Sunday, September 30, 2018

Mchezo wa Kirafiki wa Mpaju FC "Simba vs Yanga´"

Simba na Yanga ni timu kubwa sio tu Tanzania, bali hata Afrika ya Mashariki. Homa ya mchezo baina ya timu hizi mbili zenye utani wa jadi, huleta joto la kiushabiki kuanzia kwa watoto mpaka wazee,
na hata baina ya wachezaji ndani ya vilabu vingine vya mchezo wa soka nchini Tanzania.Mpaju FC, ina utamaduni wa kuwa na mchezo unaowakutanisha wachezaji wa timu hii washabiki wa timu hizi, kama sehemu ya mazoezi ya siku chache kabla watani hao kucheza. Makundi yote ya Mpaju FC hupambana kama watani Simba na Yanga.

Mbali na mazoezi, mechi hii hutumiwa kama sehemu ya kuimarisha utani na urafiki baina ya wachezaji na wadau wa Mpaju FC. Hata hivyo kuna wakati faida huweza kuwa ndogo, kwa sababu wachezaji hupanda munkari kiasi cha kukasirikiana. Hili limekuwa tatizo kubwa la uwepo wa mchezo huu

Leo pia, kulifanyika mapambano mawili, yaani kati ya mashabiki simba na yanga wa Mpaju FC U-21 na U-12. Pamoja malalamiko ya Yanga U21 kufuatia kufungwa 2-1, mchezo ulikuwa mzuri na wenye kuvutia ukishuhudia hatua kubwa iliyokwisha fikiwa na MpajuFc U-21 kwa ujumla.Makapteni wa timu hizi, Rajabu Ndelele (Mpaaju FC Simba) na Steven Mapunda (Mpaju FC Yanga) walikubali kuwa huenda matokeo siku inayofuata baina ya watani halisi ikawa hivyo pia. Kivutio kikubwa ilikuwa mchezo wa U-12, ambao ulijaa ushindani na ufundi wa hali ya juu. Mchezo huu uliisha kwa matokeo, ya Suluhu ya 1-1, na kupelekea kupigwa kwa mikwaju ya penati na kushudia Simba kushinda pia baada mikwaju 7 kupigwa na timu ya Mpaju FC Yanga kupoteza mikwaju 4 dhidi ya 3 ya wenzao. 

Baadhi ya Picha zinazoelezea tukio zima kwa kifupi ni hizi hapa chini, na video unaweza kuziangalia kupitia Mpaju Sports You Tube Channel
Vikosi vyote viwili vya Mpaju FC U-12 Simba na Yanga

Makepteni wakiwa na Kocha Dulayo





Vikosi vya Mpaju U 12 vikisubiri upigaji wa Penati
 



0 comments:

Post a Comment