hayupo,na mwanafunzi vilevile.Faida za mfumo ni nyingi kuliko ugumu na hata kama itachukua muda mrefu kidogo kutoa majibu,lakini UBORA UKIWA MBELE KILA KITU KINAWEZEKANA KAMA JEPU AU YUESIEI, “ UBONGO ”?

“NAJUA TAYARI INAONEKANA NI NDOTO, HII NI KAMA MADIWANI KUHUSIKA KWENYE MIRADI MBALIMBALI YA JAMII! HATA KAMA KUNA MATATIZO KIDOGO BADO NI BORA KULIKO KUTOHUSISHWA, MAPUNGUFU YANAREKEBISHIKA,WALE NI WATEJA WA MWISHO HIVYO WANASHIRIKISHWA ILI KUONA KAMA UBORA NDIO WANAOUHITAJI?SAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAFI”.

“HEBU TUSAIDIANE, NI NCHI GANI ILE WALIBAHATIKA KUPATA MAENDELEO?”

ZAID JUU YA TQM IN EDUCATION: (Mpangule, J.A. (2009). Total Quality Management application at Ardhi University. Dar Es Salaam: Unpublished Postgraduate Dissertation Report at ARU.

ASANTE MDAU KWA KUWA MMOJA KATI YA EFU MOJA WATAKAOFIKA HAPA CHINI! LAKINI UMESOMA UMESCROLL?

            Kama mdau, Maoni yako nini Juu ya hili!

0 comments:

Post a Comment