KIKOSI CHA MPAJU ATINISU KILICHOLETA USHINDI NA KUSHIKA NAFASI YA TATU

Hawa ndo vijana walio tung'arisha na bado wanahamu ya kufanya zaidi ya hapa...

Kikosi toto cha Mpaju SC

Hiki ndicho kikosi cha Mpaju SC upande wa watoto kikiwa kwenye ziara katika shule ya msingi Mpolo.

Mpaju FC wakiwa kwenye Picha ya Pamoja

Mpaju FC wakiwa kwenye Picha ya Pamoja wakati wa Tamasha la Mpaju Week 2019 Uwanja vya Magereza Mbeya.

Monday, July 22, 2013

SONGEA

Inauma kusikia, Songea imeumia.
SONGEA: Mwaka 1991, Yusuph Mayanga, Juma Ahmed Mpangule na Hamidu Abdalah

Nimekumbuka Songea, nimeshindwa vumilia.
Mfaranyaki tokea, majimaji tembelea.
Bombambili pandishia, Matarawe potelea
Inauma kusikia, Songea imeumia.

Sunday, July 21, 2013

SWAIBA KAMATA NJIA


“Swaiba kamata njia, Mimi nakusubiria”
Kama ndoto nakwambia, Siku hii kuwadia
Nauli imetimia, Sasa tuache kulia.
Hebu tiketi chukua, Nini wasubiria
Swaiba kamata njia, Mimi nakusubiria.

Wednesday, July 17, 2013

Mchumi wetu Mchumi, Mchumi acha umimi



Mchumi huyu Mchumi, Mchumi wetu mmimi.
Apanga mambo kivumi, Apangavyo si kichumi.
Kupanga huku uchumi, Kupanga gani Mchumi.
Mchumi wetu Mchumi, Mchumi acha umimi

Sunday, July 14, 2013

KANDANDA LA BONGO




Vijana waende ng’ambo, Liwe letu kuu JAMBO.

Fimbo tangia kitambo, Kwao TFF ni wimbo.
Bora wale wa kitambo, Waliweza wetu wimbo.
Wa leo twaona mambo, Na Mengi yao majigambo
Vijana waende ng’ambo, Liwe letu kuu JAMBO.

Monday, July 8, 2013

BAJETI YA TANZANIA 2013-14: Kama kupanga ni matumizi,WAKULIMA TUMO!



"Upenyo Sahihi wa kuboresha Bajeti ni kupitia Kuongeza Makusanyo Yetu".

Kila mtanzania ana haki ya kusema moja au kadhaa kuhusu bajeti ya nchi yetu maana kwa namna moja u nyingine itakuwa inamgusa tu! Wengi wameitazama kwa jinsi wainavyo, na kuitathmini kwa jinsi waonavyo kuwa ndio sawa!

Saturday, July 6, 2013

KISWAHILI



„KISWAHILI Muhimili, Ni Roho mengine mwili“

Kiswahili Kiswahili, Hebu wote tujadili.
Vifimbo Cheza wa hili, Mudahili Umahili.
Daima tunajadili, Madini si Kiswahili.
 KISWAHILI Muhimili, Ni Roho mengine mwili .